Kwanini Serikali haikuruhusu Tanzanite za Laizer kuuzwa mnadani ili kila mtu ashiriki?

Brightg

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
372
Reaction score
662
Serikali yetu ya awamu ya 5 inawajali sana wayonge na maskini na inahitaji watu watajirike na waondokane na umasikini lakini nauliza tu kwanini Serikai haiku ruhusu haya mawe yauzwe kwa mnada ili kila mtu ashiriki.

Na serikali ishiriki kwenye mnada ili aliye pata mawe yake apate hela nzuri itakayo tokana na mnada na sio maamuzi tu kuwa serikali imeyachukua na imepanga bei yenyewe.
mawe.jpg
 
Huyo mwenye mawe hayo umesikia kalalamika? Mwenye madini hayo yupo ktk industry ya madini zaidi ya miaka kumi, hakuna unachoweza kumdanganya kuhusu bei ya tanzanite. Tafuta hela yako ya kula mkuu acha chokochoko!
 
Huna akili kabisa, kabla ya soko walikuwa wanauzaje mawe unaelewa utaratibu, kila mtu alikuwa anaenda kwa mtu atakaye mpa hela anayo itaka watu walikuwa wanajitokeza kila mtu na ofa yake, alipofikisha kwenye soko la madini akaambiwa thamani yake na hapo hapo akaambiwa serikali ndio itachukua unafikiri hakuogopeshwa kutishana naye?

Kamuulize, ilibidi awe mpole kwann alikataliwa asimhusishe mwingine kutaka kununua. UBABE dnio ulio tumika vinginevyo ata nyanganywa. KABLA YA KUNIJIBU UNATAKIWA UWE NA AKILI ILIYO TULIA.
 
Sijaelewa hizi hoja za vichekesho zinaanzia wapi! Nimeona na mbunge mstaafu mmoja nae akinukuliwa na mtazamo kama huu.

Mmiliki by default wa madini yote Tanzania ni serikali ya JMT. Hivyo kuruhusu watz esp watu binafsi na kuwawekea utaratibu wakafaidika na huo uchimbaji bado inaonekana haitoshi na ni tatizo kubwa kwa baadhi ya watu na wengine kutafuta mileage za kisiasa!
 
Huna akili kabisa, kabla ya soko walikuwa wanauzaje mawe unaelewa utaratibu, kila mtu alikuwa anaenda kwa mtu atakaye mpa hela anayo itaka watu walikuwa wanajitokeza kila mtu na ofa yake, alipofikisha kwenye soko la madini akaambiwa thamani yake na hapo hapo akaambiwa serikali ndio itachukua unafikiri hakuogopeshwa kutishana naye?

Kamuulize, ilibidi awe mpole kwann alikataliwa asimhusishe mwingine kutaka kununua. UBABE dnio ulio tumika vinginevyo ata nyanganywa. KABLA YA KUNIJIBU UNATAKIWA UWE NA AKILI ILIYO TULIA.
Sasa kama unajua kila kitu kwa nini uliweka hii post ?
 
Kuna watu walalamishi sana.
Jua kuwa kuna baadhi ya vitu hata viwe na thamani kiasi gani huwezi uza kutokana na umuhimu wake kwako. Kwa mfano huwezi kumtoa mkeo kwa mtu mwingine sababu huna pesa au kutaka sifa hata kama una uwezo.

Kwa ukubwa wake na vile yanapatikana tz pekee, ingekuwa ni ujinga hayo madini yanunuliwe na mtu au kampuni binafsi ambayo ingeweka kwenye makumbusho zao na kupata zaidi.

So ilikuwa na lazima serikali kuyanunua hayo ili kuweka kumbukumbu kwa taifa hili. Sometimes, usiangalie faida tu, angalia na taifa lako. Hayo sasa moja ya utambulisho la taifa.

Na nakushauri, usichukie sababu amenunua jiwe, hata ingekuwa cdm ndio wanaongoza nchi kwangu wangekuwa wamefanya kitu cha maana sana sababu ni utaifa wetu kwanza.
 
Serikali ingeruhusu ungekuja na swali kwa nini serikali imeruhusu. Haya mambo ndio yameidhoofisha Chadema hadi Mbowe anasingizia kapigwa na watu wasiojulikana.
 
So ilikuwa na lazima serikali kuyanunua hayo ili kuweka kumbukumbu kwa taifa hili.
Ni leo tu au jana ndio kuna mawe yametoka ambayo yangeweza kuwekwa kwenye kumbukumbu ya nchi eti, come on usifanye kuwa kama leo ndio umesikia kuna madini yanayoitwa tanzanite, sababu hii haina mashiko, tunaangalia faida ya mtu mmoja katika maisha yake anafaidikaje na jasho lake kwa kulipata jiwe hilo kupitia soko sio akubali tu bei anayopewa.

Kwenye kilimo serikali ilisema watu wapange bei wanazoona zina wafaa kuuza mazao sio bei tu inayoletwa ambayo ni kandamizi.
 
Huna ata Elfu 50 mfukoni unataka mnada wa madini
 
Itakuwa ni dalali wewe, Katafute pesa acha kupigia mahesab vya mwanaume mwenzako.
 
Ni leo tu au jana ndio kuna mawe yametoka ambayo yangeweza kuwekwa kwenye kumbukumbu ya nchi eti, come on usifanye kuwa kama leo ndio umesikia kuna madini yanayoitwa tanzanite, sababu hii haina mashiko, tunaangalia faida ya mtu mmoja katika maisha yake anafaidikaje na jasho lake kwa kulipata jiwe hilo kupitia soko sio akubali tu bei anayopewa.

Kwenye kilimo serikali ilisema watu wapange bei wanazoona zina wafaa kuuza mazao sio bei tu inayoletwa ambayo ni kandamizi.
Lini ulisikia kuwa kuna mawe makubwa zaidi ya lile la kilo 3 ambalo liliuzwa zamani kabla ya hayo mabadiliko? nionyesha lini na wapi?
Kuhusu madini unaweza kuwa mwanafunzi wangu, so acha dharau.
 
Yaani mm niwekeze niwekeze tsh 7 halafu nipate jiwe la sh 50 niiuzie nchi kwa tsh 10 kisa uzalendo ungese huo kama wanataka mawe si nao wana chimba
Kuna watu walalamishi sana.
Jua kuwa kuna baadhi ya vitu hata viwe na thamani kiasi gani huwezi uza kutokana na umuhimu wake kwako. Kwa mfano huwezi kumtoa mkeo kwa mtu mwingine sababu huna pesa au kutaka sifa hata kama una uwezo.

Kwa ukubwa wake na vile yanapatikana tz pekee, ingekuwa ni ujinga hayo madini yanunuliwe na mtu au kampuni binafsi ambayo ingeweka kwenye makumbusho zao na kupata zaidi.

So ilikuwa na lazima serikali kuyanunua hayo ili kuweka kumbukumbu kwa taifa hili. Sometimes, usiangalie faida tu, angalia na taifa lako. Hayo sasa moja ya utambulisho la taifa.

Na nakushauri, usichukie sababu amenunua jiwe, hata ingekuwa cdm ndio wanaongoza nchi kwangu wangekuwa wamefanya kitu cha maana sana sababu ni utaifa wetu kwanza.
 
Yaani mm niwekeze niwekeze tsh 7 halafu nipate jiwe la sh 50 niiuzie nchi kwa tsh 10 kisa uzalendo ungese huo kama wanataka mawe si nao wana chimba
Unajua thamani ya gemstone ipo wapi? Maana naona wengi mnaongea kama mmeshikiwa akili.

Unajua nini kinachoipa thamani gemstone yoyote? Je, una uhakikia hii ilikuwa na thamani hizo?
 
Back
Top Bottom