Kwanini serikali isichapishe Pesa nyingi za kutosha? Gharama za kuchapisha Pesa Kwa nchi zipoje?

"Zikoje" sio zipoje
 
Thamani ya pesa ya taifa moja kwenda jingine hupishana kutokana na muingiliano wa shughuli za kiuchumi katika ya taifa moja na mengine kibishara katika manunuzi na mauzo.


Mfano, dollar ya marekani katika miaka ya uhuru ilikuwa ni sawa na shilling tano ya tanzania. Ila siku zilipozidi kwenda alipozidi kutushika shika makalio sisi na mataifa mengine na kutuzidi katika mbinu za kiuchumi kwa maana ya export na riba anazoweka katika madeni yake anayotudai anakuwa anajeuri ya kucheza na sera za serikali kupitia benki kuu kuiagiza kuzipangia benki local kiasi cha riba cha kuwachaji wanaokopa na hivyo basi kuubaka uchumi wetu.

Ila pia thamani ya pesa ya sehemu ina uhusiano wa moja kwa moja na ukuaji wa uchumi wa ndani wa hilo tafita. Kwa mfano kwa hapa tz kama tutaanza kuzalisha bizaa zetu na kununua vitu vya ndani tu, itashusha matumizi ya dollar, na tukalipa madeni yote ya nje mataifa makubwa yatakosa uwezo wa kutupangia kwa kiasi kikubwa na hivyo uchumi wetu wa ndani utaanza kukua.


Mfano, ni kenya si unaona tunanunua vitu vingi tokea kwao, maziwa, majani ya chai, na vikorokoro kibao, hii inaharibu sana ushindani kati yetu na wao maana wao wanaendelea sisi wala hatuwauzii vitu vyenye thamani zaidi ya malighafi so wanatupita kila uchao.
 

Swali lako ni la msingi kasoro pale kwenye zipoje. Sasa kusaidia tuanzie mahali fulani hivi maana unachokiuliza ni cha darasani na huchukua sio chini ya siku mbili kwa mwanafunzi kukielewa kama hajawahi kukisikia hata siku moja. Tutaenda taratibu ili kushtua uelewa wako. Kwanza jibu maswali machache kama ifuatavyo:
1. Sukari ikipotea madukani kitu gani hutokea kwenye bei ya sukari?
2. Simenti ikiwa nyingi sana dukani nini hutokea kwenye bei ya simenti?

Hebu jibu hayo kwanza halafu tutaendelea.
 
Kwa hio shilingi yetu ni nyingi kuliko dollar?
Dollar moja n sawa n shilingi ngapi?...bila shaka utakua umeelewa point yangu. .uchapishaj w hela nyingi hupelekea thamani y hela kushuka na mwisho n kudorora kwa uchumi...unawez kujikuta unabeba fuso ilojaa noti kwenda kununua kilo moja y njegere
 
kuchapisha pesa nyingi kuta sababisa mfumuko wa bei(inflation) hivyo itapelekea kuongezeka kwa bei ya bidhaaa n.k
Hahaaaaaa uongo inflation(mfumuko wa bei) unasababishwa na kuadimika kwa goods e.g mazao ya chakula,mazao ya biashara,mafuta ya kuchimbwa hivyo ni baaz n.k ila kuchapisha pesa nyingi itasababisha deflation(kushuka thaman kwa fedha)
 
Dollar moja n sawa n shilingi ngapi?...bila shaka utakua umeelewa point yangu. .uchapishaj w hela nyingi hupelekea thamani y hela kushuka na mwisho n kudorora kwa uchumi...unawez kujikuta unabeba fuso ilojaa noti kwenda kununua kilo moja y njegere
Nimekuelewa, ila swali ni je kwa sababu dola ina thamani kuliko shilingi yetu ina maanisha kiasi cha idadi za shilingi ni nyingi kuliko dollar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…