Kwanini samaki wa baharini hawafiki mikoani?

 
Samaki wa maji baridi ni watamu kuliko hawa wa maji chumvi, alafu kuna samaki wa maji baridi unaletewa akawa bado anpumua kabisaaaa
 
Unaweza ukawa kweli ila hizi habari huwa siziamini na huwa nazifuatilia google huwa sipati iliyokamili
 
Unaweza ukawa kweli ila hizi habari huwa siziamini na huwa nazifuatilia google huwa sipati iliyokamili
Nadhani watu wanazungumzia habari ya vifaranga wa Sangara wanaowekwa kwenye ponds au vitalu maeneo ya ziwani.

Samaki huwa wanabadilika kulingana na mazingira watayoishi na vitu vinavyoingia kwenye maji kama kemikali na shughuli za kibinadamu zina athiri species ya samaki.
 
Kwa soko la DSM na nje yanalipa vizuri kuluko mikoani ambako watu hawana uwezo mzuri kifedha
 
Samaki wa baharini- hawafai kuliwa kwa mtu mwenye ubongo timamu.
Radha yao mbaya
Sio watamu

Mwiko kula hawo wadudu
Pole sana mzee, hivyo pia kwa mtu wa pwani samaki wa maji baridi hawapendi, maana wengine wanashombo ile mbaya.
 
Kanda ya Ziwa pia kuna aina nyng za samak kuna ningu, nembe ila wanaishia huko huko kwann sangara na sato?
Mm nafikir kwasababu ya ladha na kuwa na kuwa na nyama nyngi
Hapo kwenye ningu na nembe a.k.a matusi ya mwanza umenikumbusha nyumbani kabisaa
 
Kuna mtaalam mmoja wa mambo ya samaki aliniambia kuna fursa ya kufuga samaki wa bahari pembeni ya bahari sema wabongo hatujaichangamkia hii fursa ngoja nimtafute niweke maduka yangu ya samaki songea mbeya dodoma na iringa kwa kuanzia

Hesabu za kwenye karatasi ni nzuri sana.
 
Inawezekana uhitaji kwa dar ni mkubwa kiasi kwamba wanashindwa kuzivusha.
 
Samaki watakua wanachoka kuogelea kutoka dar kuja huko mkoani,samaki wa dar ni wavivu tu!
 
ntafanya huu mradi hela yangu ya kustaafia
Kabla ya kuanzisha kwa Sheria za Deep Sea fishing regulations ya 2005 inatakiwa upate kibali cha DG wa uvuvi, Kisha wajue sehemu utakayotengeneza aqua culture hiyo ya kufuga samaki, pasiwe eneo la shughuli za kibinadamu,mkondo au njia ya vyombo vya majini. Kisha afisa uvuvi atajua mradi na atapita kukagua mara Kwa mara. Ukimalizana na vibali kazi ni kwako, Ziwa Victoria nimeona wanafanya hii kitu ila baharini bado sijaona.
 
sangara ni samki wa kuletwa sio asili wala sio mtamu mkuu.
mvuvi huwezi mkuta anakula sangara never sana sana utamkuta anakula gogogo sangara kama kakoswa kabisaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…