Kwanini samaki wa baharini hawafiki mikoani?

Aisee ni kweli kabisa, mfano hapa Dodoma upatikanaji wa samaki ni kiwango hafifu sana,
Samaki wengi wanatoka Mtera ambako nyama ni ndogo na hawana utamu kama Jodari, Tasi , kole kole n.k yaan mikahawa mingi hapa ni nyama ya Ng'ombe
 
Ndio, kila samaki ili avuliwe lazima uwe na kibali na ulipie. Pia kama unasafirisha kwenda nje Kuna vigezo vyake.
Duuuu aise basi kazi hipo yani kila samaki lazima upate kibali chake tena mimi nilidhani ukipata tu kibali wewe unavua mwanzo mwisho ili mradi uzivue wale ambao ni wadogo sana na hivyo vigezo vya kupeleka nje samaki ndiyo vipi tena?basi nchi yetu kwene eneo la uwekezaji tuko nyuma na utaratibu wetu niwa hovyo sana Mkuu.
 
Mkuu samaki wa pwani ni samaki wa kimwinyi, adimu sana na hata wakipatikana bado demand yao ni kubwa , kiufupi hata pwani kwenyewe hawatoshi.

Kuna baadhi ya aina za samaki hata kufika sokoni kwenyewe ni nadra , kuna mmoja ainaitwa Songoro , akipatikana huyo , kipaumbele anapewa mwenye chombo , au dalali almaarufu , kama' mboga 'nyumbani.

Uduvi hatoweza kufika mkoa kwa sababu hizo hizo , demand bado ni kubwa mno pwani
 
Hao wengine hawapatikani muda wote . Ni wa msimu hasa wa mvua kwa hiyo ni wachache . Lakini Sato & Sangara ni all over the year
Mkuu
Samaki wa pwani wapo full time pale feri , bagamoyo , somanga nangurukuru , mchinga lindi na mtwara. Kiufupi wanapayikana samaki wengi , ila pia demand ni kubwa sana.
 
Alafu bahari n kubwa kuliko ziwa Victoria
Lakn sato na sangara kila Kona ya nchi wapo.
Kanda ya ziwa ipo juu sana kwa magonjwa ya kansa na mengine mengi hatarishi kutokana na chemical contamination ya maji na samaki wa ziwa victoria , migodi huko ndio sababu.
Kwa mtu anayefatilia mambo ni ngumu sana kuendelea kutumia products za ziwa victoria .
Sato na sangara wanapatikana kirahisi Tanzania nzima sababu demand yao imeshuka sana ,
 
Acha uongo, samaki wa mahi chumvi hatuwapati tu huku bara lakini tunawapenda sana
 
Tupo wengi tu
 
Tatizo linalofanya demand kuwa kubwa ni kuwa uvuvi unaofanyika Tanzania ni local ambao ni sawa na kutafuta kitoweo Cha kula Leo tu. Ndio kinapelekea supply kuwa ndogo ingawa tuna Samaki wengi Sana ambao tunaweza ku export nje na nchi nzima wakauzwa kila Mkoa. Ndio maana Kuna Samaki wakivuliwa mvuvi anakuwa mfalme anauza Bei atakayo na Kuna muda anagoma kuuza, Kuna kipindi wakina mama wanaenda ferry wanakosa hata hao dagaa mchele au Samaki wadogo.

Uvuvi wetu unatumia zana za kizamani na uwekezaji bado mdogo sana kuanzia Kwenye meli, vifaa(fishing gears) na sehemu za kutunzia na kuwachakata samaki.
 
Unapo export samaki wale unaowapelekea wanakupa vigezo hao samaki wawe katika ipi.

Uwekezaji bado Sana sekta ya uvuvi, benki ya kilimo na kituo Cha uwekezaji zilitakiwa kutia nguvu. Uvuvi ukiwekeza unaweza ukainua Sana pato la taifa. Kama wavuvi wanabahatisha wapi watapa samaki wakati technology Sasa Kuna fishing camera na fish finder inakuonyesha wapi samaki wapo. Na uvuvi wa kisasa meli inatakiwa iwe na sehemu za kuhifadhia samaki maana inaweza ikatumia mpaka mwezi ipo baharini na kuja bandarini kushusha mzigo
 
Kuna mtaalam mmoja wa mambo ya samaki aliniambia kuna fursa ya kufuga samaki wa bahari pembeni ya bahari sema wabongo hatujaichangamkia hii fursa ngoja nimtafute niweke maduka yangu ya samaki songea mbeya dodoma na iringa kwa kuanzia
 
Watu wa mikoani hawapendi samaki wa maji ya chumvi pia wazanzibar hawapendi samaki wa maji matamu
 
Vyombo duni ziwani vinaweza vuna mazao mengi sana. Jiulile boat ya kivuvi ya juu kabisa ziwa vic inagharimu chini ya 15 milion hivyo wamejikuta wawekezaji huku ni wengi kuliko baharini. Na kujikuta mazao ya huku yanakuwa mengi na kufanya bei ishuke kuliko wa baharini. Kitu cha pili ni uhamaji wa watu kutoka bara kwenda pwani.

Mtu anatoka bara akiwa kazoea chakula chake na kuhamia pwani hivyo muuzaji anampelekea hukohuko na ananunua ila wanaotoka pwani ni wachache sana kuja bara hivyo muuzaji anakuwa hana uhakika na wanunuzi wa mzigo wake
 
Wanamjua Mkundajiii hawa..
 
Nani alipandikiza? Hizi story sijui zinapatikana wapi
Igombe fisherman nyumbani Mwanza nilikua nauza samaki wa kukaanga akaja mzee fulani akakuta nina sato wengi na pia sangara,akasema nimfungie sato ila akasema kama wangekua ni wa moto angependa wa kutafuna pale pale,nikamwambia zunguka huko nyuma mama anakaanga ukachukue waliotoka motoni kabisa.

Baada ya kwenda akasema basi amehairisha maana apendi sato waliokaangiwa mafuta ya sangara kwakua hao sangara waliletwa ziwa victoria yeye angali kijana.Hivyo akachukua tu sato wabichi ambao wataenda kumkaangia nyumbani kwake.Pia humu kuna uzi nilishawahi uona unazungumzia hichi kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…