Kwanini Rostam ameuza hisa zake za Vodacom?

Kwanini Rostam ameuza hisa zake za Vodacom?

Kuhusu kusufia,
Kumbuka ndugu yake yuko "ndani" kwa utakatishaji
Swali la msingi ni kwanini anauza na wakati huo huo anatuambia Magu anajenga uchumi mzuri sasa kwanini asiziache apate faida kufanya biashara TZ
 
Unajiona unajua Kumbe hujui

Kwenye Ulimwengu wa uwekezaji akitokea Mfanyabiashara Mkubwa wa level ya Rostam akiuza hisa zake huo ni Mjadala Mkubwa Sana Kwa Kuwa unaleta Impact kubwa kwenye FDI ( Foreign direct investment)

Hata Wafanyabishara wakubwa kabla ya kuwekeza wanaenda kwenye Stock market kuona trend ya kuuza Na kununua hisa Sasa Wewe Kwa kutojua unadhan Ni ajabu Mtu kuleta mjadala wa kujadili issue ya Rostm kuuza hisa zake

Sio Kila usichojua Basi hakijulikani

Wakati Mwingine chukua peni Na pensel ujifunze Kwa vitu usivyo Na utaalam navyo Na si dhambi kutojua Ila Ni dhambi kujifany unajua wakati hujui
You wrote it all!
 
Amecheza game ya Kibaishara

Kauza hisa Za Kampuni yake Kwa Kampuni ile ya ki South Africa Halafu kaenda kununua hisa Za ile Kampuni ya South Africa

Katika Lugha rahisi kafanya kuhamisha Mtaji wake kutoka Hapa Nchini mpaka South Africa lakin faida ya Uwekezaji wake ataipata kupitia South Africa
Hajanunua hisa SA ila anataka hamishia pesa zake kwenye biashara nyingine.
Kilimo na viwanda mmoja wapo.
 
Hii inatufundisha kwamba serikali iache ubabe na vitisho kwa wafanyabiashara nchini.
kwahiyo kahama kutoka umiliki wa hisa kwenye kampuni ya kitanzania akaenda kwenye umiliki wa hisa kwenye kampuni ya kikaburu.

Hii inatufundisha nini?
 
Mbona tuliaminishwa kuwa Rostam ni fisadi papa! ile mahakama ya mafisadi siku hizi si-i sikii tena au imeamia ile nyumba nyeupe pale magogoni maana tuliambiwa kuwa Lugumi ni fisadi, mdhulumu uchumi ila alivyoitwa sehemu nashangaa akageuka malaika uku serikali ya jiwe ikiambia ndo ilikuwa na shida.

Labda Ikulu sasa imegeuka mahakama ya mafisadi maana kila anayeingia kule ndani basi anaachiliwa huru
 
Wewe ungeuliza poromosheni za wooda ziko wapi siku hizi? Mazingira ya kucheza na kodi ni magumu sana siku hizi. Kila ujumbe unahesabiwa huko jumba la mawasiliano na vat yake inafekwa ju kwa ju.
 
Siamini kama ataziuza direct.. Hizo hela zitakuwa zinazunguka humo humo kwenye biashara zake
 
kwahiyo kahama kutoka umiliki wa hisa kwenye kampuni ya kitanzania akaenda kwenye umiliki wa hisa kwenye kampuni ya kikaburu.

Hii inatufundisha nini?
Akili ndogo tu, serikali ilikuwa ikimsumbua sana kuhusu hizo hisa, kwa akili yangu ndogo naona kama wanafungasha, huyu jamaa ana uraia wa canada anasepa hivyo
 
Ningekuwa mimi ndio ROSTAM ,MENGI,BAKHRESA,MO DEWJI

Ningeshahamisha mitaji yangu huko kwenye nchi zinazoeleweka kuliko kung'ang'a humu ndani .

Bahati mbaya mimi ni kapuku fulani niliye itilima huku[emoji23]
 
Swali la msingi ni kwanini anauza na wakati huo huo anatuambia Magu anajenga uchumi mzuri sasa kwanini asiziache apate faida kufanya biashara TZ
Sisi tuliokuwa tunapenda kusoma hadithi Enzi tukiwa watoto hatukuwahi kujuwa kuwa hizo hadithi zilikuwa zinatufundisha mambo ambayo baadae ukiyaona akili inabidi ipate tafsri haraka. kuna hadithi nilisoma kulikuwa na mfalme alipenda sifa sana, kuna mtu fundi mashuhuri wa kushona mavazi ya ajabu akaamua kumshonea mfalme vazi la ajabu lisiloonekana. Mfalme akalivaa akaenda kwenye umati wa watu akashangaa watu wanamshangaa, mwanzoni alidhani wanashangaa vazi lake lilivyo la ajabu ila watoto walianza kupiga kelele yuko uchi yuko uchi kwa sababu wakubwa waliogopa kumwabia kwamba yuko uchi. Kile kitabu ambaye anacho ebu akiweke humu ambao hawakubahatika kukisoma wakisome.
 
Rostam ni mfanya biashara sio mwanasiasa.
Rostam hakurithi utajiri kama Mo na Manji.
Kukutana kwake na Mzee pale white house kuna toa picha na tafsiri juu ya personality ya Rostam, binafsi namuona kama mtu mzima anayejielewa..

Kuuza hisa zake ni tafsiri ileile inayosema yeye ni mfanya biashara na kama mfanya biashara anataka faida na usalama wa mtaji na brand yake kama Rostam, credibility ya Rostam kwenye biashara nje na ndani ni kubwa kuliko wengi wanavyomjua. Rostam ni mfanyabiashara mkubwa wa nje na ndani na kwa miaka mingi anadeal na international business hasa kwenye construction na mining maana wengi mnamjua kupitia voda na CCM lakini huyu jamaa anapiga hela nyingi kwenye mining na construction hapa Tanzania na middle east akifanya kazi na international companies na hapo ndipo credibility yake na brand yake anaogopa kuviharibu kwa kujiondoa kwenye business zenye kelele za wanasiasa...
 
Yaani muda mwingine utasema tu kuwa watanzania bado tunayo safari ndefu. Hivi kijana kama huyu unategemea aje adai uhuru wake. Anaandika kabisa kwanini kauza. Kuna mtu hapa atakuuliza kwanini umeuza baskeli yako. Hivi unawaza sawa sawa. Au ndio umeamka kutoka usingizini
Mibange tu inamzingua
 
2011 Akili kubwaaaz Rostam Abdul rasoul Aziz alipojiuzulu Ubunge wa Igunga alitoa hotuba Fupi Sana akielezea mwelekezi wa Siasa zetu kwenda Mrama lakin ma vuvuzela kina Said Kubenea Na kipeperushi chake Cha Mwanahalisi walikuwa busy kumchafua Kwa Kashfa Za kutunga

Nakumbuka ilifikia hatua alipofiwa Na Baba yake Mzazi Rostam ilitakiwa uwe Na roho ya kijasiri kwenda msiban pale kwake Kwa kuwa ilionekana Kama Ni kusaliti Taifa

Wakati Mzee wake akiwa Hospital Kule France ilikuwa watu wanaaga kwenda Marekan Kumbe uongo wanaenda France lakin Kwa usiri Mkubwa Hata Ubalozin kwetu hawafiki ili wasijulikane wakati Ni watu wakubwa Sana ,

ukitaka kumuua mbwa mpe jina Baya wahenga walinena


Kuna Rafiki zake wakubwa Sana ilibidi waende usiku usiku kuhani msiba wakati alikuwa Mtu wao wa Karibu Sana Kwa zaid ya Miaka 15
Yaonyesha unajua mengi
 
Ningekuwa mimi ndio ROSTAM ,MENGI,BAKHRESA,MO DEWJI

Ningeshahamisha mitaji yangu huko kwenye nchi zinazoeleweka kuliko kung'ang'a humu ndani .
Pesa ipo hapo hapo walipo, huko nchi zilizoendelea zina wenyewe wanaoshikilia masoko yao na ushindani ni mkubwa sana. Hao jamaa wakiwa Tanzania ni first class citizens na wananyenyekewa na serikali na mabenki, wanaweza kuchukua ardhi bure halafu wakaitumia kuomba mikopo, huko nje ni watu baki tuu na kunavizingiti chungu mzima. Wao siyo wajinga kufanya biashara zao Tanzania.
 
Mafisadi waliitandika CCM wakarudi wakawanyoosha Chadema tumebaki mashabiki hatujielewi! Mara kumtetea Rostam mara chama!

Mengi tuliyotabiri 2015 ndio yanayoendelea. Sometimes inachosha hata kufatilia hizi mambo na uelekeo wa michango ya siku hizi.
 
Ningekuwa mimi ndio ROSTAM ,MENGI,BAKHRESA,MO DEWJI

Ningeshahamisha mitaji yangu huko kwenye nchi zinazoeleweka kuliko kung'ang'a humu ndani .

Bahati mbaya mimi ni kapuku fulani niliye itilima huku[emoji23]

Hakuna sehemu ya kupata supernormal profit Kama sehemu yenye vichwa Maji wengi
 
Mlitaka asiuze?
Nafikiri hilo swali angeulizwa mwenyewe!

Ova
 
kwahiyo kahama kutoka umiliki wa hisa kwenye kampuni ya kitanzania akaenda kwenye umiliki wa hisa kwenye kampuni ya kikaburu.

Hii inatufundisha nini?
Hii inatufundisha kwamba hali ya uwekezaji kwa Tanzania ni ngumu sana.
 
Back
Top Bottom