Kwanini Simba haipandishi mashambulizi

Kwanini Simba haipandishi mashambulizi

Edson Carrington

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2022
Posts
216
Reaction score
636
Habari wakuu,

Shida ni nini pale Simba, kwanini hatupandishi mashambulizi na tukipata mpira tunacheza sana pasi za nyuma.

Kipindi cha pili ilibidi mpaka Che Fondoh Marlone awe anapandisha mashambulizi mwenyewe maana kiungo ilikuwa ovyo kabisa kwenye kufanya mashambulizi.
Wings nazo zilishindwa kabisa kufanya attacking.

Ni mara chache sana Simba walienda kumshambulia mpinzani.

Benchi la ufundi liangalie suala hili kwa umakini zaidi haswa kuelekea mechi za klabu bingwa Africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inferiority complex dhidi ya waarabu ndicho kinachotutesa Wana Simba tunapitia kipindi kugumu sana
 
Simba sasa hivi wanapata ugumuj sana kupandisha mashambulizi kwa sababu wanacheza taratibu sana. Hata wakati mwingine unakuta wachezaji wa timu pinzani wamekuja karibia wote kushambulia halafu wachezaji wa Simba wakapoka mpira lakini bado watataka wapige "square pass" kwenye eneo lao badala ya kufanya "counter attack" ili hali sasa hivi wana wachezaji kibao wenye kasi. Na hii sio kwa mechi ya jana tu bali hata kwenye ligi ndio maan utakuta mechi karibia zote wananza wao kufungwa halafu ndio wanazinduka. Ni kazi ya benchi la ufundi kerekebisha hii kasoro ili timu icheze "counter attack" kwa kasi kwenda lango la adui pale timu inapopoka mpira na adui hajajipanga vizuri. Na benchi la ufundi lisione shida kujifunza namna Al Ahly walivyokuwa wanapiga "counter attack" za kiwango cha kimataifa.
 
MTASEMA KILA NENO LAKINI HAPA NILIMALIZA YOTE.

Sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom