Kwanini saa tunasoma kinyume kwa mfano mshale ukionesha 1,2,3,4 inasomeka au tunatamka saa 7,8,9,10?

Kwanini saa tunasoma kinyume kwa mfano mshale ukionesha 1,2,3,4 inasomeka au tunatamka saa 7,8,9,10?

Msishangae

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
392
Reaction score
284
Habari WanaJamiiForums,

Mimi kwa kweli huwa najiuliza jinsi majira au saa invyotamkwa inakuwa ni kinyume kabisa hivi wana JamiiForums

Nijuzeni kwa nini inakuwa hivyo?
 
12 ni saa 6, kwahiyo 12-6= 6
13 ni saa 7 kwahiyo 13-6=7
14 ni saa 8 kwahiyo 14-6=8

Sijui umenielewa sasa??
 
Mkuu iyo ni science tu

Kuna kitu kinaitwa Greenwich meridian time ni mstari uliochorwa kutofautisha wakati maeneo mbalimbali

Kila kona unayoiona kwenye mstari Ina maana mfano kuna E. A. T, B. S. T, N. K

Na lengo ni kuweka uwiano mdogo wa mda Kati ya maeneo na ilionekana mfumo wa jua kuzama na kuchomoka una jumla ya masaa 12 ivyo tukigeuza mda kwa 1isome saba deviation itakua sio kubwa

Ni Machche tu ayo
 
ili uendane na dunia usiwahi kuzungumza ukweli hata ukiwa unauona, zungumza uongo ili siku ziende
 
Mkuu hili swali lako ni marudio ya thread nyingine.
Lilishajibiwa vizuri tu.

Kifupi:
Waswahili siku inaanza saa moja asubuhi.
Watengeneza saa (wazungu) siku inaanzia saa sita usiku. Wakati wewe mswahili una amka na kuanza moja (1) wao wapo masaa saba(7) mbele yako.

Ufanunuzi Kirefu:
Sasa anza kuhesabu masaa yapo mangapi toka saa sita usiku hadi saa 1 asubuhi.
Saa 6:00 usiku - Saa 7 usiku = Saa 1
Saa 7:00 usiku - Saa 8 usiku = Masaa 2
Saa 8:00 usiku - Saa 9 usiku = Masaa 3
Saa9:00 Alfajiri - Saa 10 usiku = Masaa 4
Saa 10:00 Alfajiri - Saa 11 usiku = Masaa 5
Saa 11:00 Asubuhi - Saa 12 Asubuhi = Masaa 6
Saa 12:00 Asubuhi - Saa 1 Asubuhi = Masaa 7 au saa ya/la saba toka mwanzo wa siku. Yaani kizungu ni 7hrs After Meridian ( 07: 00 AM)

Meriadian ndiyo nini? Nakuachia homework.

Funguo (Key):
"Saa 6:00 usiku - Saa 7 usiku" isomeke "Saa 6:00 usikui hadi Saa 7 usiku".
 
Mtoa mada anakubali siku inamasaa 24 lakini kwa nini saba iwe saa moja na moja iwe saa saba, au mbili iwe saa nane n.k?
 
Tatizo ushamba wetu waswahili wa kukariri kila kitu.

Kwanini tusirekebishe saa kulingana na majira yetu yaani siku ianze saa moja asubuhi na mshale wa saa uwe kwenye moja (1)?
Sisi elimu yetu ni ya kukariri mambo tu, kwamba saa ya mzungu ikisoma moja basi yangu lazima isome moja badala ya saba.
 
mtoa mada anakubali siku inamasaa 24 lakini kwa nini saba iwe saa moja na moja iwe saa saba,au mbili iwe saa nane n.k?
Mkuu hata tukitumia hiyo modulo 24 badala ya modulo 12 kwenye saa kwa kufuata majira ya kiswahili basi saa saba usiku itasoma 13 badala ya 1, saa sita usiku itasoma 12 badala ya 0, saa 11 asubuhi itasoma 23 badala ya 5.
 
Mkuu hili swali lako ni marudio ya thread nyingine.
Lilishajibiwa vizuri tu.

Kifupi:
Waswahili siku inaanza saa moja asubuhi.
Watengeneza saa (wazungu) siku inaanzia saa sita usiku. Wakati wewe mswahili una amka na kuanza moja (1) wao wapo masaa saba(7) mbele yako.

Ufanunuzi Kirefu:
Sasa anza kuhesabu masaa yapo mangapi toka saa sita usiku hadi saa 1 asubuhi.
Saa 6:00 usiku - Saa 7 usiku = Saa 1
Saa 7:00 usiku - Saa 8 usiku = Masaa 2
Saa 8:00 usiku - Saa 9 usiku = Masaa 3
Saa9:00 Alfajiri - Saa 10 usiku = Masaa 4
Saa 10:00 Alfajiri - Saa 11 usiku = Masaa 5
Saa 11:00 Asubuhi - Saa 12 Asubuhi = Masaa 6
Saa 12:00 Asubuhi - Saa 1 Asubuhi = Masaa 7 au saa ya/la saba toka mwanzo wa siku. Yaani kizungu ni 7hrs After Meridian ( 07: 00 AM)

Meriadian ndiyo nini? Nakuachia homework.
Walau ww ulikuwa na point nzuri japo umetuacha kwenye mataa.
 
Nijuavyo mimi wao wanaanza kuhesabia siku kuanzia usiku kwahiyo saa saba usiku Ndio saa yao ya Kwanza ya siku ndio inakua saa Moja.

Kwahiyo unapoanza kuhesabu siku asubuhi ya saa Moja kwao inakua saa 7 tangu saa 6 usiku. Sioni Shida labda sisi kwetu siku inaanza saa ngapi?
 
Habari WanaJamiiForums,

Mimi kwa kweli huwa najiuliza jinsi majira au saa invyotamkwa inakuwa ni kinyume kabisa hivi wana JamiiForum

Nijuzeni kwa nini inakuwa hivyo?

Kwa sababu siku mpya inaanza baada ya saa 6 usiku,hivyo saa 7 usiku inahesabika kama saa moja ya siku mpya, na ndiyo chanzo cha 7 kusomeka 1 katika mfumo wa saa !!
 
Siku inaanza saa 6 na sekunde 1 usiku wewe unapoa amka saa 1 asubuhi na kujichanganya ndio siku imeanza wenzako ndio wapo saa la 7 tangu siku imeanza ila ww ndio unataka lisaa la 7 liwe la 1 kwa sababu ndio umeamka mpaka inafika saa 6 mchana unatoa macho huelewi imefikaje wenzio ndio wamefika lisaa la 12 toka siku ianze wanapoanza ungwe ya pili ya siku ww ndio una haha pakwenda kula au utakula vp wenzio wanakata saa la 13 mpaka ije irudi kwenye 12 unayo iona ww wenzio walisha kata saa la 24 wanaanza upya maisha huku ww unaota ndoto za alinacha ukisubiri siku yako inayo anzia lisaa la 7 kutoka kwa wenzio walio ianza mda ambao ww unaota! Hapo kama hujaelewa print kachemshe unywe kama chai
 
Mkuu hata tukitumia hiyo modulo 24 badala ya modulo 12 kwenye saa kwa kufuata majira ya kiswahili basi saa saba usiku itasoma 13 badala ya 1, saa sita usiku itasoma 12 badala ya 0, saa 11 asubuhi itasoma 23 badala ya 5.
Saa 7 usiku haiwezi kusomeka 13 ungwe ya pili ya siku inaanzia saa noon lisaa la 12 na sec1 tangu siku ianze 00:00 usiku hapo ndipo saa 7 mchana inakua 13
 
Back
Top Bottom