Kahindi95
Member
- Mar 7, 2019
- 31
- 100
Kumekuwa na mfumuko mkubwa sana wa gharama za maisha sasa mathalani lita moja ya mafuta ya kula 2015 iliuzwa kati ya tsh 1500 hadi 2200.
Leo inauzwa 5500 hadi 6500. Hali hii ni kwa kila bidhaa sokoni si Unga, Michele, sabuni, nishati ya kupikia, nguo n.k bei hazikamatiki sokoni!
Serikali kwa kuliona hili Mwaka 2022 iliboresha posho na nights za maafisa almost mara mbili ya zile za awali, Mwaka 2023 ikaboresha posho za wabunge na mawaziri almost marambili ya zile za awali, yaani kikao kimoja Sasa mbunge au waziri anapata posho Tsh. 600,000/- au zaidi.
Serikali imeboresha mishahara ya wabunge kutoka mil 12 hadi mil 18+ kwa mwezi!
Lakini serikali hii haijaona umuhimu wa kuwatizama watumishi wa chini kama wauguzi, madaktari,polisi na waalimu kabisaa!
Imagine mwalimu analipwa take home ya Tsh 350,000/- kwa mwezi na Hana posho yoyote kazini kwa mwezi mzima. Na serikali imejikita Katika kuboresha maposho na mishahara ya maafisa, wakurugenzi, wabunge na mawaziri, inamaana serikali hii ya Samia haiwatambui kabisa watumishi wa chini wanaoihudumia jamii?
Mbaya zaidi hao wenye maslahi bora na wanaoboreshewa kila siku maslahi yao, wakistaafu wanapata pensheni zao kamili, na Hawa waalimu wakizeeka wanatandikwa na kikokotoo wafe kwa sukari na pressure!
Rais Samia na wapambe wako is this your real intention zako kwetu?
Kila kukicha mnaongeza Kodi na tozo kwenye bidhaa muhimu, vitu vinapanda bei sokoni kwa Kasi yaajabu, huku salary slip za waalimu ziko vile vile miaka nenda rudi, Rais Samia unataka tukueleze kwa kutumia lugha gani utuelewe wewe na wasaidizi wako?
Imefika hatua Sasa kazi ya ualimu imekuwa ni kazi ya kifukara sana hata kwenye jamii, mwalimu Sasa anadhaulika na kila mtu, kuanzia serikali yenyewe Hadi jamii nzima inatudharau sana waalimu kutokana na unyonge wetu!
Kwa mshahara anaolipwa mwalimu na Hali ya maisha ilivyo, hivi Sasa waalimu ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa mikopo umiza, mwalimu Hana matumaini na mshahara, Hana matumaini na pensheni. Kwa ujumla waalimu tumekuwa mahohehahe. Na serikari inafurahia.
Hofu yangu kubwa ni kwamba malalamiko haya ya waalimu yanavyozidi kupuuzwa na serikari pamoja na jamii! Madhara tutayaona very soon kwa watoto wetu. Huwezi kutengeneza waalimu fukara wenye msongo wa mawazo Kisha utarajie waalimu hao wakuandalie taifa Bora la kesho!
Tuiambie serikali iache mara Moja ukandamizaji huu au tukae kimya tusubiri matokeo ya tunachokipanda!
UALIMU NI KAZI SI WITO! MWALIMU ANAFAMILIA PIA KAMA ILIVYO KWA WABUNGE NA MAAFISA, MWALIMU ANASTAHILI MASLAHI BORA ALITUMIKIE TAIFA LAKE KWA ARI.