Kwanini Sheria ya uvaaji nembo ya mdhamini ivunjwe?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Tunaposema mpira wa Tanzania umejaa siasa ni kwa mambo kama haya. TFF na NBC Ltd wameingia mkataba wa NBC kuidhamini ligi kuu Tanzania na moja ya nasharti ni vilabu vyote lazima vivae nembo ya mdhamini kama ilivyo bila masharti yoyote kanuni na 16(1:1) yahusika.

Leo katika mechi ya Yanga na Azam tumeshuhudia timu ya Yanga ikivaa jezi zenye nembo yenye rangi tofauti na nembo ya mdhamini kinyume na kanuni na 16(1:1) ya mkataba wa TFF na NBC ltd.

Je, kwanini yanga hawaheshimu mkataba wa TFF na NBC Ltd?

Kwanini TFF na NBC Ltd wairuhusu yanga tu kuvaa nembo tofauti na nembo ya mfadhili?

Je, vilabu vingine navyo vikitoa masharti tofauti na mkataba itakuwaje?

TFF acheni siasa kwenye mpira heshimuni sheria na kanuni zilizopo kisheria.

 
Ukisikia siasa ni wewe sasa. Kwani kwako wewe ungeiona ile nembo waliyovaa Yanga leo sehemu nyingine labda say kwenye TV au kwenye gazeti vile vile Black and white ungeijua ni NBC au usingejua?

Nadhani waTanzania tupunguze siasa na ujuaji! Iwapo mdhamini aliyetoa hela zake halalamiki wewe kapuku unaona uchungu ili iweje kwa mfano. Mambo mengine unaanchana nayo tu mkuu.

Na wala usiitaje TFF, hayo mambo ni dunia nzima huwa hivyo. Hujawahi sikia makampuni makubwa yamebadili rangi ya nembo zao walipowadhani baadhi ya timu kubwa za nje ku suit itikadi za hizo timu? Unahisi simba wanaweza kuvaa nembo au kitu chochote cha njano na kijani?

Ikiwa wewe ni shabiki wa Simba (which is very likely) ungekaa chini tafakari mwenendo wa timu yako kwa sasa na achana na hizi ishu ndogo ambazo hazina kichwa wala Tija kwa timu yako.

Ushauri tu lakini, ni hiyari yako kupokea au kuacha
 
Mambumbumbu njoeni mjadili nembo baada ya kuona pira la hatari lililochezwa leo na timu ya wananchi
 
Mambumbumbu Makolo fc Mmekosa cha kukosoa sasa mmehamia kwenye nembo
Yani majina yako hata hayakeri wala kuchekesha.

Manara hajawahi kutoa jina lolote la utani kwa vidimbwi na lika trend HALIPO

Aliyetoa majina kama Utopolo, kidimbwi, vyura, gongo wazi n.k si YEYE 😝😝
 
Makolo mnatafuta pakusemea baada ya kuona mwaka huu hamna pakutokea.
 
Mbona nembo ipo, au wewe una matatizo ya macho?
Hawa Ni watu wa hovyo tu,Yanga siyo Kama vitimu vyao vingine, Yanga ina utamaduni,ina tunu na ina miiko. Utamaduni wa Yanga lazima uheshimiwe. Inapoitwa timu ya wananchi si bure ,kuna maana yake. Nashangaa kuna mtu namuheshimu Sana na yeye amejiingiza kwenye upumbavu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…