Kwanini raia wa kigeni wanapewa kadi za NIDA na pasipoti za Tanzania?

Kwanini raia wa kigeni wanapewa kadi za NIDA na pasipoti za Tanzania?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Mnaofahamu tusaidieni utaratibu wa kupata kitambulisho cha NIDA na Pasipoti incase hata wageni wanaruhusiwa kupata.

Kuna wageni wanafanya biashara na kuajiriwa hapa nchini awali walikuwa na Pasipoti za Kigeni lakini siku hizi Wana Pasipoti za Tanzania kwenye makampuni Yale Yale na TRA taarifa za awali zinasoma ni RAIA WA Somalia, Kenya, Uganda, Yemen , Msumbiji nk

Hawa watu wanapataje uraia mbona tukienda kwao Pasipoti hatupewi kirahisi? Viongozi waliopewa dhamana yakulinda ajira zetu wazawa wanafanya kazi yao inavyotakiwa?

Je, maafisa wa chini wanaweza kutoa NIDA au cheti cha kuzaliwa au Pasipoti Kwa mgeni Bila wakubwa kujua? Mgeni anawezaje kuwa na kuzaliwa nje ya nchi lakini kwenye Pasipoti anaandikwa amezaliwa Tanzania?

Kwa hali inavyotokea sasa ya makundi ya kigaidi upo uwezekano viongozi wanaotoa vyeti vya kuzaliwa, NIDA na pasipoti wakawa wanatumika kutengeneza documents za kugushi kuwapatia Pasipoti wageni wajiunge na maaramia kwenye vikundi vilivyopo mataifa jirani.

Mimi nadhani eneo hili liangaliwe upya kuna shida na kama mamlaka zinazohusika hazijajua basi watambue wageni wengi Sana wanashirikiana na viongozi kupata Pasipoti yetu.

Nimeandika Uzi huu baada ya kuona Tanzania tumeanza kuwasaidia Diaspora kupata Pasipoti kupitia balozi zetu. Huku nje ya nchi sina shida, napata shida na viongozi waliopo huko bongo hasa kurasini ambao tukienda Sisi wanataka Hadi vyeti vya kusoma PhD ila wakienda watu wenye rangi rangi na umate umate wanapita moja Kwa moja kwenda Kwa wakubwa hata foloni hakuna kupanga kudadeki.

Mwamba unamjua kabisa huyu tumesikia naye south akiwa raia WA Somali mkombizi ila akishajichanga anaenda Kwa wadosi bongo kurasini asubuhi jioni anakitabu.

Wengine wapo hapo Zambia wamekaa wakizaa tu wanaipeleka watoto bongo wakachukie Pasipoti, huu ni upumbavu mnatufanyia Sisi weusi wenzenu ila nawaapia mnatengeneza bomu msipokubali kubadilika.

Hizo pesa walizonazo hawa wageni za kuwa na Pasipoti na hata mkiwakamata wamedanganya mnawaomba waondoke taratibu zitawatokea puani one day.

Sisi huku nje tunavyoteseka kukaguliwa hatuna hamu kabisa, kisa kuna wanigeria na wasomali wachache Wana Pasipoti zetu kimagumashi wanatunyima Amani airport za watu tunaonekana wote kanjanja Tu.

NIDA weusi tuna namba wenye rangi mnawapa vitambulisho poa.

Watu wa vyeti vya kuzaliwa watoto wetu vyeti kupata shida ila vya wageni mnatoa tena kwakuwafanya wazaliwe Tanzania wakati siyo wazaliwa wa Tanzania poa.

Magresheni mnadanganywa mnatoa vitabu Kwa wageni poa.

Ila lindeni Tanzania, vipesa mnavyopewa vinaweza kuingamiza Tanzania. Hao wanaoghushi awaitakiii mema Tanzania watailipua tuilinde. Hasa ninyi viongozi mnaosimamia utoaji wa Pasipoti. South inateketea Kwa kuwa na Wana rushwa kama Tz. Chukieni hii piteni kariakoo, kagueni wafanyabiasha wa Kigeni mtagundua TRA Wana NI wageni Uhamiaji ni Watanzania.

Unganisheni system zenu mtagundua uozo uliopo.
 
Mamlaka husika zijitafakari.

Kadi ya NIDA Ni kwa wazawa tu. Labda kama Sheria imeboreshwa kuruhusu raia wa Kigeni.Mkurugenzi Mkuu NIDA jitafakari kama kweli ushahidi upo wa kutoa kadi kwa raia wa kigeni, wakati raia wa Tanzania wamepewa namba za NIDA miaka mitatu lakini hawajapewa kadi.

Passport za Tanzania kuwa kwenye mikono mwa raia wa kigeni,ni jambo la hatari mno.
Mamlaka husika zijitafakari.

Ninashauri kama kuna ushahidi, orodha au jina la raia wa kigeni mwenye kadi ya NIDA na passport ya Tanzania,
Orodha ipelekwe/jina lipelekwe kwenye Mamlaka husika,nakala Waziri mwenye dhamana na taasisi hizo
 
Naona unajichanganya mtu akipata passport ya Tanzania sio tena raia wa nje. Maana yake ameomba uraia na kupewa kisheria. Hivyo sio kitu cha ajabu mtu kuanza kama mgeni na kuomba uraia. Waomba uraia sio wakimbizi tu.
 
Mamlaka husika zijitafakari.
Kadi ya NIDA Ni kwa wazawa tu .Labda kama Sheria imeboreshwa kuruhusu raia wa Kigeni.Mkurugenzi Mkuu NIDA jitafakari kama kweli ushahidi upo wa kutoa kadi kwa raia wa kigeni, wakati raia wa Tanzania wamepewa namba za NIDA miaka mitatu lakini hawajapewa kadi.
Passport za Tanzania kuwa kwenye mikono mwa raia wa kigeni,ni jambo la hatari mno.
Mamlaka husika zijitafakari.
Ninashauri kama kuna ushahidi, orodha au jina la raia wa kigeni mwenye kadi ya NIDA na passport ya Tanzania,
Orodha ipelekwe/jina lipelekwe kwenye Mamlaka husika,nakala Waziri mwenye dhamana na taasisi hizo


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Ingia tovuti ya NIDA ujifunze, mbona NIDA inaruhusiwa hata kwa wakazi wasio Raia?? Ipo kisheria.
 
Haiwezekani ukazaliwa Kenya then ukaja kupewa cheti cha kuzaliwa Tanzania kwamba umezaliwa Ilala

Hatuna utaifa Pacha ndio maana wakina Kibatala wameenda mahakamani, means kuna viongozi wameweka maslahi binafsi mbele kuliko maslahi ya Taifa...

Taratibu zikiguafwa hakuna mgeni atapata Pasipoti kinyime cha sheria.

Mtu anakuwa Tanzania na Pasipoti ya Tanzania, ukimkuta Lusaka au South ana Pasipoti ya Kenya au Somalia au Uganda how?

Lengo letu nikuweka habari habari naamini mamlaka zina njia zake zakufuatilia na kuchukua hatua ikiwemo kutumbua wanashindwa kurizika na kidogo wanachopata Hadi wanatumia madaraka kuuza nchi.

Peleka majina ya wageni kwenye hizo malka uone kama watakamatwa........watakachofanya nikuwaambia wasepe . Tumeshapeleka mara kibao wakipata ukweli unasikia nenda kwenu uje na Pasipoti yako wakati Pasipoti wanayo.....

Tusiposema tutakuwa tunaliteketeza Taifa; vita vilivyopo mataifa jirani vilichangiwa na hizi rushwa ndogo ndogo na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Taasisi nyeti za umma zinakula rushwa wazi kabisa, ni rushwa na kukosa uzalendo kwa taifa watu wanataka mafanikio chap kwa haraka akuna kulala.
 
Mamlaka husika zijitafakari.
Kadi ya NIDA Ni kwa wazawa tu .Labda kama Sheria imeboreshwa kuruhusu raia wa Kigeni.Mkurugenzi Mkuu NIDA jitafakari kama kweli ushahidi upo wa kutoa kadi kwa raia wa kigeni, wakati raia wa Tanzania wamepewa namba za NIDA miaka mitatu lakini hawajapewa kadi.
Passport za Tanzania kuwa kwenye mikono mwa raia wa kigeni,ni jambo la hatari mno.
Mamlaka husika zijitafakari.
Ninashauri kama kuna ushahidi, orodha au jina la raia wa kigeni mwenye kadi ya NIDA na passport ya Tanzania,
Orodha ipelekwe/jina lipelekwe kwenye Mamlaka husika,nakala Waziri mwenye dhamana na taasisi hizo
Hata mimi nina rafiki zangu watatu ambao si Watanzania kwa maana yoyote ile lakini wana ID za NIDA.
 
Ila vijana wa kitanzania starehe zitatuponza sanaa tunapokea rushwa kwaajili ya tamaa hatuangalii tena maslahi ya nnchi tunachowaza ni kwenda kidimbwi na wavuvi kempu kuvimba.
 
Mkuu mtoa hoja upo sahihi kwa mawazo yangu ila relax, hii issue ipo more complicated kuliko unavyoiona,ngoja nikuulize swali wewe mtoa hoja,nijibu honestly na usinielewe vibaya, wewe mwenyewe nitakutambua vipi kama wewe ni raia wa nchi hii? Kutokana na maelezo yako inaonekana umetembea hasa huku kwenye SADC, wenzetu wanatambuana kwa IDs ambazo zipo wired kote kuanzia police, banks, maduka ya kukopeshana,hospital's, licenses etc etc na hii imetokana na kuwa na systems inayoongea, mtoto akizaliwa wazazi wanampa Jina mfano Nkanini, na serikali inampa Jina, ID number, hii number atakufa nayo, hapa eti NIDA ina ukomo! Bado mkuu na bado sana.
 
Ila vijana wa kitanzania starehe zitatuponza sanaa tunapokea rushwa kwaajili ya tamaa hatuangalii tena maslahi ya nnchi tunachowaza ni kwenda kidimbwi na wavuvi kempu kuvimba.
Taifa limekuwa la wakata mauno tu

Ova
 
Inasikitisha sana unakuta pale uhamiaji wahindi wapo kwa makundi na wapakistani kusubiri passport za michongo wengine mpaka ujificha chooni.Tanzania tuwe wa wazalendo
 
Mkuu mtoa hoja upo sahihi kwa mawazo yangu ila relax, hii issue ipo more complicated kuliko unavyoiona,ngoja nikuulize swali wewe mtoa hoja,nijibu honestly na usinielewe vibaya, wewe mwenyewe nitakutambua vipi kama wewe ni raia wa nchi hii?,kutokana na maelezo yako inaonekana umetembea hasa huku kwenye SADC, wenzetu wanatambuana kwa IDs ambazo zipo wired kote kuanzia police,banks, maduka ya kukopeshana,hospital's, licenses etc etc na hii imetokana na kuwa na systems inayoongea, mtoto akizaliwa wazazi wanampa Jina mfano Nkanini, na serikali inampa Jina,ID number, hii number atakufa nayo, hapa eti NIDA ina ukomo!!!,bado mkuu na bado sana
Ninyi mnaojua ndo mtusaidie sasa, tutarelax kwenye matatizo? Kwa mtu ambaye amewahi kusoma madhara ya wageni kuwa ignored na system hasa south Afrika akiona na Sisi tunaleta ujamaa kwenye masuala nyeti ya uraia lazima aumie

Kama kuna kitu cha kulinda Kwa gharama zote ni Utanzania wetu. Tupo kwenye angle ambayo ni hatarishi Sana tumezubgukwa na majirani wenye wivu mkubwa wakitaka Tanzania iingie kwenye machafuko.

Tukiwa wazalendo tukasimamia utumbuaji wa yeyote anayechezea utanzania wetu tutakuwa tumefanya kazi kubwa kuliko hata kujenga reli.

Pasipoti inakqenda kuzalisha watu kibao wasio na sifa za utanzania. Watu hao kwakuwa Wana mataifa Yao awachelewi kutuachia chokochoko tukauana na kuvunja hata reli na barabara.

Tuilinde Tanzania Kwa kuzuia yasitupate ya South Afrika. Let us think about kibiti saga....ule ni mfano wa kukubali kuingiliwa

Nina hasira mjue.....ogopeni Sana kitu kinaitwa XENOPHOBIA
 
Mwaka flani zilitangazwa nafasi za kazi wakaomba maelfu ya watu; serikali ilipoona Ile fedhea siku hizi wanatangaza na kufanya short listing kimya kimya kukwepa fedhea.

Nini tafsiri ya wimbi kubwa la vijana kukosa kazi? Idle mind always inawaza uovu. That's y wakija kugundua wao hata fursa yakusafiri nje wamenyimwa, ajira zimekaliwa na wageni na wageni wanapewa bendera ya Taifa (Pasipoti) wakaiwakilishe nchi nje basi na wao watageuka wezi, majambazi, wauaji na kila roho ya ukatili.

Tunalo BOM jamani ; muulizeni Balozi wa Tanzania South Afrika situation ipoje Kwa sasa. Chukieni maafisa magresheni na NIDA wapelekeni hata bhapo bongo ubalozi wa South wakajifunze " impact ya utoaji WA uraia kiholela" watawaambia. Au wapelekeni south wakajionee
 
Mamlaka husika zijitafakari.
Kadi ya NIDA Ni kwa wazawa tu .Labda kama Sheria imeboreshwa kuruhusu raia wa Kigeni.Mkurugenzi Mkuu NIDA jitafakari kama kweli ushahidi upo wa kutoa kadi kwa raia wa kigeni, wakati raia wa Tanzania wamepewa namba za NIDA miaka mitatu lakini hawajapewa kadi.
Passport za Tanzania kuwa kwenye mikono mwa raia wa kigeni,ni jambo la hatari mno.
Mamlaka husika zijitafakari.
Ninashauri kama kuna ushahidi, orodha au jina la raia wa kigeni mwenye kadi ya NIDA na passport ya Tanzania,
Orodha ipelekwe/jina lipelekwe kwenye Mamlaka husika,nakala Waziri mwenye dhamana na taasisi hizo
NIDA sio kwa wazawa tu mkuu hata wenye permanent residence wanahaki hiko kiufupi NIDA zipo aina zaidi ya mbili hivyo tofauti yeye anaweza asiwe indicated kama RAIA ila kwenye kadi akawa indicated kama mkaazi wa kudumu n.k
 
Back
Top Bottom