Kwanini serikali ya Tanzania iliachana na vita dhidi ya Umasikini?

Kwanini serikali ya Tanzania iliachana na vita dhidi ya Umasikini?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
China inasafiwa kwa kupiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi lakini inaisfiwa zaidi kwa hatua kubwa na za haraka za uchumi na maendeleo yaliyomaliza umasikini wa watu wake hadi kuwa china ya 1%.

Ni muhimu kujua unaweza kuwa taifa lenye uchumi ukubwa mkubwa na umasikini mkubwa sana kama vile Nigeria, Pakistan, Misri na Ethiopia.

Serikali yake ya Tanzania ina mpango gani wa kumaliza umasikini wa watu wake ambao kwa sasa makadirio ni kati ya 41% na 43% ya raia wake wanaishi katika umasikini uliokithiri/ uliotopea

Kwa kila mwaka mmoja serikali ya Tanzania ina mpango wa kupunguza kiwango cha umasikini wa raia kwa asilimia ngapi?
 
Sahivi iko buzzy na vita dhidi ya USHOGA, Umaskini sio shida zao kabisa.
 
Wanasiasa wetu wana vested interest kwenye umasikini wa wananchi, lakini pia hakuna uendelevu wa sera, kila Rais anakuja na lake.
 
Kuna watu wanazo mbinu na mikakati ya kumaliza umasikini wa watu, wapewe nafasi, walioshindwa wakae pembeni.
Itakuwa umasikini una nguvu sana umeitia nchi kabali ya mbao na kila ikijitahidi kuinuka inapigwa tanganyika jeki...😂
 
Kwa viongozi gani wa Tanzania na CCM yupo kupambana juu ya hali ya watu wa chini,watu hawana ajira ya kudumu na wenye ajira wanalipwa mshahara usiotosheleza.

Viongozi wapo kwa ajiri ya matumbo yao na vizazi vyao tu.

Huko china wanasheria madhubuti juu ya viongozi wala rushwa na wahujumu uchumi ila sisi ndio kwanza sheria zinawakumbatia.
 
Sahivi iko buzzy na vita dhidi ya USHOGA, Umaskini sio shida zao kabisa.
Sio kweli mkuu. Kwa sasa Serikali ya Tanzania inatumia mbinu za kimkakati kupitia mifumo ya Sera na Mipango ya Maendeleo kama ifuatavyo:
  • Kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa (Vision 2050) na Mipango ya Miaka Mitano (FYDP): Lengo kuu la Dira mpya ya 2050 ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa juu na kutokomeza kabisa umasikini uliokithiri (zero extreme poverty).
  • Na kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF / PSSN): Mfumo huu unatoa ruzuku za fedha moja kwa moja kwa kaya masikini sana pamoja na fursa za ajira za muda mfupi kwenye miradi ya kijamii na mtaji wa kuanzisha miradi midogo ya kiuchumi.
 
Duuh kumbe.
 
Kama unae kiongozi anayedhani chadema ni tatizo kwa nchi na katiba imeruhusu vyama vingi unadhani agenda ya kitaifa utaipata hapo zaidi ya ujinga tuu!!?
 
Back
Top Bottom