Kwanini samaki wa baharini hawafiki mikoani?

Kwanini samaki wa baharini hawafiki mikoani?

Vyombo duni ziwani vinaweza vuna mazao mengi sana. Jiulile boat ya kivuvi ya juu kabisa ziwa vic inagharimu chini ya 15 milion hivyo wamejikuta wawekezaji huku ni wengi kuliko baharini. Na kujikuta mazao ya huku yanakuwa mengi na kufanya bei ishuke kuliko wa baharini. Kitu cha pili ni uhamaji wa watu kutoka bara kwenda pwani. Mtu anatoka bara akiwa kazoea chakula chake na kuhamia pwani hivyo muuzaji anampelekea hukohuko na ananunua ila wanaotoka pwani ni wachache sana kuja bara hivyo muuzaji anakuwa hana uhakika na wanunuzi wa mzigo wake
 
Samaki wa maji baridi ni watamu kuliko hawa wa maji chumvi, alafu kuna samaki wa maji baridi unaletewa akawa bado anpumua kabisaaaa
 
Igombe fisherman nyumbani Mwanza nilikua nauza samaki wa kukaanga akaja mzee fulani akakuta nina sato wengi na pia sangara,akasema nimfungie sato ila akasema kama wangekua ni wa moto angependa wa kutafuna pale pale,nikamwambia zunguka huko nyuma mama anakaanga ukachukue waliotoka motoni kabisa.

Baada ya kwenda akasema basi amehairisha maana apendi sato waliokaangiwa mafuta ya sangara kwakua hao sangara waliletwa ziwa victoria yeye angali kijana.Hivyo akachukua tu sato wabichi ambao wataenda kumkaangia nyumbani kwake.Pia humu kuna uzi nilishawahi uona unazungumzia hichi kitu
Unaweza ukawa kweli ila hizi habari huwa siziamini na huwa nazifuatilia google huwa sipati iliyokamili
 
Unaweza ukawa kweli ila hizi habari huwa siziamini na huwa nazifuatilia google huwa sipati iliyokamili
Nadhani watu wanazungumzia habari ya vifaranga wa Sangara wanaowekwa kwenye ponds au vitalu maeneo ya ziwani.

Samaki huwa wanabadilika kulingana na mazingira watayoishi na vitu vinavyoingia kwenye maji kama kemikali na shughuli za kibinadamu zina athiri species ya samaki.
 
Kwa soko la DSM na nje yanalipa vizuri kuluko mikoani ambako watu hawana uwezo mzuri kifedha
 
Samaki wa baharini- hawafai kuliwa kwa mtu mwenye ubongo timamu.
Radha yao mbaya
Sio watamu

Mwiko kula hawo wadudu
Pole sana mzee, hivyo pia kwa mtu wa pwani samaki wa maji baridi hawapendi, maana wengine wanashombo ile mbaya.
 
Kanda ya Ziwa pia kuna aina nyng za samak kuna ningu, nembe ila wanaishia huko huko kwann sangara na sato?
Mm nafikir kwasababu ya ladha na kuwa na kuwa na nyama nyngi
Hapo kwenye ningu na nembe a.k.a matusi ya mwanza umenikumbusha nyumbani kabisaa
 
Kuna mtaalam mmoja wa mambo ya samaki aliniambia kuna fursa ya kufuga samaki wa bahari pembeni ya bahari sema wabongo hatujaichangamkia hii fursa ngoja nimtafute niweke maduka yangu ya samaki songea mbeya dodoma na iringa kwa kuanzia

Hesabu za kwenye karatasi ni nzuri sana.
 
Inawezekana uhitaji kwa dar ni mkubwa kiasi kwamba wanashindwa kuzivusha.
 
Samaki watakua wanachoka kuogelea kutoka dar kuja huko mkoani,samaki wa dar ni wavivu tu!
 
ntafanya huu mradi hela yangu ya kustaafia
Kabla ya kuanzisha kwa Sheria za Deep Sea fishing regulations ya 2005 inatakiwa upate kibali cha DG wa uvuvi, Kisha wajue sehemu utakayotengeneza aqua culture hiyo ya kufuga samaki, pasiwe eneo la shughuli za kibinadamu,mkondo au njia ya vyombo vya majini. Kisha afisa uvuvi atajua mradi na atapita kukagua mara Kwa mara. Ukimalizana na vibali kazi ni kwako, Ziwa Victoria nimeona wanafanya hii kitu ila baharini bado sijaona.
 
Ukweli ni kwamba watu wa bara wengi ni antagonistic kutumia bidhaa za bahari. Msukuma ale papa, nguru, taa, tasi? Wao watakwambia wamezoea sato na kidogo sangara.

Kuna msukuma mmoja tulikua tunafanya naye kazi tulikaa pale hotel ya Peacock nikamzoesha kula changu ndio akaanza kuwaelewa samaki wa baharini.

Na hata huko kwao Mwanza utasikia sato....sangara hawawapendi. Ila kimsingi sangara ana mnofu sana. Napenda sangara kuliko sato
sangara ni samki wa kuletwa sio asili wala sio mtamu mkuu.
mvuvi huwezi mkuta anakula sangara never sana sana utamkuta anakula gogogo sangara kama kakoswa kabisaa
 
Back
Top Bottom