Pre GE2025 Kwanini Serikali ya Rais Samia imeruhusu maandamano ya CHADEMA?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)


Umefanya observation nzuri sana.
 
Haya maandamano yamejikita kwenye sheria za uchaguzi tu, suala la katiba limefukiwa.

..uchaguzi wa 2024 na 2025 ndio sababu ya wadau kuelekeza nguvu zaidi ktk Tume Huru.

..Naamini uchaguzi ukishafanyika madai ya katiba mpya yatakuwa kipaumbele namba 1 cha wadau wa demokrasia.
 
..uchaguzi wa 2024 na 2025 ndio sababu ya wadau kuelekeza nguvu zaidi ktk Tume Huru.

..Naamini uchaguzi ukishafanyika madai ya katiba mpya yatakuwa kipaumbele namba 1 cha wadau wa demokrasia.
Mmeingia kwenye mtego wa Ccm, maana mpaka hapo wamezika ajenga ya katiba kwa sasa.
 
Mmeingia kwenye mtego wa Ccm, maana mpaka hapo wamezika ajenga ya katiba kwa sasa.

..Ccm hawana tatizo na " katiba mpya. "

..isipokuwa kuna mambo hawayataki kabisa.

..moja wapo ni TUME HURU ya uchaguzi.

..sasa anayedai tume huru hawezi kuwa amenasa ktk mtego wa Ccm.

..wewe waambie Ccm tuandike katiba mpya lakini tume ibakie kama ilivyo sasa hivi uone kama watakupinga.

Cc Tindo
 
Katiba ndiyo sheria mama....hilo la time huru ni sehemu tu ndani ya katiba.

Kukumbatia tume huru na kuitosa agenda ya katiba mmeonyesha mna tamaa za kurudi tena bungeni tu sio kutatua mzizi wa tatizo yaani katiba mbovu
 
Katiba ndiyo sheria mama....hilo la time huru ni sehemu tu ndani ya katiba.

Kukumbatia tume huru na kuitosa agenda ya katiba mmeonyesha mna tamaa za kurudi tena bungeni tu sio kutatua mzizi wa tatizo yaani katiba mbovu

..Ndio na hapana.

..ukiwa practical na realistic utaona mantiki ya kudai Tume Huru ya uchaguzi sasa hivi.

..Na ili Tume iwe huru ni lazima ufanye mabadiliko madogo ya katiba ya sasa hivi.

..Naamini mazingira ya kudai Katiba Mpya tukiwa tayari na tume huru yana afadhali kuliko ilivyo sasa hivi.

..kuna mambo mengi ya kuzingatia na yanaathari ktk harakati za kudai Katiba Mpya na moja wapo ni chaguzi mbalimbali.

..Binafsi naamini mapambano ya kudai Tume Huru ni sehemu ya mapambano ya Katiba Mpya.
 

1. Hakuna chama kitakachoingia madarakani kisiipende katiba ya sasa, CHADEMA siyo malaika!. Ndiyo maana ni muhimu kuvipush vyama vyote kuwa ili kama vinataka vopate support yetu viweke mbele ajenda ya katiba mpya kwanza!

2. Ukiwapa wanasiasa reforms za kuwarahisihia kupata ubunge wao, udiwani wao na uraisi wao kamwe hawatakuwa na Interest kubwa ya kupush katiba mpya, kelele za katiba ziliintensify baada ya Magufuli kuwafanya kitu kibaya kwenye uchaguzi wa 2020

3. Mabadiliko madogo ya katiba ya sasa hayawezi kutupatia uchaguzi huru tunaohitaji maana mfumo wa uchaguzi ni machinery mtambuka, inahusu tume yenyewe, Jeshi la polisi, mahakama n.k Bila kufanya reforms ktk hayo basi uchaguzi utaendelea bado kuwa manipulated japo athari inaweza kuwa imepunguzwa kidogo

4. Kama tunakubaliana na hoja kuwa tufanye reform ndogo za katiba ya sasa basi tuwaombe radhi CCM maana huo ndiyo msimamo wao toka zamani kuwa wako tayari kufanya reform ndogondogo za katiba ya sasa kwenye mambo ya uchaguzi lakini katiba mpya siyo wakati wake. TUliwakatalia wakati huo, sijui kwa nini tunataka kuwakubalia sasa!

5. Itakuwa ni ajabu hoja za ACT wazalendo za "TUME HURU KUELEKEA KATIBA MPYA" tulizokuwa tunaziponda humu kuwa zimekaa kiuchaguzichaguzi, leo eti ndo tunaona ndiyo busara na realistic way ya kwenda.
 
Mkuu, Usisahau kuwa the underlying point ni kwamba polisi ndio husabibisha, huanza na hufanya fujo!
 
🔊🆒
 
🔊🆒
 
👍👌👏🙏🔊🆒
 

..Cdm walikuwa sahihi kudai Katiba Mpya ambayo ndani yake kuna tume huru wakati ambapo muda ulikuwa unaruhusu kuipata kabla ya 2025.

..Sasa hivi tumechelewa. uchaguzi uko karibu mno, hivyo kinachowezekana ni mabadiliko madogo yatakayowezesha kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
 

Tunaweza kukubali kutokukubaliana.

Ila Hakuwezi kuwa na Tume huru ya Uchaguzi kwa kufanya mabadiliko madogo madogo katika katiba ya sasa. Itapaswa kugusa hata madaraka ya rais ktk mambo fulanifulani na hayo siyo mabadiliko madogo!. The only way ya kupata tume huru ni Katiba mpya na si ktk katiba ya sasa!

CCM iliyoplay delay tactic kuwadanganya akina Mbowe hadi kuwafikisha hapa leo hawadai katiba mpya bali wanadai mabadiliko madogomadogo ndiyo CCM hiyohiyo ambayo haitokupa mabadiliko yoyote ya kukusaidia ktk uchaguzi wa 2025.

Msimamo sahihi wa CHADEMA ni ule wa mwanzo kuwa NO KATIBA MPYaa no KUSHIRIKI CHAGUZI. Ni msimamo mgumu, una cost yake lakini ndiyo msimamo wa kukijengea chama heshima mbele ya umma na matunda kitayaona mbele.

Uchaguzi wa 2025 wala siyo critical kuisaidia Chadema kushika dola, ila utasaidia tu kuwapunguzia njaa makada wake wakuu wanaotamani kurudi mjengoni wwkale pesa rahisi
 

..suala sio Chadema kushika dola.

..jambo la muhimu ni tupate TUME HURU kabla ya uchaguzi wa 2025.

..pia uchaguzi wa Serikali za Mitaa usisimamiwe na Tamisemi.

..
 
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri kwa hao kina Thomaso wa Lumumba
 
Maandamano ya jana inaonekana yamekuumiza sana hisia zako. Pole sana kada mtiifu
 
Mkuu hamkuchelewa ila mlicheleweshwa kwa makusudi na Ccm na kwa hilo wamefanikiwa.


Uchaguzi kufanyika kwa katiba hii hii ndicho Ccm walichokilenga, hata ule mpango wa kutoa elimu ya uraia kwa miaka 3 kabla ya mchakato wa katiba ni moja ya mbinu za Ccm kupoteza muda ili waendelee kunufaika kwa katiba ya sasa.

Kwa katiba hii hiyo 'tume ya uchaguzi ' haitokuwa na Uhuru mnaoutaka yaani kwa katiba inayoruhusu aina ya demokrasia ya chama kimoja tu haiwezi kuruhusu Tume huru yenye kuleta uwiano sawa baina ya vyama tofauti shindani, kiufupi Ccm wamefanikiwa kuwazidi kete na mmeingia kwenye mtego wao kwa kulazimishwa.

Hata baada ya uchaguzi (maana Ccm watashinda tu), hiyo katiba mpya hamtoipata hata au la mtapata aina ya katiba wanayoitaka Ccm.

Nguruvi3 Rabbon zitto junior
 

CCM wamewastudy vizuri wakagundua kuwa jamaa zetu wanapozungumza kuwa wanataka katiba mpya kimsingi wanataka mazingira mazuri ya kupata viti vingi vya ubunge na ruzuku kuongezeka. Hawana Interest sana na major reforms ambazo wananchi wanazidai. Ndiyo maana CCM imewacorner na kuwafikisha point ambayo imeweza kumask sura zao, na sura zenyewe ni "Tufanye mabadiliko madogo ya kutuwezesha kutupeleka katika uchaguzi wa 2025" . Chama ambacho kiko tayari kusettle kwa mabadiliko madogo ya katiba ya sasa kwa ajili tu ya uchaguzi hakina strength ya kupigania katiba mpya kwa moyo mmoja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…