Kwanini samaki wa baharini hawafiki mikoani?

Kwanini samaki wa baharini hawafiki mikoani?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wandugu kwanini hao samaki wa baharini hawafiki huku mikoani. Huku sijawahi ona bucha linauza samaki wa baharini. Labda vibua kidogo. Ingekuwa poa sana na sisi tupate dagaa mchele tupige na ugali.

Mabucha yote ni sangara na sato. Kwani pweza na hao samaki wengine wa baharini hawakai kwenye mafriza?

Nini kinakwamisha uduvi wasifike mikoani?
 
Swali zuri sana, japo zimeagizwa meli kwa ajili ya uvuvi ambazo zitagawanywa kwa Zanzibar na Tanzania bara na tukumbuke samaki wa ziwa Victoria sangara na sato wanapatikana nchi nzima na Dar wanapatikana kwa uhakika zaidi na kwa bei nafuu kuliko wa baharini mpaka uende fery.
 
Ukweli ni kwamba watu wa bara wengi ni antagonistic kutumia bidhaa za bahari. Msukuma ale papa, nguru, taa, tasi? Wao watakwambia wamezoea sato na kidogo sangara.

Kuna msukuma mmoja tulikua tunafanya naye kazi tulikaa pale hotel ya Peacock nikamzoesha kula changu ndio akaanza kuwaelewa samaki wa baharini.

Na hata huko kwao Mwanza utasikia sato....sangara hawawapendi. Ila kimsingi sangara ana mnofu sana. Napenda sangara kuliko sato
 
Kanda ya Ziwa pia kuna aina nyng za samak kuna ningu, nembe ila wanaishia huko huko kwann sangara na sato?
Mm nafikir kwasababu ya ladha na kuwa na kuwa na nyama nyngi
 
Kanda ya Ziwa pia kuna aina nyng za samak kuna ningu, nembe ila wanaishia huko huko kwann sangara na sato?
Mm nafikir kwasababu ya ladha na kuwa na kuwa na nyama nyngi
Hao wengine hawapatikani muda wote . Ni wa msimu hasa wa mvua kwa hiyo ni wachache . Lakini Sato & Sangara ni all over the year
 
Back
Top Bottom