Kwanini Polisi wanapomshikilia mtu wanakimbilia kwenye simu na Laptop yake?

Kwanini Polisi wanapomshikilia mtu wanakimbilia kwenye simu na Laptop yake?

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Amani iwe nanyi Waungwana!

Mimi swali langu ni Short and clear, huu utaratibu wa Polisi kushikilia mtu kisha wanabeba na simu yake pamoja na Laptop yake, wanataka nini hasa? Ni sheria gani inayoruhusu wao kuingia na kufungua simu na computer zangu bila ridhaa yangu wakati mimi ni mshukiwa wala siyo mkosaji?

Tuseme sawa, baada ya kumuachia mtu kwa dhamana wanaendelea kukaa na vifaa vyangu vya nini? Usalama wa vifaa hivyo mwenye uhakika navyo ni nani?

Nijuavyo mimi ni kwamba ukimkamata mtu na properties zake muda huo anatakiwa kukabidhi kwa maandishi na zihesabiwe. Sasa hii ya kunyang'anywa kwa nguvu inatoka wapi?

Wanasheria mnaweza kusaidia kutoa lesson kwenye hili jambo kwetu sisi maamuma wa sheria. Sheria ya Cyber ya 2016 inasemaje?
 
Na hasa polisi wa Tanzani, lengo kuu ni kuwapigia simu watu wako wa karibu ili kuwaomba hela
 
Polisi ni sehemu ya wizi. Hapo utakuta wameshagawana vitu vyako tayari. Ndiyo maana Hamza hakuchelewa, aliwafikishia ujumbe mapema.
 
Kama wanagawana hadi nyama vipi kuhusu computer na laptop
 
Back
Top Bottom