Kwanini raia wa kigeni wanapewa kadi za NIDA na pasipoti za Tanzania?

Mkuu nimekuelewa haswa ila hapa tulipofika kama nchi ni kama cancer ambayo ipo stage 4 ,mgonjwa lazima atakufa, Tanzania hii inahitaji generation mpya ya viongozi ili kuinasua nchi, wazo langu hii wizara ya mambo ya ndani ni dude kubwa sana, mimi ningeligawa kuwa na police ministry na home affairs (uraia &immigrations ),sheria nyingi za kikoloni ningezifuta, nchi tungetengeneza systems mpya na inayoongea na dept zote nchini, mtoto hawezi kupata ID kama hana birth certificate iliyondani ya systems ya nchi, passport zitaombwa tu kwa wenye ID book, yaani unakwenda pale kurasini na 🆔 book ONLY kuomba passport, uchafu mwingine tupilia dampo la tabata
 
Ila bado hujanijibu swali nililokuuliza ,ukijibu ndio utajua tatizo lipo wapi?,je wewe ni raia wa nchi hii?na nitakutambua vipi kama ni mtanzania?
 
Mkuu., Zipo kadi za NIDA za aina mbili..

1.Kadi kwa raia (CITIZENSHIP CARD). Hii inatolewa bure kwa kila Mtanzania mwenye sifa stahiki.

2.Kadi kwa mgeni mkazi(LEGAL RESIDENCY CARD). Hii inatolewa kwa mhusika kwa malipo maalum kabisa katika mfumo rasmi wa NIDA.
 
Mkuu utakufa na stress zako bure tafuta pesa usomeshe wanao, hii nchi sio yako ina wenyewe, tulishawahi kutawaliwa na mkimbizi na viongozi wa juu wapo wengi ni wakimbizi wana nguvu hata kuliko babu yako.
Umeniumiza sana!
Yaani kile ambacho mimi kwa mawazo yangu nilikuwa nadhani kuwa ni hisia zangu tu za kijinga, wewe umeki-confirm kwa kunijulisha kuwa hisia zangu si za kijinga bali ni ukweli! Umeniumiza sana
 
Sheria zipo na kila nchi zina taratibu zake
Kuna nchi huwezi kupata Uraia hata uishi miaka 100 au izaliwe huko
Na kuna nchi ukikaa miaka 7 tu unapata Uraia

Wewe washangaa kadi kuna watu wana silaha za moto kwa mujibu wa sheria za nchi wanaruhusiwa huku wengine wakiwa na Resident permits tu hata sio passport wala NIDA

Watu wengi hawajui maisha yanavyokwenda duniani
Mtu anasema ooh nchi yetu usalama wake uko hatarini [emoji1] [emoji1787]
Kwa lipi mnafikiri intelligence imelala?

Basi Rishi na Suella na Sadiq Khan wasingepewa post kubwa hivyo mpaka PM,waziri wa mambo ya ndani na Mayor wa jiji la London

Hatuna hata kiwanda cha toothpicks halafu tunalia na usalama

Watu wamekuja kuchuma hela na kupambana nani ana shida na mambo ya siasa uchwara
 
Naona unajichanganya mtu akipata passport ya Tanzania sio tena raia wa nje. Maana yake ameomba uraia na kupewa kisheria. Hivyo sio kitu cha ajabu mtu kuanza kama mgeni na kuomba uraia. Waomba uraia sio wakimbizi tu.
Hivi unafahamu prosese za mtu kupewa urai au unajilopokea tu, maana wabongo kila kitu wanajua
 
Watoto wa Mbowe na Lissu ni raia wa marekani, lakini Wana vitambulisho vya taifa vya Tanzania na passport za Tanzania
 
Hivi unafahamu prosese za mtu kupewa urai au unajilopokea tu, maana wabongo kila kitu wanajua


Vijana wa siku hizi wajinga jinga mimi nimeanza kwenda US 1997 mpala leo sijui utaratibu wa Uraia wa Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…