Kwanini Serikali isipige marufuku Kitchen Party?

Wakuu hii kitu miaka ya 90 sikuwahi kuisikia. Sijui imetokea nchi gani.

Sioni kama wanafundishana mambo ya maana zaidi ya ukahaba na kuvizia vijizawadi.

Mwaka 2004 nimewahi kuzamia kitchen party ya walimu wangu kwa kujificha aisee walikuwa wanamfundisha yule Mwalimu mwenzao uhuni na ukahaba, sikuona kama ni mambo ya ndoa pale.

Pili washabiki wa hizi kitu ni wanawake walioachika, wasimbe wasio na mpango wa kuolewa, wanawake wanaotawala waume zao wasiofugika au kuonyeka. Watu kwenye maadili hawaungi Mkono kabisa hii kitu.

Juzi nikiwa mahala flank nawasikia Kikundi cha wakina mama wanaajipanga kuvaa robo tatu uchi kwenye kitchen party ila itabidi waondoke na madera home ili waume wao wasijue.

Kuna bibi wa heshima na maana sana lakini kumbe huwa anavua vinguo hadi kubaki na nguo ya ndani akiruka sarakasi kwenye hizo party, jimama moja linakatikia chupa hadi inazama nusu sirini.

Haya ni mafunzo ya zinaa na uasherati.

Nashauri kitchen I party zifutwe alafu hayo mambo mwanamke afundishwe na mama au Ndugu sake sirini tens kwa adabu.
Sijawahi kwenda kwenye kitchen party, hata sijui how it looks like, na wakati wa harusi yangu zaidi ya send off, sikufanyiwa kitchen party aisee my mom aliniambia malezi niliyokulea ni kitchen party tosha mwanangu ikabidi niwe tu mpole
 
Uko vzr Mkuu.
Kule sio pa kwenda.
Wanaweza kupindisha maelezo eti hii ni ya dini ooh hii haina sijui mambo hayo lkn mwisho ni kulekule.

Tamaa ya vitu ambavyo hata ukiwa na mume wako mtanunua mdogomdogo.
 
Wakuu hii kitu miaka ya 90 sikuwahi kuisikia. Sijui imetokea nchi gani.

Sioni kama wanafundishana mambo ya maana zaidi ya ukahaba na kuvizia vijizawadi.

Mwaka 2004 nimewahi kuzamia kitchen party ya walimu wangu kwa kujificha aisee walikuwa wanamfundisha yule Mwalimu mwenzao uhuni na ukahaba, sikuona kama ni mambo ya ndoa pale.

Pili washabiki wa hizi kitu ni wanawake walioachika, wasimbe wasio na mpango wa kuolewa, wanawake wanaotawala waume zao wasiofugika au kuonyeka. Watu kwenye maadili hawaungi Mkono kabisa hii kitu.

Juzi nikiwa mahala flank nawasikia Kikundi cha wakina mama wanaajipanga kuvaa robo tatu uchi kwenye kitchen party ila itabidi waondoke na madera home ili waume wao wasijue.

Kuna bibi wa heshima na maana sana lakini kumbe huwa anavua vinguo hadi kubaki na nguo ya ndani akiruka sarakasi kwenye hizo party, jimama moja linakatikia chupa hadi inazama nusu sirini.

Haya ni mafunzo ya zinaa na uasherati.

Nashauri kitchen I party zifutwe alafu hayo mambo mwanamke afundishwe na mama au Ndugu sake sirini tens kwa adabu.
Sasa Mkuu kwanini ulienda kufanya huu utafiti peke yako?mi kichwa uwa kinauma sana,ungenipitia kidogo kingekaa sawa,ningeangaliaaaaa tu weeeeee ningeliondoka zangu kimya nimepona
 
Bibi yangu mmoja alishadadia hii kitu baada ya ukweni upande wa Tanga kutaka iwekwe na bajeti ya kuwalipa wadada wa baikoko kwenye kichern party ye alijua no michezo ya kawaida...mi niliwaonya hawakusikia....kimbembe walivoenda uko kicheni party yao mbona ukumbi waliachiwa watu wa Tanga tu....inasemekana wale watoto wa baikoko walifanya kufuru
 
Ya Ngoswe muachie Ngoswe😂😂😂😂😂😂😂.

Mlikataa Jando na Unyago mkaleta kitchen party sasa kaaeni kimya ndio madhara ya kuiga
 
Mwanaume usiruhusu mkeo mtarajiwa afanyiwe huo ujinga.

Kama ni Vyombo hata Adamu na Eva waliumbwa bila sufuria. Mtazipata tu
 
Ukiyafuta watakujia juu na mabango ya GENDA EQUITY , EQUALITY AND WOMEN EMPOWERMENT, na jinsi walivyo mafundi wa kuongea watakushinda tu! Mie nafkiri hayo mambo yangewekewa mwongozo ili watakaotoka nje ya mstari na wabebe gharama zake!
 
Back
Top Bottom