Kwanini Seychelles wanavua samaki katika maeneo yetu?

Kwanini Seychelles wanavua samaki katika maeneo yetu?

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Global Fishing Watch shared workspace

Kutokea hio webusite ni live na inaonyesha meli au vyombo vya uvuvi vinavyovua,inaonyesha jama wanapenya mpaka karibu ya Mtwara na lindi na kukaribia visiwa vya Zanzibar kwa umbali wa kilomita kama 120. Je, walinzi wetu wanaweza kufika umbali huo kulinda Tanzania Exclusive Economic Zone.

1611816538117.png
 
Waache wavue tu. Sisi tumewekeza kwenye siasa za kuwanunua wapinzani na pia kuiba kura.

Siku akili zikitukaa sawa, na sisi tutanunua meli za kisasa za uvuvi na zinazoweza kuingia kwenye kina chochote kile cha bahari.
 
Hivi international waters ni Km ngapi kutokea kwny fukwe zetu?
Funguwa hiyo webu ipo rula kwa kushoto unaweza kupima na eneo limeandikwa kuwa hili ni la Tanzania hata kule kwenye ugonvi Kenya na Somalia lile eneo limeandikwa hivyohivyo kuwa hapa kuna mbinde.

Sasa helikopta zetu za jeshi na vyombo vya baharia wanaweza kupunguza kurandaranda wakiangali hapo wanaweza kufuata na kuzichukua hizo meli,nakumbuka wale samaki wa magufuli ile itakuwa meli iliisha mafuta na karibu ni Tanzania ndio wakajiingiza.
 
Tatizo ni uzembe wetu sisi tumekalia kutoa leseni za uvuvi lakini hatuna sehemu ya kuhifadhi samaki kwa hiyo meli zote zinazovua zinaenda kuhifadhi samaki ama mombasa Kenya au Seychelles. Tumeweza kujenga jengo la kuhifadhi magari lakini tumeshindwa kujenga cold room ya kuhifadhi samaki.
 
Ina shangaza Zanzibar wana angiza samaki asilimia kubwa nje pamoja na Kuku ndio karibia 90% wanaagiza kutoka Brazil.
 
Walinzi wako buzy kulinda wapinzani. Samaki acha wavue kwani bahari ni yetu pekeyetu? Kumbuka hata samaki baharini humigrate tokana na hali ya hewa
Mbowe, Tundu na Mnyika ndio wanalindwa? Au unamaanisha nini🤔🤔
 
Kuna Uzi niliuona huku ukiuliza kwanini kipindi hiki cha Hussein vyombo vya usalama vipo karibu sana na ikulu ya Zanzibar?
Tumwache afanye kazi
Zanzibar watu wapo hoi asije wa malizia sijuwi walikwama wapi kile kisiwa bara bara zote mbovu
 
Waache wavue tu. Sisi tumewekeza kwenye siasa za kuwanunua wapinzani na pia kuiba kura.

Siku akili zikitukaa sawa, na sisi tutanunua meli za kisasa za uvuvi na zinazoweza kuingia kwenye kina chochote kile cha bahari.
zikinunuliwa,ghafla zinageuka si kipaumbele.
 
Tatizo ni uzembe wetu sisi tumekalia kutoa leseni za uvuvi lakini hatuna sehemu ya kuhifadhi samaki kwa hiyo meli zote zinazovua zinaenda kuhifadhi samaki ama mombasa Kenya au Seychelles. Tumeweza kujenga jengo la kuhifadhi magari lakini tumeshindwa kujenga cold room ya kuhifadhi samaki.
Usiogope, tutaanza huo ujenz pale chato
 
Back
Top Bottom