Nikifikiria unakuja na uchambuzi makini wa namna gani huyo mgombea wako atatatua hizo changamoto.
Lakini unatujia na kingereza chepesi cha "he is a solution".
Nilifikiri utatuambia nini atafanya kuondoa Rushwa, nini atafanya kuondoa urasimu, ukabila, ukanda na uzandiki ambao umegandamana katika soka la Tanzania!!!
Mimi nilifikiri ungetuambia hapa uzoefu wa huyu mgombea wako katika kushughulikia matatizo ya kimpira maeneo aliyopita. Mfano: ungetuambia, alifichua uozo wa rushwa baada ya kuingia madarakani huko mkuranga (mfano), au aliipandisha timu ya Kimbangulile fc daraja kutoka ligi daraja la nne mpaka ligi kuu alipokuwa mwenyekiti. Hivyo yani. Sasa wewe unatujia na bra bra zako za "he is a solution"
Jipange, pale siyo kolomije.
Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app