Kwanini serikali isichapishe Pesa nyingi za kutosha? Gharama za kuchapisha Pesa Kwa nchi zipoje?

mkuu dmkali ingia google upate ABC za uchumi kuhusiana na hicho unachokihoji sio lazima usome uchumi darasani ili ujue kuhusu uchumi.
 
An increase in the quantity of money,leading to a devaluation of existing money!
 
Pesa haichapishwagi tu kama gazeti ati kisa imeadimika. Pesa inapimwa uwepo wake kwa thamani iliyobeba.

Ndio maana hapo nyuma lipokuwa inaibiwa na kudokolewa hovyo mnajionea kuwa watu wengi walilemaa na kushindwa kushiriki katika shighuli za uzalishaji wa kiuchumi.

Ila kwa sasa inakamuliwa kwa kasi sana na kurejeshwa ilipotoka......hii itawapa watu akili ya kuitafuta kwa njia halali bila kufoji au kuiba.


Kumbuka ni mwaka wa pili tu huu tokea iadimike. Sitegemei watu ambao wameishi zaidi ya miaka 20 kwa dili za udokozi wanaweza kujirekebisha chap hivyo, itachukua muda ila watu watakaa sawa na hatimaye tutarejea katika mfumo wa kutafuta kwa kufanya kazi .

Hapa penyewe ninavyozungumza kuna biashara mpya zinafunguliwa kila uchao na watu wanafanya biashara mambo yanakwenda.
 
Japi muuliza Swali ni mlevi lakini nipo upande wake nami nataka kujua
 
Nitasoma digrii za mambo mangapi mkuu ? Mambo mengine tufahamishane hapa
Kuna vitu ambavyo any graduate anapaswa kuvijua mojawapo ni basic knowledge ya economics Ila kuuliza ni vyema.....mimi sio mwanauchumi ila from my basic knowledge ya economics ni hivi...
Ukiprint pesa unaongeza kwenye mzunguko wa fedha pesa isiyo na dhamani. Hii hupelekea mfumuko wa bei na hatimaye kudorora kwa uchumi
Jaribu kuassume serikali imeprint mabilioni ya fedha halafu ikagawia wananchi wake ...je watafanya kazi kweli?Kazi itakua si ya muhimu kwao kama ni chakula na mahitaji mengine watanunua .Je hao wakuwauzia mahitaji watukua wapi wakati kila mtu ameshapewa pande lake kapiga hivi....endelea kuimagine yatayotokea ukifanya hivyo...
 
Asante mkuu Kwa maelezo! Vipi kuhusu swali LA pili na LA tatu
 
Dhamani[emoji777]

Thamani [emoji818]
 
Mkuu pesa ikiwa nyingi mtaani thamani yake hupungua hivyo kuongeza gharama za bidhaa na huduma kwakua pesa ipo nyingi tu ya kutosha mtaani watu wanaweza kumudu kununua bidhaa na huduma kwa bei kubwa hivyo kupoteza thamani ya pesa

Kwahiyo inashauriwa pesa iwe 'relative scarce' kwa maana siyo nyingi sana wala siyo chache sana ili kuzuia mfumuko wa bei na kuporomoka kwa thamani ya shilingi dhidi ya pesa nyingine za kigeni,

Vivyo hivyo ikiwa chache sana husababisha deflation yaani kupungua mno kwa bei ya huduma na bidhaa hivyo kuathiri thamani ya kazi na shilingi vile vile. Kwahiyo si suluhisho hata kidogo kuchapisha noti nyingi ili kufanya maisha kuwa bora,

Fikiri kila mtu akiwa milionea bei za bidhaa zitakuaje? Yaani husemi hata nipunguzie, je production sector itakuaje? Gharama za kuajiri zitakua juu sana hivyo kusababisha bidhaa zizalishwe kwa gharama kubwa na kuuzwa kwa bei kubwa, je fikiri kuhusu pesa ikiwa chache mnovkiasi kwamba mshahara mkubwa zaidi iwe elfu 50 je utakua unaumiza mwili kiasi gani kupata milioni 1? Hayo ni machache tu kwa sasa.
 
Ungekuwa umesom uchumi swali kama hili ni simple sana ukichapisha pesa nyingi na zikaingia ktk mzunguko kinachotokea asilimia kubwa ya watu wanakuwa na pesa nyingi ambayo inasababisha mfumuko wa bei kwa sababu kila mtu anapesa hapa usishangae kilo 1 ya sukar ikauzwa 20,000 so bot wanamfumo wao wakuchapisha fedha baada ya mda fulana kutokana na uchumi ulivyofulia..

Thaman ya pesa yako inatokana na wewe unauza nini ktk mataifa mengine au ni foreigner wangapi wanaingia nchini na kudemand pesa yetu..
 
Kwasababu umesema upo bar unasherekea mwaka mpya acha tuungane na kuimba iyena iyenaa...
 
Gharama zipo, na kuna viwanda vipo kabisa mataifa ya nje (sikumbuki nchi), vinalindwa sana na shughuli hufanywa kwa umakini sana. Hivyo basi gaharama za uchapishaji zipo sana tu maana pesa nayo ni kama document nyingine ya kiserikali inayotumika katika shughuli za kinaendeleo. Usiri wa kuichapisha unafanania na ule wa karatasi za kupigia kura, mitihani ya taifa, kwa maana ni nyaraka nyeti sana ambazo kuna unyeti sana katika kupatikana kwake na malipo yake hufanyikaje.



Vigezo ambavyo hutumika katika kuchapisha pesa serikalini ni pale inapotokea BOT wamegundua kuna upungufu wa pesa katika mzunguko ili hali shughuli za uzalishaji zimekuwa. Mfano, assume, serikali mwaka 2000 ilitoa pesa katika mzunguko zenye thamani ya trilion tano, halafu miaka kumi baadae shughuli za uzalishaji zikaongezeka na ukichukua thamani ya bidhaa na huduma katika uchumi zinafikia lets say trilion sita au nane then serikali wanalazimika kuchapa tena pesa zingine na sarafu ili kufidia upungufu huu amasivyo itaharibu uchumi utakuwa unadororesha uzalishaji.

Vigezo vingine ni kama speed ya uchakavu wa pesa especially noti maana kila raia ana namna yake ya kutunza pesa ndio maana ni kosa la jinai ukichana noti au kuichoma, au kuiharibu kwa namna yoyote.

Kubadilika kwa alama muhimu za utambuzi wa fedha halali, kwa maana ya zile alama za utambuzi. Mfano noti za elfu kumi, elfu tano, zilibadilishwa hivi juzi kati ila ni watu wachache sana walijua hiyo kitu.

sababu zipo nyingi za kwann serikali wanachapa noti mpya.
 
Hahaha

Akina Bhakhresa na akina Mengi wajitengenezee kabisa viwanda vya kuchapa noti waache kuhangaika na uzalishaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…