Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Unaweza kumuona hana mvuto kw sababu watu wanatoa maoni yao be it positive or negative. Jiwe kwa vile alikuwa na upande mmoja wa kusifia (wapingaji walikomeshwa) unaweza kuona kuwa Jiwe alikuwa na mvuto, lkn kumbe hakuwa na mvuto wowote maana upande wa kukosoa ulinyamazishwa
 
Mwacheni mama yetu samia afanya kazi zake vizuri
Mama samia ni mkarimu sana
Mama samia ni mpenda haki
 
Hamna Rais humu, uliona wapi Rais naye analalamika kama wananchi badala ya kutoa ufumbuzi!
kuna utofauti mkubwa kati ya raisi kiongozi na raisi mtawala ...... mara zote raisi kiongozi kama samia huwa anamsaada kwa wananchi nanafuu kwa wananchi wote ndio maana we unaweza kumkosoa na wala isiwe shida na kauli ni ya amri lakini linatumika neno 'naomba' kwa maana ileile ya amri lakini ombi la kiongozi kumbuka ni amri ili linakuwa lina beba ustaarabu
sio kama kauli za tofali samahani nimekosea nakusudia jiwe yeye hana ustaarabu matokeo yake ndio katusababishia mpaka deni la taifa limezidi mara milioni yaani sijui alikuwaje yule bwana
 
Bila kufokewa hamuendi nyinyi
 
Wangapi watafukuzwa kwa kulaghai? tafakari.
 
Acha uongo, wakati wa JPM jamii forum, Facebook, Instagram na Twitter zimetumika kikamilifu kwa watu kutoa maoni yao positive na negative. Twitter na Jamii forum ni mitandao iliyoongoza kwa Uhuru wa watu kutoa maoni ambayo asilimia kubwa yalikuwa negative dhidi ya serikali. Lakini kiuhalisia JPM alikuwa na mvuto kwa kundi kubwa la watu wa tabaka la chini ambao siyo wadau wakubwa wa mitandao ya kijamii.
 
Ikiwa una msongo mkubwa wa mawazo kila kitu kwako kitakosa mvuto... waweza hata kutembea utupu maana kila utakayoivaa itakupwelepweta!!
Rais anarekebisha nchi kwa kutengeneza taasisi imara ambazo zitatimiza wajibu kwa nchi na si majizi imara yaporayo kwa jina la uzalendo!!
 
Kusema ukweli hana mvuto. Tena ni kwa wengi tu. Ila nawashauri Watanzania wamvumilie amalize muda wake kwani miaka minne si mingi. Hata taarifa za habari watu hawafuatilii tena. Watu wake wa karibu mshitueni msimdanganye kamwe.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Sukuma gang kazini
 
Yule alikuwa analalamika huku akifanya maamuzi, though pia alikuwa anatutengenezea mazingira ya kutupiga pia.

Tatizo ninaloliona sasa hivi, yeyote anayempinga mama anaonekana ni timu Magufuli.
Nimekuelewa hapo kwenye kutupiga
 
Bwahahaha....... MTU mzima haambiwi muongo . mbona katika uchaguzi mitandao ilizima ikiwa unasema mambo yalikuwa guru unatoa mawazo yako utakavyojiskia
 
Ripot yacag mbona watu hawafikishwi mahakamani? Chonde wananchi katiba mpya tutoe maoni atakae kula mali ya umma anyongwe au kupunguziwa adhabu kifungo cha maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…