Kwanini Serikali isipige marufuku Kitchen Party?

Sijawahi kwenda kwenye kitchen party, hata sijui how it looks like, na wakati wa harusi yangu zaidi ya send off, sikufanyiwa kitchen party aisee my mom aliniambia malezi niliyokulea ni kitchen party tosha mwanangu ikabidi niwe tu mpole
 
Sijawahi kwenda kwenye kitchen party, hata sijui how it looks like, na wakati wa harusi yangu zaidi ya send off, sikufanyiwa kitchen party aisee my mom aliniambia malezi niliyokulea ni kitchen party tosha mwanangu ikabidi niwe tu mpole
Uko vzr Mkuu.
Kule sio pa kwenda.
Wanaweza kupindisha maelezo eti hii ni ya dini ooh hii haina sijui mambo hayo lkn mwisho ni kulekule.

Tamaa ya vitu ambavyo hata ukiwa na mume wako mtanunua mdogomdogo.
 
Sasa Mkuu kwanini ulienda kufanya huu utafiti peke yako?mi kichwa uwa kinauma sana,ungenipitia kidogo kingekaa sawa,ningeangaliaaaaa tu weeeeee ningeliondoka zangu kimya nimepona
 
Bibi yangu mmoja alishadadia hii kitu baada ya ukweni upande wa Tanga kutaka iwekwe na bajeti ya kuwalipa wadada wa baikoko kwenye kichern party ye alijua no michezo ya kawaida...mi niliwaonya hawakusikia....kimbembe walivoenda uko kicheni party yao mbona ukumbi waliachiwa watu wa Tanga tu....inasemekana wale watoto wa baikoko walifanya kufuru
 
Ya Ngoswe muachie NgosweπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Mlikataa Jando na Unyago mkaleta kitchen party sasa kaaeni kimya ndio madhara ya kuiga
 
Mwanaume usiruhusu mkeo mtarajiwa afanyiwe huo ujinga.

Kama ni Vyombo hata Adamu na Eva waliumbwa bila sufuria. Mtazipata tu
 
Ukiyafuta watakujia juu na mabango ya GENDA EQUITY , EQUALITY AND WOMEN EMPOWERMENT, na jinsi walivyo mafundi wa kuongea watakushinda tu! Mie nafkiri hayo mambo yangewekewa mwongozo ili watakaotoka nje ya mstari na wabebe gharama zake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…