Kwanini resale value ya Subaru Legacy iko chini?

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,238
Reaction score
4,885
wakuu hbr poleni na mihangaiko ,wengine mnasubuliwa na hang over ,msaada wa hili kwa nini kwa sasa subaru legency bei imekuwa chini sana na bado watu hawazichangamkii shida haswaa ni nini ? Toka anguko la TOYOTA ALTEZA soko la bongo naona pia kama Subaru legency nayo ilipitiwa na upepo je shida ni mwarabu kwa kuwa ina Turbo??? Au wabongo bado wamekariri??

Gari hii imetengenezwa kwa maumbo mawili ambayo ni station wagon kwa ajili ya off road na saloon.

Nayozungumzia hapa ni yenye umbo la saloon

Upande wa kushindana katika soko inashindana na gari zifuatazo Audi A4, VW Passat, Toyota Mark X, Nissan Teana, Mercedes C Class, BMW 3 Series na Mazda 6.

Mwenye A,B,C hebu atupe nimeona km tatu zinauzwa bei ya kawaida sana na bado zipo kwenye hali nzuri mno ikiwemo hii niliyopost picha


Je hizi gari zina tatizo gani mpk zinafanya bei inapoa??
 
Mkuu Subaru Legacy haina resale value ndogo..kama hauujui nenda umvvs.tra cheki legacy ya 2005 na 2006 ushuru wake unachezea wapi..na legacy nyingi zinazouza ni za humu humu ndani yenye recent registration utaikuta ni ya 2003, Toyota Altezza inanunuliwa na mtu mwenye mapenzi nayo....
 
Mi nachozungumzia zinazouzwa humu ndani mbn bei ni kitonga je zinachangamoto zipi
 
Legacy za kuanzia 2009.. 2.5L Turbo huwa nazielewa sana
 
Aisee nina subaru legacy hapa, huu ni mwaka wa pili sijawahi jutia maamuzi yangu. Kuhusu wese ni kawaida kulingana na matumizi yako tu.

Hii gari ni ya kwanza kwangu na nimeiabuse sana lakini bado naikubali mno. Safari ya Dar to Geita huwa siwazi, ukiachilia mbali rough road za huku vijijini Mbogwe.

Subaru will always be my choice.
 
Mkuu hii subaru legacy kuagiza nje mpaka inafika hapa bongo jumlisha na ushuru, ni kiasi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…