Kwanini Serikali haiziki maiti zilizokufa kwa Corona?

SOPINTO

Senior Member
Joined
Oct 19, 2020
Posts
153
Reaction score
388
Kumekuwa na wimbi kubwa la vifo vya ugonjwa wa korona karibia kila kona ya taifa hili kama wimbi la tatu lilivyokuja kwa kasi kubwa lakini ukiangalia kwasasa maambukizi ya virusi vya korona yanaenea kwa uzembe sana, utakuta watu wanajua wazi kuwa huyu mtu kafariki na virusi vya korona na hospitali wameandaa maiti kwa kuzingatia masharti ya mgonjwa wa korona lakini cha ajabu ni kwamba japokuwa hiyo maiti imefungwa na mfuko wa plastiki kwa lengo la kuzuia virusi lakini hiyo maiti inapoenda nyumbani kwa marehemu familia inamuaga kama vile huyo mtu kafa na malaria yani sijui tunaelekea wapi , huo mfuko wanaufungua na kumuaga huku wengine wakiangaika kuiweka sawa bila tahadhari.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA SERIKALI ISIKWEPE HILI JUKUMU
Naishauri serikali kuwa kwa vile tayari tumekubali kuwa tuna ugonjwa wa korona nchini na kwa vile tunatafuta takwimu la wagonjwa na vifo basi kazi hii ya kuzika wale waliokufa na korona wote wazikwe na serikali hii iwe kwa lazima na litolewe tamko rasmi la serikali , vnginevyo tutaambukizana sana na tutakufa sana , serikali hisikwepe hili jukumu naombeni wote tupige kelele kuwa serikali izike wafu wa Corona.
 
Naunga mkono hoja ....watu wanaachiwa waambukizwe kiholela holela sana
 
Kwani mwendazake Meko, Kijazi, Mfugale, Seif et el hawakuzikwa na serikali
 
Kuna ujinga sana unaendelea, wewe uliona juzi juzi waziri alitangaza taarifa za wagonjwa wa corona, cha ajabu hakutangaza vifo. Sasa jiulize kwanini?, kama wameamua kutangaza kwanini hawatangazi vifo?
 
Serikali ishatoa miongozo ya uzikaji wa waliokufa kwa korona.
 
Kuna ujinga sana unaendelea, wewe uliona juzi juzi waziri alitangaza taarifa za wagonjwa wa corona, cha ajabu hakutangaza vifo. Sasa jiulize kwanini?, kama wameamua kutangaza kwanini hawatangazi vifo?
Wakitangaza vifo tutatafutana
 
Wakitangaza vifo tutatafutana
Hapana, huu utaratibu wa kufichana ukweli ndio maana watu hawaoni umuhimu wa kuchanja kwakuwa ugonjwa wenyewe hauna madhara. Mtu anakuambia wewe umeshasikia nani kafa kwa corona?

Yaani eti wamekufa watu 21 toka 2020, unaamini hivyo?, rais mwenyewe kasema Moshi, Mwanza watu wanakufa, lakini cha ajabu hawatangazwi.

Dunia nzima iko hivyo mbona watu hawakimbiani, sana sana itasaidia watu kujilinda na kutilia maanani maelekezo yanayotolewa na wataalamu wetu.
 
Kwani mwendazake Meko, Kijazi, Mfugale, Seif et el hawakuzikwa na serikali
hawa 29 waliotangazwa uliona wamezikwa na serikali? hapa hatusemei ngazi ya viongozi nasemea raia yoyote wa kitanzania serikali kupitia wizara ya afya ifanye jukumu lake vingine kuna siku muda utafika tutatafutana hapa nchini , ile ya India itakuwa ndogo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…