Kwanini Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hawapewi kibali cha kuajiri tangu 2019 leo 2023

Kwanini Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hawapewi kibali cha kuajiri tangu 2019 leo 2023

Serikali kuwatafuta kwa mitutu watoto ili waende shule alafu wakimaliza masomo biashara inaishia hapo na wahitimu kurudi mtaani kuanza kuzurura huku serikali hiyo hiyo ikikataa kuwapa ama kuweka mazingira ya wao kupata ajira ni sawa na kuwahujumu wazazi na familia za hawa wahitimu.

Kwa mzazi kuliko hili jambo kutokea anaona ni bora abaki na mwanae nyumbani kwake hiyo miaka 4-9 amfunde na kumfundisha mwanae maarifa huenda akasaidia familia baadae ama hata kuoa/kuolewa akawa na familia yake ya kawaida. Wazazi wanaumia sana na haya mambo ya eti watoto lazima wasome, ili litokee nini wakati hata wale waliohitimu juzi wamegeuka wazururaji na wadangaji

Kutoa ajira ni jukumu la serikali na wazazi na wanafunzi wanayo haki ya kuandamana kudai ajira maana serikali ndo baba na mama. Wananchi wanalipa kodi, mali za Taifa ziko mikononi mwa serikali kwa niaba ya wananchi, bado serikali inaajiri watu wasiozidi 20000 kwa mwaka wakati wahitaji ni zaidi ya 300000 kwa mwaka.

Ajira za binafsi ama makampuni binafsi hayawajibiki kwa mwananchi kama serikali yao hivyo kuwaambia wajiajiri ama waajiriwe na makampuni ni njia ya serikali kuukimbia ukweli, pesa nyingi zinaishia khchezewa na watu kula bata maofisini kwa kununua magari ya mamilioni badala ya kuongeza ajira serikalini.

Huu nao ni unyonyaji kwa wananchi wa Taifa hili
Duniani Kote Serikali Sio chanzo Rasmi cha Akira,Serikali inaajiri watu wachache Tu,Lakini Sisi wabongo macho yote Kwa serikali sababu mnapenda ule mteremko na wizi na maadili,JIAJIRINI anzeni kidogo kidogo na mtapanda kwa kadri ya juhudi,Tuacheni Ubishooo na malalamiko kila Dakika,
 
Kaingia mwanamke pale, tunamuombea afanikishe hili la ajira
 
Duniani Kote Serikali Sio chanzo Rasmi cha Akira,Serikali inaajiri watu wachache Tu,Lakini Sisi wabongo macho yote Kwa serikali sababu mnapenda ule mteremko na wizi na maadili,JIAJIRINI anzeni kidogo kidogo na mtapanda kwa kadri ya juhudi,Tuacheni Ubishooo na malalamiko kila Dakika,
Mkuu hapa umeandika kama Mwijaku
 
😁😁 usikute huyo jamaa kabla hajaajiriwa au hajajipata alikua mlalamikaji ,kalamba asali kawa motivational speaker anataka vijana wajiaji
Bahati Mbaya Hapana,Ila Nailaumu Sana Serikali Kwa kuamfanya kitu kama Job Security ndomana wengi mnapenda huko,wangeweka ajira za mkataba Serikalini Sidhani kama wengi wetu macho twengeyapeleka huko zaidi
 
Kwenye hilo nakupa 5
 
wametangaza ajira 2 Jana mambo ya plumbing and pipe fittings,
ila Kuna shida kwenye kuapply unaweza jaza Kila kitu sawa according to sifa walizotaja ila ukiapply wanakwambia huna sifa
 
Pia inawezekana walikua wanapewa sana vibali vya kuhamia kujaza ikama zilizopo. Tukumbuke vibali hutoka kwa kuzingatia wage bill ya serikali.​
 
Back
Top Bottom