Kwanini Rais huwa haongozani na wale Special Force akiwa katika ziara za nje ya nchi?

Kwanini Rais huwa haongozani na wale Special Force akiwa katika ziara za nje ya nchi?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Nimejiuliza hili swali mara nyingi, kwanini Rais wa Jamhuri ya Muungano akiwa nje ya Tanzania, huwa haambatani na wale walinzi wenye silaha nzito? Leo Rais SSH ametua Malawi bila wale walinzi hata alipoenda Rwanda ni hivyo hivyo! Wajuzi wa mambo njooni mtujuze utaratibu upoje?
 
Labda ni ubabe wa ndani tu. Wakitoka nje ya mipaka wanakalishwa.
 
Wale ni counter assault team. Siyo special forces.

Rais wa Marekani huwa anaenda nao kila sehemu aendayo hapa duniani.

Kwa Tanzania sidhani kama tuna rasilimali za kutosha kuweza wao kuambatana na Rais kila aendapo.

Hivyo, naamini jukumu hilo huwa linakabidhiwa kwa nchi mwenyeji.
 
Tuna hela za kusafirisha ile troop yote mzee baba?

Maana hata gari la Rais nalo tututaka tulibebe kama wafanyavyo USA...
 
Nchi mwenyeji ndio huchukua jukumu la ulinzi wa Rais awapo nje ya nchi although kuna special case kwa Marais wa USA,Russia,France,North korea na China na pia PM wa UK na India kama sikosei,wao huwa wanasafiri na troop yao yote ya ulinzi kwa sababu za kiusalama.
 
Siku izi silioni lile Gari lililokuwa na Antena nyingi sijui hata linaitwaje, wakati wa mwendazake lilikuwa halikosekani kwenye msafara.
Mbona lipo...kwenye msafara wa kiongozi yeyote mkubwa lazima liwepo
 
Siku izi silioni lile Gari lililokuwa na Antena nyingi sijui hata linaitwaje, wakati wa mwendazake lilikuwa halikosekani kwenye msafara.
Lilikua lnanikera Sana Lile dubwasha.

Likipaki sehemu, hata simu hupigi.

Linakata network mitandao yote[emoji3525]
 
Jukumu la ulinzi wa rais anapokua nje ya nchi lipo chini ya nchi anayozuru/ tembelea hivyo atatakiwa kuwa na walinzi wachache iwezekanavyo.
Isipokua kwa haya mataifa makubwa haya super powers na vinchi vidogo vyenye nguvu za kiuchumi na kiusalama. Watu wanapiga kambi wiki au miezi kadhaa kabla au baada ya kutangaza ziara. Zile ziara za dharura kama misiba pia zina arrangements zake prior

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Wale ni counter assault team. Siyo special forces.

Rais wa Marekani huwa anaenda nao kila sehemu aendayo hapa duniani.

Kwa Tanzania sidhani kama tuna rasilimali za kutosha kuweza wao kuambatana na Rais kila aendapo.

Hivyo, naamini jukumu hilo huwa linakabidhiwa kwa nchi mwenyeji.
Huwa nashangaa hao counter assault team kujifanya wapo busy wakizunguka na silaha nzitonzito as if wanategemea a serious assault kutoka kwa wanyonge wale huko vijijini ambao hata kupinga tozo mpya hawawezi.
 
Radio jamming vehicle. Ila pia ku bypass signals ni rahisi pia tu kama ilivyo ngumu kuset hizo frequevies

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
Tuna washukuruni nyote kwa majibu haya, nimeingia mtandaoni nimeliona aisee, aisee Uraisi ni mtamu nakumbuka mstaafu Mwinyi alisema kiti kitamu sana kile na usipokuwa na hofu ya Mungu ndio balaa kabisaa,lijidubwa limoja tu la mamilioni kumlinda mtu mmoja duh! 😳 😳
 
Back
Top Bottom