Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Alitegeneza kile ambacho kiingereza huitwa cult sina kiswahili chake.
Alisifiwa hadi kuitwa Mungu tena na profesa aliyejisifu usomi sana japo alikuwa kihiyo wa kawaida. Samia naye hakubaki nyuma.
Alikuwapo kama hakuwapo. Alisifia kiasi cha kupewa fursa ya kugombea na mwendazake tena. Sasa amechukua madaraka, anarudia mchezo ule ule.
Je Rais Samia hajajifunza kuwa binadamu si lolote bali mavumbi na anaweza kutoweka wakati wowote na mipango yake ikatibuka?
Pili, Rais Samia hajui hawa wanomsifia hawamsifii yeye kama ambavyo alimfanyia mwenzake bali kitumbua? Je anayajua ya kesho?
Chawa wanaanza kutangaza atagombea, je nani kampitisha? Je inakuwaje chawa waanze kampeni mapema?
Je unamshauri nini Samia Suluhu Hassan kuhusiana na changa la macho analopigwa na chawa?