Kwanini ripoti ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini wa Mtwara hayatolewi kwa Umma wa watanzania hadi sasa?

Kwanini ripoti ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini wa Mtwara hayatolewi kwa Umma wa watanzania hadi sasa?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Mwanzoni mwa mwezi February mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliunda Tume ya kuchunguza ya Mauaji ya mfanyibiashara wa madini, Mussa Hamisi, kwa maelekezo ya Rais Samia.

Tume hiyo iliyoundwa na Waziri Mkuu, ilipewa muda wa wiki 2 kukamilisha ripoti hiyo.

Tume hiyo ilikamilisha ripoti yake na kumkabidhi Waziri Mkuu ripoti hiyo na Waziri Mkuu alisema, wakati anakabidhiwa ripoti hiyo kuwa ataikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ili aipitie ripoti hiyo na baadaye itolewe kwa Umma wa watanzania.

Hivi leo ni zaidi ya miezi 2 imepita, ripoti hiyo haijatolewa kwa Umma wa watanzania.

Swali ninalouliza, ni kwa nini utawala wa awamu ya 6, chini ya Rais Samia, unapata kigugumizi kuitoa ripoti hiyo kwa Umma wa watanzania?

Kuna nini kilichojificha, Hadi Tume hiyo ripoti yake isitolewe kwa Umma wa watanzania?

Ni hayo maswali yangu machache, ambayo naomba mamlaka husika, zinijibie maswali yangu hayo

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania...........

KAZI IENDELEE
 
Zile zilikuwa mbwembwe tu, ndiyo imeitoka hiyo.
 
Itaanza kufuka moshi kama ulivyoianzisha halafu watapaliwa nao wakohoe sana.
Wanaona ripoti ile imempaka matope Sirrooooo na huyo ndiye anayeendelea kukiweka madarakani chama chao cha CCM, kwa kuvuruga kila uchaguzi unaotokea Katika nchi hii, kwa kutumia mitutu ya bunduki..........

Kwa hiyo mama kaona kuitoa ripoti hiyo hadharani ni kukitia kitanzi chama chake cha CCM!
 
Wenye mamlaka wameamua kuifukia ripoti hiyo na kuiweka uvunguni!
Polisi waliilia timing hii ripoti. Wakati kamati inachunguza na kuandaa ripoti, Manjagu wakawapeleka Manjagu wenzao mahakamani na kusomewa mashtaka. Hivyo sasa, ikitolewa leo ripoti itakuwa inaingilia "Uhuru wa Mahakama". teh! teh! teh! teh! Akili mukichwa!!!!??
 
Ile ilikuwa kiki tu za Magu na Makonda. We ushawahi kuona kesi zile za noti bandia na upatu aliokuwa anakamata Sabaya? Alitakiwa aonyeshe mashine ya kuprint hizo noti bandia. Ila ndo hivyo kila kitu walikuwa wakimtukuza mwendazake.
We huijui tz umesahau mtu aliyeiba mafuta kigamboni mpk leo hatumjui... ukitaka kufa na stress waza stress za bongo Bora unywe zaki k vant maisha Yaendelee

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile ap
 
Kipindi mh.Rais anaanza uongozi,alipitia mitandaoni akaona tuhuma kuwa BOT kulichukuliwa bill 90 wakati magu anaumwa,basi nae haraharaka akaagiza uchunguzi ufanyike apewe ripoti hiyo..tulitegemea kwa kuwa aliagiza hadharani basi ripoti nayo ingetolewa hadharani,lakini hadi leo kimya
Nadhani hakujua kuwa Nchi Mambo ya kupakana matope pia yapo
 
Jaribu kufa uone kama tutakumbuka hata unyayo wako
 
Polisi wana laana.
Polisi wana tamaaa.
Polisi hawasimamii haki.

Polisi anababaika hata akiona laki 2 tu kwa raia, anababaika ili aichukue, Mungu anawapiga upofu mmoja hawana akiba, hawana biashara, wanaishi kimagendo tu kama si rushwa basi kujiweka kwa wadada wenye pesa au wanaume wenye pesa.

Hawasimamii haki kabisa.
Kwenye hii kesi kuna mmoja mke wake ameuza vitu vyote vya ndani, pamoja na kiwanja ili kumuokoa mumewe lakini hola, haijatosha zaidi ya kuongeza ugumu wa maisha na kuwa na madeni kila kona, hata nauli ya kwenda mtwara siku ya mahakama hana, achilia kumnunulia mahitaji mumewe akiwa mahabusu.
Leo hii hii kesi tunaiongelea sababu ya marehemu Greyson, Greyson asingekuwa na back up ya nguvu ingeisha kimya kimya.

Kuna askari mwingine yeye majambazi, matapeli wa viwanja ndo washkaji zake, na kwa sababu amepangiwa kulinda watuhumiwa na wahalifu wanaopelekwa na kurudishwa mahakamani, basi yeye ndo mtu kati yake na hakimu.
Yeye ni chanzo kikubwa sana kwa matapeli ya viwanja, na ujambazi kuongezeka.
Fikiria mtu anapambana kwa jasho lake mwaka au miaka ili asave hela anunue nyumba au kiwanja, wewe polisi unashirikiana na matapeli kumtapeli.

Mungu atakuacha?
Sasa ni miezi 5 yupo kitandani, sijui figo ina vimelea vya kansa,sijui koo limefanyaje.

Senti 5 hana, wanabaki kupitisha bakuli.

Njoo hawa polisi wa Cyber, simu inapotea.
Atakuambia kuitafuta wiki au wiki 2.
Kwa kuwa mtu anauhitaji sana anaingia gharama ya kumlipia nauli au hela ya mafuta, lunch n.k ili afanye kazi, ajabu ataipata na ataiuza au hatompa mwenyewe anajua mwenyewe atakapoipeleka.

Mapolisi mjirekebishe.

Big up kwenu mnaosimamia haki, na kujua majukumu yenu.
 
ripoti ipi ilishawahi kutolewa hawamuizi anzia ile ya ajali ya moto moro,labda ile samaki mto mara
 
Back
Top Bottom