kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Ukifuatilia sala na maombezi mengi yanayofanywa hasa na viongozi wa dini ya kikikristo ambayo Mimi Ni muumini utaja majina ya viongozi wa kitaifa, kimkoa, kiwilaya na hata mataifa mengine. Katika sala hizo utajwa kwa majina, Rais na Marais wastaafu, Makamu, Waziri mkuu, Jaji Mkuu, Spika ,vyombo vya dola na viongozi wengine. Msingi wa maombi huwa kuwaombea afya njema, kuwaombea watumiwe na roho mtakatifu, waendeshe maeneo yao ya utawala kwa haki nk
Lakini katika sala na maombi hayo uwezi kusikia maombaji wakiwaombea wanaodhulumiwa, uwezi kusikia wakitajwa viongozi wa upinzani, uwezi kusikia wakiombea makundi ambayo yanapingana kwa hoja na utawala. Hii dhana naamini inawanyima amani baadhi ya watu hasa wale ambao makundi yao hayatajwi popote na viongozi wao wa dini.
Swali langu; kwanini viongozi wa dini wameshindwa kufanya maombi ambayo siyo biased? Je ndivyo imani inavyotaka? Kwamba tuwaombee wenye madaraka tu na siyo makundi yote Tena kwakuwataja majina Kama tunavyofanya kwa viongozi wengine? Kwanini tunasali kwa ubaguzi?
Naomba kufungua mjadala huu kuwaweka sawa wahubiri, Wana mombi na watu wengine wanaoliombea Taifa kutokufanya ubaguzi maana amani ya nchi haitikani na viongozi inatokana na wananchi.....yamkini walikuwa hawajui sala zinaweza kuleta ubaguzi Sasa nawaomba wainuke waombe Mwongozo wa kiroho.
Wanashindwa kukemea maovu na dhulma Basi waombee dhulma na uovu viondoke kwenye jamii ili pawe salama kwao kutangaza neno. Wapo watu wanakwama kwenda kwenye nyumba za ibada maana wanaoongooza nyumba hizo awataki kusimama na Haki wanasimama na mahitaji ya wanadamu waliopewa utawwala.