Kumekuwa na wimbi kubwa la vifo vya ugonjwa wa korona karibia kila kona ya taifa hili kama wimbi la tatu lilivyokuja kwa kasi kubwa lakini ukiangalia kwasasa maambukizi ya virusi vya korona yanaenea kwa uzembe sana, utakuta watu wanajua wazi kuwa huyu mtu kafariki na virusi vya korona na hospitali wameandaa maiti kwa kuzingatia masharti ya mgonjwa wa korona lakini cha ajabu ni kwamba japokuwa hiyo maiti imefungwa na mfuko wa plastiki kwa lengo la kuzuia virusi lakini hiyo maiti inapoenda nyumbani kwa marehemu familia inamuaga kama vile huyo mtu kafa na malaria yani sijui tunaelekea wapi , huo mfuko wanaufungua na kumuaga huku wengine wakiangaika kuiweka sawa bila tahadhari.
USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA SERIKALI ISIKWEPE HILI JUKUMU
Naishauri serikali kuwa kwa vile tayari tumekubali kuwa tuna ugonjwa wa korona nchini na kwa vile tunatafuta takwimu la wagonjwa na vifo basi kazi hii ya kuzika wale waliokufa na korona wote wazikwe na serikali hii iwe kwa lazima na litolewe tamko rasmi la serikali , vnginevyo tutaambukizana sana na tutakufa sana , serikali hisikwepe hili jukumu naombeni wote tupige kelele kuwa serikali izike wafu wa Corona.