usiwe unakurupuka kuleta vitu bila kufanyia uchunguzi,
sio kila wanachosema waandish wa habari makanjanja ni kweli,
Kupitia taarifa ya Habari ITV saa 2, taarifa imesema katika utafiti uliofanyika na benki ya dunia katika nchi 100 Rwanda imekuwa nchi ya 7 kati ya 100 ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi kila mwaka na mfumuko wa bei umeshuka kwa kasi sana.
Najua wengi tunaichukia Rwanda na Kagame na hasa kutokana na mtafaruku na Raisi wetu lakini wenzetu wanafanya vizuri katika kupanga mipango yao na utawala wao unafuata sheria na hakuna ufujaji wa fedha za umma kama huku kwetu na hili linafanyika kutokana na Kagame kuwa mkali, tunatakiwa tujifunze mazuri kutoka huko ili nasi tuendelee.
Aisee una akili wewe! sijawahi ona, ni kweli rwanda pamoja na kujisifia na kupiga propaganda kwamba uchumi wao unakua lakini sio endelevu. Hawana rasilimali, hawana viwanda, hawana ardhi ya kutosha kulima na kuzalisha mazao ya chakula na biashara duh nisitaje mengi kifupi wana majanga mengi, watupigie magoti tu sisi baba zao TZ, ila tusiwapokee mpaka kagame atokeee!!
Wewe si Mtanzania Ww ni mhamiaji Haramu kwani utetezi wako kwa Kagame umedhihilisha jinsi ulivyo mtumwa wa Fikra za kagame fikra za wizi wa Rasirimali za Congo na Kujifai eti amekuza Uchumi ! Ni Ukweli gani umeuleta ?hakuna Ukweli juu ya mtizamo wa kumtetea Kagame .Acha Mifano ya ajabu Kumbuka Tz hailingani na Rwanda tz kuna watu Milion 45 huku Rwanda ni Sawa na Wilaya ya kinondoni kwa idadi ya watu iweje ulinganishe ukubwa wa Ka Nchi kaduchu kanakotawaliwa kibabe na Taifa Kubwa linalopenda Amani ?umejisahau sana kumbuka Zoezi la Wahamiaji haramu linakuja Popote Ulipo utaludishwa Rwanda mkabanane huko huko kwa wapenda vita na waumini wa M23Mimi ni mtanzania halisi, tatizo lenu wauza unga hampendi kuambiwa ukweli, usifiche mshumaa chini ya uvungu wa kitanda ulete giza utaunguza kitanda na nyumba. Kagame anapiga kazi nchi yake inapiga hatua, nyinyi kupiga domo tu eti anaiba Kongo. Endeleeni kusafiri na mihadarati yetu muimarishe chama wenzenu wanafana mambo ya maendeleo.
Tuleteeni ushahidi acheni kuongozwa na mihemko na chuki zenu kwa Kagame
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .