Kwanini simba hawakumsajili Awesu Awesu ?

Kwanini simba hawakumsajili Awesu Awesu ?

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Miaka miwili nyuma kwenye mechi za preseason au kwenye kombe la fa sina uhakika simba walienda Arusha kucheza na klabu ya madini fc ya Arusha inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Kwenye mechi ile mchezaji wa madini fc Awesu awesu alicheza mpira wa hali ya juu kiwango cha kutisha alionyesha mpaka viongozi wa simba waliokuwepo pale walikunwa vichwa na mpira ulivyokwisha viongozi wa simba walimfuata na kuongea nae na Hans pope alisema tayari walishaongea nae na kuchukua namba yake ya simu na msimu ujao ambao ni huu kama sijakosea ndio wangemsajili ila nadhani walimsahau.

d288365afbb04461cac1edc8549f2222.jpg

Bwana mdogo kumbe kasajiliwa mwadui na leo amecheza vizuri mno dhidi ya simba sc...kiukweli jamaa anaujua sana
 
Namjua Huyu Jamaa Akiwa pale Madini Fc Aliwatesa sana Viungo wa Simba

Pamoja na Yule Goli kipa wa Madini
 
kwa wakati ule simba ingemsajili ilikuwa ni kucheza kamari na hata huyu Awesu angeweza kupotelea benchi kwani kwa timu kama simba ingewezekana asipate nafasi ya kutosha kucheza . wapo wachezaji wengi wa madaraja ya chini na hata timu ndogo za ligi kuu ni mafundi kweli kweli lakini wapeleke simba au yanga utashangaa na wengine wakiachwa na hizi timu kubwa ndio nitolee kabisa. nafikiri kwa sasa baada ya kujenga jina na kuonyesha uwezo wake ndio wakati muafaka wa kwenda simba au yanga.
 
Yupo MWADUI na kesha kutana na akina nonga walioenda timu zinazojilazimisha kuitwa kubwa yakawakuta na wamemjaza sumu dogo kagoma haondiki
 
Back
Top Bottom