Kwanini serikali iliamua kufunga shule kwa ajili ya sensa?

mzamifu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2010
Posts
6,400
Reaction score
3,853
Serikali ilifunga shule zake zote za msingi na sekondary kuanzia August 3 hadi September 9/2012.

Sababu zilizotolewa zilikuwa walimu wangeshiriki katika zoezi la sensa. Sasa kuna ushahidi kwamba shule nyingi tu hazijatoa mwalimu hata mmoja kwa ajili hiyo. N

yingine walimu wawili hadi watano huku walio wengi wamebaki. Sasa kuna haja gani ya kufunga shule?

JAMANI MBONA SIASA ZINAZIDI? HATA MTOTO MDOGO ANAONA UKWELI KUWA WALIMU WAMEKOMOLEWA. Sawa waache wapumzike lakini subiri matokeo!
 
Hilo la kufungwa shule lilikuwa kwenye mpangilio hata kabla ya hicho unachofikiri ndio sababu.
 
suala la kufungwa shule lilishajulikana tangu mwanzoni mwa mwaka,kwa ratiba kabisa,sasa unataka shule zizifungwe kwa sababu walimu wengi hawashiriki sensa?na leta kielelezo kinachosema sensa ni lazima walimu washiriki kwa wingi!wewe unadhani hao wanafunzi hawatakiwi kuhesabiwa makwao?
 
sawa lakini kawaida shule hufungwa June kuelekea July. Walimu walitakiwa waandae kazi zao kwa mwelekeo huo kwani wangeshiki sensa. sasa hilo halipo. kwamba kama ni kuwapumzisha kwani wafanyakazi wote na wamepewa likizo ili wahesabiwe. unapaswa kuchanganua mambo kabla ya kusema tu. utaratibu huu umewasumbua sana wanafunzi wanaojiandaa na mitihani sasa wengine wanahaha kutafuta tuition mitaani
 
si kwamba nataka shule zisifungwe hoja yangu ni kwanini lengo la awali limegeuka? watu wakubwa wanapanga halafu mwisho wanapangua bila sababu za msingi au basi wawe wazi
 
ndio serikali hufunga shule kwa muda ili kuwatumia walimu katika kazi hiyo na wala si kwa kusudi la kuwawezesha wahesabiwe au wanafunzi wahesabiwe. ndiyo maana sekta zote zingine zinaendelea na kazi kama kawaida. tatizo ni kwamba wameleta usumbufu kwa wanafunzi na walimu maana zilipofunguliwa july kabla ya wanafunzi kukaa sawa mara likizo huo umekuwa pia ni usumbufu. ni bora walimu wangeendelea na hiyo kazi ingeeleweka vingine
 
mwezi wa 6 hawakufunga sasa unataka wasipumzike mwaka huu

Walifunga mkuu 2 wks, shule nyingine walipofungua wakakaa 1 wk then wakaanya mitihani then baada ya mtihani mgomo, baada ya mgomo wamefunga shule.

In short mhula huu hawakusoma kabisaa, ingawa private zingine wanaendelea kupiga shule hadi 24 ndo wanafunga. Swali langu ni kwamba mbonavyuo vya ualimu wako chuoni wao ndo hawapaswi kuhesabiwa makwao?

Kuna mwnangu yuko english medium day, but baada ya shukle kufungwa wako camp boarding wanasoma, nao je?

In short hii serikali yetu ina matatizo ya kufikiri. Na ndo maana inafika mwisho wa mwaka silabasi zinakuwa uncovered, na failures wanaongezeka.

Mungu wasaidie viongozi wa Tanzania ktk uwezo wa kufikiri.
 
si kwamba nataka shule zisifungwe hoja yangu ni kwanini lengo la awali limegeuka? watu wakubwa wanapanga halafu mwisho wanapangua bila sababu za msingi au basi wawe wazi

lengo limegeukaje wakati lengo ni kuwezesha sensaifanyike?sasa sensa si itafanyika?au unadhani walisema shule zifungwe ili walimu wasimamie sensa?haikuwa hivyo jamani msiseme yasiyomo,shule zimefungwa kuwezesha zoezi la sensa kufanyika.
 
sawa lakini kawaida shule hufungwa June kuelekea July. Walimu walitakiwa waandae kazi zao kwa mwelekeo huo kwani wangeshiki sensa. sasa hilo halipo. kwamba kama ni kuwapumzisha kwani wafanyakazi wote na wamepewa likizo ili wahesabiwe. unapaswa kuchanganua mambo kabla ya kusema tu. utaratibu huu umewasumbua sana wanafunzi wanaojiandaa na mitihani sasa wengine wanahaha kutafuta tuition mitaani

wafanyakazi wao katika maeneo yao ya makazi ,wanafunzi je wao kwenye maeneo yao ya makazi?au unadhani kila mwanafunzi anasoma ktk eneo la makazi ya familia yake .
 
suala la kufungwa shule lilishajulikana tangu mwanzoni mwa mwaka,kwa ratiba kabisa,sasa unataka shule zizifungwe kwa sababu walimu wengi hawashiriki sensa?na leta kielelezo kinachosema sensa ni lazima walimu washiriki kwa wingi!wewe unadhani hao wanafunzi hawatakiwi kuhesabiwa makwao?

Si lazima ulale kwako ndo uhesabiwe,tena shuleni ingekua rahisi kuwahesabu hata watoto ambao wazazi wao ni UAMSHO,we fikiria na watakao lala guest nao ni nyumba zao?
 
you have a very strong point there..
 
suala la kufungwa shule lilishajulikana tangu mwanzoni mwa mwaka,kwa ratiba kabisa,sasa unataka shule zizifungwe kwa sababu walimu wengi hawashiriki sensa?na leta kielelezo kinachosema sensa ni lazima walimu washiriki kwa wingi!wewe unadhani hao wanafunzi hawatakiwi kuhesabiwa makwao?

Wewe kweli bongo lala! Yani pamoja na matangazo yote haya bado haujafahamu utaratibu wa sensa ulivyo!!!??? Eti "Unadhani hao wanafunzi hawatakiwi kuhesabiwa makwao?" Nani alikwambia lazima mtu ahesabiwe kwao kama vile unavyohesabu ng'ombe zizini! Mtu anahesabiwa alipolala huo usiku wa kuamkia makwao. Hivyo kama mwanafunzi yuko shule ya bweni angehasabiwa shule na wa kutwa angehasabiwa alipolala kama nyimbani au kwenye mageto waliobanga!

Mkuu jaribu kutia akili kidogo! Kama shule zinafunguliwa tarehe 10 septemba na darasa la saba wanafanya mitihani tarehe 12 na 13 Septemba unategemea nini?
 
...ivi inakuaje mawazo mazuri na mazito kama haya yanapatikana hapa JF ..na cabinet nzima haikuliona hili?? Damn..
Ivi washauri wa RAISI wanamshauri nini??
Mh. Mnyika hakukosea.
 
Ni kweli kabisa suala la kufunga shule lilikuwa wazo toka awali, lakini kukmbuka ilikuwa ni kwa sababu ya kupisha zoezi zima la sensa hasa ukizingatia kwamba waalimu ndio walikuwa wawe watendaji wakuu katika zoezi hilo.
Sijui kwa nini watanzania sisi ni wepesi wa kusahau, hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya viongozi siku zote,lakini ghafla mpango ulianza kubadilika baada ya kusikia na kutokea mgomo wa walimu, na pia tukikumbuka semina kwa makalani wa sensa ilikuwa ianze tar. 6 august lakini ikazogenzwa mbele, na tunasikia tetesi kuwa lengo ilikuwa ni kupata nafasi ya kuwaengua waalimu na kuwabakiza wachache kama ushahidi.
Fanya utafiti mdogo tu utagundua kuwa idadi ndogo sana ya waalimu wamechukuliwa na wengine ni marafiki zetu tunapata taarifa kila siku.
Hoja ya msingi ni kwamba wangewaacha waalimu walio wengi ambao kwa sasa wapo mitaani wangeendelea na wanafunzi kwani zoezi lingechukuliwa kama waalimu wanaokwenda kusaisha mitihani.
NB. Nchi yetu siasa nyingi hivyo yahitaji sana jicho la pili au la tatu kuona na kutambua mchezo harisi.
 
Wewe kweli bongo lala! Yani pamoja na matangazo yote haya bado haujafahamu utaratibu wa sensa ulivyo!!!??? Eti "Unadhani hao wanafunzi hawatakiwi kuhesabiwa makwao?" Nani alikwambia lazima mtu ahesabiwe kwao kama vile unavyohesabu ng'ombe zizini! Mtu anahesabiwa alipolala huo usiku wa kuamkia makwao. Hivyo kama mwanafunzi yuko shule ya bweni angehasabiwa shule na wa kutwa angehasabiwa alipolala kama nyimbani au kwenye mageto waliobanga!

Mkuu jaribu kutia akili kidogo! Kama shule zinafunguliwa tarehe 10 septemba na darasa la saba wanafanya mitihani tarehe 12 na 13 Septemba unategemea nini?

...Na hata hao 4m4 hasa maskini wanaosoma shule za kata (wasio na access na tuition) wanaoanza mitihani mapema october wataathirika sana kwa sababu wakifungua september 10 ni mfululizo wa mishemishe za graduation kuanzia za dini hadi ile ya shule ya kijumla na wakija kushtuka mitihani hii hapa.
 
Back
Top Bottom