#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Mimi na familia yangu hakuna atakaechanjwa iwe jua iwe mvua
 
Ndo shida ya wazanzibar hawawezagi kufikiria Bila waarabu
 
Yuko sahihi kabisa maana lazima ashauriwe kitaalam ili ajue ni njia ipi sahihi tunatumia, kama hujafanya utafiti huna mamlaka ya kusema lolote , huyu sio kama jiwe anasikiliza ushauri na anaongeza na zakwake baada ya kuambiwa, hapa Rais tunaye nyie masalia ya chattle mwacheni mama afanye kazi .
 
Mataga na wapiga vigelegele wa Sukuma gang mnapita katika kipindi kigumu sana.

Ghafla mmegeuka kuwa wapinzani. Hahahahaha
Mabavicha nao wamekuwa wapiga vigelegele wa ccm
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Unadhani hii inampa faida nani?
 
Mataga na wapiga vigelegele wa Sukuma gang mnapita katika kipindi kigumu sana.

Ghafla mmegeuka kuwa wapinzani. Hahahahaha
Mkuu, toa mchango na sio kutanua wigo wa ukabila na kudhalau kabila la mwingine, Okey, licha ya hivyo Kweli hao jamaa Wana makabila mengi ya kutaniana

Lakini embu toa mchango wako hapo Achana na utani mahali pasipo stahili
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Mkuu unajuaaje wanakufa wengi kukiko Tanzania wakati sisi hatuna data ya wagonjwa wala waliokufa kwa Covid?
 
Chanjo ni hiyari zije tu!
 
Unalaumu bure,hiyo covid yenyewe mpk
Leo dawa haijapatikana ambayo ni sahihi
Au ulitaka mpigwe lockdown
Kama tahadhari kuchukua siyo mpaka uambiwe

Ova
Japan hawana lockdown, South Korea hawana lockdown na nchi nyingi ila viongozi wao wanahimizana kuchukua tahadhari.

Sisi kiongozi anasema amemuachia mungu, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia corona isimuue?

Kama kuchukua tahadhari sio lazima uambiwe, nini maana ya kua kiongozi? Unaelewa maana ya mtu kuchaguliwa awe kiongozi? Ama unaelewa nini maana ya neno uongozi, kuongoza
 
Cha umuhumu tudungwe Chanjo,Mama anastahili Pongezi kwa kutujali Watanzania
Sasa hilo nalo linahitaji kuunda kamati ya corona ndio imshauri? kinachofanya hadi sasa asiseme tuvae barakoa kwa kuanza na yeye ni kwamba hadi apate ushauri kwenye hiyo kamati?
 
Mtani Ruta . Rais Samia yuko sahihi kabisa . Hili jambo halitaki siasa wala mzuka. Nilishangaa mwaka Jana boss (RIP) alipotaka kuongelea hali ya Corona nchini. Badala ya kuita wataalamu wa afya, aliwaita wakuu wa vyombo vya Dola . Huyu ametaka kuwashirikisha wataalamu wahusika wa tatizo lenyewe.

Kinachowasumbua nyinyi wafuasi wa Jiwe ni kuwa hamuamini kuwa Jiwe limedondoka na halinyanyuki tena . Huyo amepita na zama zake.

Hata Magu enzi za Mkapa na Kikwete hukumsikia akisema neno. Lakini alipoingia akawananga . So is normal

Odhis *
 
Hahah raha sana kuona CCM wao kwa wao wanarushiana mawe...
 
Kenya wanaofuata COVID19 protocols wako wapi?
Je hamsikii hosptali na mfumo wa afya ulivyozidiwa?
Mbona bongo tunaishi na vizuri tu na maisha yanaendelea kama kawaida?
Tunataka maisha gani zaidi?
Pengine unataka kumfuata Magufuli sawia na Watanzania wengine kibao waliotangulia mbele ya haki kutokana na janga la COVID 19?! Kuna Watanzania wengi sana wamefariki kwa COVID 19 tena unreported, ndugu. Muache Rais Samia Suluhu asafishe nchi dhidi ya COVID 19.
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Unasema wanakufa kwasababu wanazo takwimu nyie hata kama mnakufa kwa korona hamtojua.
 
Sasa hilo nalo linahitaji kuunda kamati ya corona ndio imshauri? kinachofanya hadi sasa asiseme tuvae barakoa kwa kuanza na yeye ni kwamba hadi apate ushauri kwenye hiyo kamati?
Mama hataki kuwa Dikteta anataka kila jambo ashauriwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…