mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,773
- 2,183
Jumuia ya Waislamu duniani kote imekuwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hapa Tanzania na Afrika Mashariki nzima sikukuu ya Idi inatarajiwa kuwa Alhamisi au Ijumaa, kutegemea na kunadama kwa mwezi.
Swali langu ni kwamba kwa nini sayansi na teknolojia isitumike kufahamu mwezi utaonekana siku gani? Teknolojia hii imekuwapo siku nyingi na ni rahisi kabisa kufahamu mwezi utaonekana siku gani na saa ngapi na dakika ipi.
Hata ukitaka kufahamu mwezi wa Julai 2027 mwezi utaonekana lini, saa ngapi na dakika ipi, utaambiwa. Binafsi naona inaleta mantiki
kutumia sayansi kufahamu na kutangaza mfungo utaisha lini ili kuwawezesha watu kufanya mipango ya sikuu hiyo kuliko kubahatisha ama ilivyo sasa.