Kwanini serikali haiwathamini wanafunzi wa shule za msingi Tanzania?

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,583
Reaction score
4,009
Mimi ni mkazi wa majiji mawili Tanzania. Dar es salaam na Arusha. Wanangu ambao wote ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanapitia matatizo makubwa sana ya usafiri wa kwenda na kutoka shule.

Dar- mwanangu anaondoka saa 11 asubuhi na mpaka sa Moja hajapata mwendokasi kituoni na mwendokasi ukifika ni wanagombea mpaka sasa anatembea kwa kuchechemea, kwa kuuumia mguu wakati akigombea kupanda kwenye mwendokasi.

Mwanangu ambae ni mrembo na tayari ameshauvunja ungo wake ikifika jioni anakaa kituoni tangu saa kumi mpaka hata saa mbili usiku na Wala serikali haijali na haicheki na wowote.

Yani mwanangu kachoka na haya maisha kabisa, na nayaona maisha yake yapo hatarini ama kwa kurubuniwa na wenye vitambi ama kwa kudhuriwa na watu wabaya hiyo mida mibaya anayotembea kwa sababu tu serikali imeshindwa kumpatia na kumhakikishia usafiri wa uhakika.

Kwingineko wanangu wengine wapo Arusha ambapo kuna 'ruti' ambayo hice hamna zipo tu bajaji ambazo zinabeba watu wanne na hazikubali kutoza nauli elekezi ya mia mbili kwa wanafunzi hali inayopelekea wanafunzi kutembea kwa mwendo mrefu hivyo kuchelewa kufika nyumbani wakiwa wamechoka kweli.

Bajaji sio daladala Bajaj ipo kwenye category ya tax, ni chombo chenye magurudumu matatu ambacho sina hakika kama kina chases.

Mnadhan mzazi anapata wapi nauli ya kumpa mtoto ya mtu mzima Kila siku na wanenu wanapanda mabus yenye rangi ya njano? Ina maana serikali ya hapo Arusha haijui na hailioni hili tatizo ikahakikisha daladala zinarudi kwenye hiyo njia Ili kutoka maisha ya wanafunzi wengi wanaotegemea hizo barabara?ama hizi bajaji ni miradi ya watu flan ambao hawagusiki?

Serikali hamlipendi Taifa la kesho. Asanteni.
 
Tafuta hela usomeshe watoto shule nzuri na wawe wanatumia school bus
Mambo ya kulalamika ni ujinga tu
Hao watoto kuna mtu kakulazimisha kuzaa na unataka ulelewelewe na serikali Wewe ndio unatakiwa uwapaambanie watoto wako na sio vinginevyo
 
Si wanafunzi tu wasiothaminiwa bali na wewe baba/mama yao. Imagine gharama iliyotumika ku fund kinacho itwa uchaguzi wa sasa, mfano mabango pekee niliona of money zimeteketea, USISHANGAE BY JANUARI MWAKANI SEREKALI HII ILA KULAZIMISHA KUCHANGIA 20,000/- YA MADAWATI.
 
Mimi ni mkazi wa majiji mawili Tanzania. Dar es salaam na Arusha. Wanangu ambao wote ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanapitia matatizo makubwa sana ya usafiri wa kwenda na kutoka shule.

Dar- mwanangu anaondoka saa 11 asubuhi na mpaka sa Moja hajapata mwendokasi kituoni na mwendokasi ukifika ni wanagombea mpaka sasa anatembea kwa kuchechemea, kwa kuuumia mguu wakati akigombea kupanda kwenye mwendokasi.

Mwanangu ambae ni mrembo na tayari ameshauvunja ungo wake ikifika jioni anakaa kituoni tangu saa kumi mpaka hata saa mbili usiku na Wala serikali haijali na haicheki na wowote.

Yani mwanangu kachoka na haya maisha kabisa, na nayaona maisha yake yapo hatarini ama kwa kurubuniwa na wenye vitambi ama kwa kudhuriwa na watu wabaya hiyo mida mibaya anayotembea kwa sababu tu serikali imeshindwa kumpatia na kumhakikishia usafiri wa uhakika.

Kwingineko wanangu wengine wapo Arusha ambapo kuna 'ruti' ambayo hice hamna zipo tu bajaji ambazo zinabeba watu wanne na hazikubali kutoza nauli elekezi ya mia mbili kwa wanafunzi hali inayopelekea wanafunzi kutembea kwa mwendo mrefu hivyo kuchelewa kufika nyumbani wakiwa wamechoka kweli.

Bajaji sio daladala Bajaj ipo kwenye category ya tax, ni chombo chenye magurudumu matatu ambacho sina hakika kama kina chases.

Mnadhan mzazi anapata wapi nauli ya kumpa mtoto ya mtu mzima Kila siku na wanenu wanapanda mabus yenye rangi ya njano? Ina maana serikali ya hapo Arusha haijui na hailioni hili tatizo ikahakikisha daladala zinarudi kwenye hiyo njia Ili kutoka maisha ya wanafunzi wengi wanaotegemea hizo barabara?ama hizi bajaji ni miradi ya watu flan ambao hawagusiki?

Serikali hamlipendi Taifa la kesho. Asanteni.
October 29 unatiki au unatoka?
 
Nyama choma na Land Rover festival ndio kipaumbele,
God forbid watoto wako wasije kuwa WADUDU.
Chuga hip hop imekufa. RIP. 💐
 
Tafuta hela usomeshe watoto shule nzuri na wawe wanatumia school bus
Mambo ya kulalamika ni ujinga tu
Hao watoto kuna mtu kakulazimisha kuzaa na unataka ulelewelewe na serikali Wewe ndio unatakiwa uwapaambanie watoto wako na sio vinginevyo
Vidole havilingani. Halafu we mpuuzi kweli
 
Tafuta hela usomeshe watoto shule nzuri na wawe wanatumia school bus
Mambo ya kulalamika ni ujinga tu
Hao watoto kuna mtu kakulazimisha kuzaa na unataka ulelewelewe na serikali Wewe ndio unatakiwa uwapaambanie watoto wako na sio vinginevyo
Umeandika pumba.
Duniani hatulingani, hata vidole havilingani.
Na ukweli ni kwamba anayeandika pumba kichwani kumejaa pumba.
 
Nyama choma na Land Rover festival ndio kipaumbele,
God forbid watoto wako wasije kuwa WADUDU.
Chuga hip hop imekufa. RIP. 💐
Warangi na wanyaturu wamezaliana pale chuga hatari, ladha imekuwa kama ya barabara ya vumbi sio Tena uhardcore wa chuga. Wale ma og wamehamia kimara na mbezi daresalam. Jimbo limedondokea kwa mkolomije kilaiiinii kwa kupewa bia Moja na finyango tatu ya nyama
 
Wewe ndo umezagamua, wewe ndo umeruhusu mtoto kuzaliwa.
Halafu unataka serikali iwajibike kwa machaguo yako ya kumpeleka mtoto shule ya mbali na kwao.
 
Back
Top Bottom