Kwanini Simba SC Imepoteza Mvuto?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kama kipindi ambacho Simba haizungumzwi kwenye midomo ya watu na vuombo vya habari basi ni katika kipindi hiki haswa zaidi katika mwaka huu.

Zipi sababu zimepelekea Yanga SC kuwazidi Simba SC kwa mbali zaidi kwenye "media and social attention"?

Kuna habari ambazo sasa zinatolewa na klabu yao lakini zinaonekana hazina mvuto kushinda zile za mahasimu wao wa upande wa pili? Yaani habari inaweza isitrend zaidi ya masaa 4 lakini zile za upande wa pili zina trend siku nzima na siku ya pili raia wana amka nazo.

Kwanini habari za Yanga zinauza zaidi kuliko za upande wa pili?

Hivi leo mchana wameitisha press conference kuhusu udhamini wao mpya wa timu ya vijana, lakini cha ajabu hakuna vyombo vya habari vilivyo jitokeza zaidi ya media house 3 ambazo pia ni za youtube tu. Ayoma TV, Ayo TV na Mpenja TV.

Je pengo la Barbara linajidhihirisha wakati huu? Je viongozi wao waliopo wanashindwa kufanya kazi kwa mikakati kama wenzao wa Yanga SC?

Wafanye nini ili wafikie levels za Yanga SC?

 
Wamrudishe Manara tu

Mana jamaa alikuwa anajua kuinogesha simba.

Na akianza kuinanga YANGA kiutani yaan mpaka Mwanayanga mwenyewe unapoga SONYO la kukubari
Zirudi zama zile manara VS j muro
 
Kwa hiyo wewe ulitaka uone mic 20 zimejazana hapo ndiyo ungefurahi? Hiyo habari siyo kubwa ndiyo maana hauoni simba wameisukuma sana. Kama ni udhamini wa U20 press zake zimeshafanyika zaidi ya 2 na hiyo ya leo hata kwenye platform za Simba hawajairipoti.

Hivi kweli umeuliza "wafanye nini ili wafikie levels za Yanga SC?"
 
Sio tu habari hiyo.

Habari zao zote kwa ujumla yaani zimeonekana kupwaya kwenyw macho na masikio ya wakulungwa.
 
Sio tu habari hiyo.

Habari zao zote kwa ujumla yaani zimeonekana kupwaya kwenyw macho na masikio ya wakulungwa.
Labda ni kwa sababu hazikufurahishi ukizingatia wewe si mshabiki wa Simba.

Hizo habari lengo lake ni kuwafikia mashabiki wa Simba na mpira kwa ujumla na lengo hilo linaweza kufikiwa bila habari kutrend. Siyo kila habari inayotrend ni njema kwa timu. Habari za Yanga zilizotrend hivi karibuni ni za Feisal na Nabi, na tunajua hamkuwa na furaha nazo.
 
Nenda page ya Simba instagram...imegonga 5million followers...club yenu ina ongelewa kwa kuwa ilikua inadanganya uma...kumbe wachezaji wa kikongo walikuwepo kwa mkopo...
 
1. Ukienda social Media Simba inaongoza kuwa na MASHABIKI wengi.

2. Maidhirio ya Viwanjani Simba inaongoza.

3. Lete MICHANGO ushindanishe Simba na yanga. Bado Simba yupo mbali sana anaongoza.

USIFANANISHE SIMBA NA KITU CHOCHOTE.
 
Yanga Wana timu ya marketing chini Jackson group ya kelvin twissa.

Haya mambo huwa hayaendj hivi hivi.
Lazima ujipange.
 
Mwenyekiti simuelewi hata kidogo.
 
1. Ukienda social Media Simba inaongoza kuwa na MASHABIKI wengi.

2. Maidhirio ya Viwanjani Simba inaongoza.

3. Lete MICHANGO ushindanishe Simba na yanga. Bado Simba yupo mbali sana anaongoza.

USIFANANISHE SIMBA NA KITU CHOCHOTE.
"Maidhirio" ya mwaka gani mliwazidi??
 
Yanga Wana timu ya marketing chini Jackson group ya kelvin twissa.

Haya mambo huwa hayaendj hivi hivi.
Lazima ujipange.
Aisee hili nalo ni jambo.

Inabidi nao Simba wajifunze kwqetu kwa sababu wamelala sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…