Inasikitisha sana kuwa serikali yetu iko kimya sana kuhusu hii ishu.
Nini kifanyike ili wananchi wa Tanzania wasikumbane na madhila ya namna kama hii?
Elimu itolewe kuhusu utapeli wa mitandaoni.
Unataka Elim ya namna gani?
Tukiwa wadogo tulifundishwa Hadithi ya "Abunuas" Kuna siku aliazima sufuria , siku anairudisha kaweka na kasufuria kadogo.
mwenye sufulia yake ,akauliza kulikoni mbona umereta mbili? Akajibiwa ilikubwa imezaa hako kadogo.
Siku nyingine alivyo azima hakulejesha , mwenye sufuria akaenda kuulizia kuna nini sufuria hairudishwi? Akajibiwa " imefariki" kutahamaki akapewa swali mbona ilivyo zaa hukusituka ? Kila chenye kuzaa kina kifaa.
Hii Hadithi hukufundishwa?
Kitabu Cha "KUSADIKIKA" Marehem Shaban Robert. Amesimlia kisa Cha mtu mwenye tamaa na uvivu wa fikira alie fanyiza mkataba na mwenzake mwenye bahati ya kuomba na kupta alicho kiomba kwa Mola wake bila kuchelewa.
ndani ya mkataba huo kipengere kikuu ni ;Kila kitakachoombwa watagawana sawa. Jamaa akukubali kiroho safi baada ya mkataba kisainiwa ,akainua mikono juu akaomba wapewe upofu maana yeye kachoka kuona maovu yanayo tendeka Duniani.
Hii nayo hukufundishwa?
Kuna video (I )mwanachuo analalama , kawaunganisha wa nachuo wenzake , na WA hadhili wake. Sasa tujiulize mtu alie aminiwa nakukabiziwa vijana, aendeleze bongo zao ziweze kuchanganua na kung'amua nae anatapeliwa Kindwanzi namna hii kweli?
Kiujumla hakuna wakuaelimisha wajinga wenye PhD.
DEC ilitisha kua funzo kubwa , lakini Cha ajabu hata miaka kumi natani haijapita mmepigwa Tena. Wacha mambo yaende hivyo.
Safari ya mwenye mafanikio ,inaitaji msindikizaji asie na tamaa.