Kwanini shule binafsi (private) zimeathirika katika matokeo?

Kwanini shule binafsi (private) zimeathirika katika matokeo?

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Sababu kubwa zinazohisiwa na watu kwa matokeo mabaya ya form four mwaka huu ni mgogoro kati ya serikali na walimu na ubovu wa shule za yeboyebo.

Hata hivyo nadhani inabidi tujadili zaidi ya hapo. Ingawa matokeo katika shule za private sio mabaya kama shule za serikali (kwa wastani), bado tumeshuhudia anguko la ghafla katika shule kongwe za private, ambazo miaka ya nyuma zilikuwa zinafanya vizuri zaidi. Shule hizi zina majengo na vifaa, na walimu wake hawana mgogoro na serikali

Nini tatizo?

Chini hapa ni jedwali la matokeo kwa shule 9 za private kwa miaka mitatu ya nyuma na mwaka huu (kwa bahati mbaya ya mwaka 2010 sikuyapata online). Shule nilizofanyia analysis ni Forest, Shauritanga, Kibosho girls, Don Bosco Seminary, Kiraeni, Usseri, Namfua, Lutheran Junior Seminar na Olaleni.

Jumla ya watahiniwa waliohusika katika analysis hii ni 3947 kwa shule zote kwa miaka 4.

attachment.php


cc kiwatengu, gakato, shabani asigwa Lyceum mfalmee ChiefmTz Prishaz GOOGLE Salary Slip Ndachuwa Kitaeleweka LESIRIAMU FUSO Kongosho FJM Uwezo Tunao kichwabaya Mwanafunzimg Lorah Tetty Kamundu PATRICE akenajo omujubi kelao kinanape Bramo acheche Nguruvi3 Kiby Young Tanzanian kaburu mdogo Lunyungu MASHANJARA gakato Kitila Mkumbo Mzee Mwanakijiji, Invisible Novel Idea

Na wanaJF wengine wote
 

Attachments

  • matokeo.png
    matokeo.png
    3.3 KB · Views: 1,347
Wenye kutaka mikamati uchwara juu ya kufeli kwa ndugu zetu, karibuni hapa na mkajitazamie huo muhtasari hapo juu; siongezi neno wala kupunguza kitu hapo.
 
..........bado tumeshuhudia anguko la ghafla katika shule kongwe za private, ambazo miaka ya nyuma zilikuwa zinafanya vizuri zaidi. Shule hizi zina majengo na vifaa, na walimu wake hawana mgogoro na serikali Nini tatizo?......
Mkuu nafikiri kuna kitu kinaanza kuchomoza ambacho kilikua kinafukuta chini kwa chini katika mfumo wetu wa elimu.

Kwanza ni kweli kuwa elimu ya Tanzania haiendani na mazingira na wakati au kizazi tulichopo..Shule na elimu kwa sasa ni mzigo,Vijana wengi wa kizazi hiki hawana morali na shule kama zamani na wanasoma bora liende na ukichunguza kwa jicho la tatu utaona kuwa "EDUCATION SYSTEM IS OUTDATED"....

Suala la pili nafikiri ni kutokua na mitaala inayoeleweka pamoja na nini watoto wafanye, Kumekuwa na mrundikano wa mambo ambayo mwanafunzi anasoma na mengi hayatoki katika mitihani, watahiniwa wengi hutumia past papers kama refference ya kufahamu nini cha kusoma na nini cha kuacha, Kuna tetesi nazisikia huku mitani na ni za muda mrefu kuwa hao wanaofaulu katika shule binafsi wengi wakuu wa shule zao wanafahamu japo kwa wizi wizi ni nini cha kufundisha mwaka huu na ni nini cha kuacha kwa kuwa wana watu kwenye "system", japo ni tetesi siwzi kuzithibitisha....
 
Mzee Tuko!
Ni kweli kuna mengi sana ya kuyaongea hapa, moja ni kweli kuwa matokeo yamekuwa mabaya sana toka 2010, na sababu ni so obvious kwamba ndio mwaka ambao SHULE ZA KATA zilianza kutoa MAZAO, mabao wengi wetu tumekubaliana kuwa ni JANGA LA KITAIFA kwani hawa wanasoma kitu ambacho ningependa kukiita 'GLORIFIED PRIMARY SCHOOLS' hakuna qualitative differences na SHULE ZA MSINGI kiukweli, zaidi ya majengo na uniform na labda idadi ya wanafunzi. Hili moja

Pili nafikiri tatizo kubwa lililofanya hata shule nyingine kongwe zisifanye vizuri mwaka huu sasa ni hili la KUBADILISHWA MTAALA kutoka CONTENT BASED ASSESSMENT kwenda COMPETENT BASED ASSESSMENT. Hapa wakulaumiwa ni SERIKALI. Nafikiri walimu wengi katika shule nyingi bado hawajaandaliwa vizuri katika mfumo huu wa kumtaini mwanafunzi, ingawa NECTA wao wanafuata mfumo huo bila kujua to what extent watainiwa wanajua hayo? Nimepata kushuhudia walimu wakifundisha na sikuona tofauti kabisa kati ya mfumo wa sasa na wa mwanzo. Kwahiyo nadhani wanafunzi wengi bado hawaandaliwi sawa na MATAKWA YA NECTA, tatizo ni hili sasa la MASS FAILURE hata kwenye shule kongwe.

NB. HATA HIZI SHULE ZINAZOFAULISHA SANA KUNA FAIDA NYINGI SANA ZINAWAFANYA WAFAULU ZAIDI, MOJA YA MSINGI KULIKO ZOTE NI class. SHULE HIZI NDIZO WATOTO WOTE WA WAKUBWA WA SERIKALI, MATAJIRI, INFLUENTIAL MIDDLE CLASS, NA CLERGYMEN WANASOMA. hapa comparatively kuna kitu kinawapa FAIDA hawa ambayo ni so indirect LAKINI ina maana saana katika KUATHIRI MATOKEO YAO, ndio maana wao kufeli ni DIVISION THREE. Kinachofurahisha hawa hawa waliopata hizo div. one ukikutana nao vyuoni ni WATUPU KABISA WA KUTUPA.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom