Leo Haji S. Manara amethibitisha hili lakini nimebaki najiuliza maswali kwa nini iwe hivyo?...
TOFAUTI KATI YA MFUMO WA YANGA NA SIMBA KATIKA UTARATIBU WA UWEKEZAJI.
Kuna tofauti ya mfumo wa uwekezaji wa Simba na ule wanao taka kuutumia Yanga. Pengine wale waliokuwa wanapinga utaratibu wa Simba yawezekana hawakupewa semina ili waelewe mfumo wa Simba, au walielewa lakini hawakuridhika.
Baadhi ya tofauti zilizopo katika uwekezaji wa Simba na Yanga ni hizi zifutazo.
i) Katika mfumo wa uwekezaji wa Simba, Mwekezaji anapewa timu hata kabla ya kununua hisa. Mfano Mo anaendesha shughuli za timu lakini hakuwahi kulipia hisa zake 49% ambazo ni tshs 20 bil kwa wenye timu yao ambao ni wanasimba na Mo ni mwekezaji pekee katika uwekezaji wa Simba.
Yanga baada ya kubadili Katiba, wataanzisha kampuni ,kampuni hiyo itakua ya Yanga kwa 100%, baada ya hapo watauza hisa 49% kwa wawekezaji 3 au wasio zidi 4, wawekezaji maximum watakua 4 na minimum watakua 3. Na mwekezaji atapewa cheti cha uwekezaji baada ya kulipia hisa zake (Hakuna mali kauli au mkopo)
2) Katika Simba,ili kupata thamani ya "Simba, tathmini, ilizingatia mali zote za klabu ya Simba yakiwemo majengo nk. ndio maana akina Mzee Kilomoni walikua wanalalamika, kwanini Mo apewe haki ya kumiliki majengo na viwanja vya Simba, wakati hajalipia hata hela ya hisa? Ndio maana uwanja wa Bunju ukaitwa Mo Arena. Ule uwanja ni wa SSC sio wa mwekezaji, mwekezaji ameukuta.
Katika kutafuta thamani ya klabu ya Yanga, tathmini inafanyika kwa kuangalia fan base, kuangalia nembo ya Yanga, yaani mtaji wa Yanga ni mashabiki, wapenzi na wanachama. Vitu kama majengo viwanja nk vinabakia mali ya Yanga FC ,havihusiki katika Kampuni.
3) Uwekezaji ndani ya Simba ,yule mwenye hisa ndogo ndiye mwenye mamlaka, yaani ndiye Mwenyekiti wa Bodi , lakini katika uwekezaji wa Yanga Mwenyekiti wa Bodi atatokana na yule mwenye hisa kubwa.
Hizo ni baadhi ya tofauti katika mifumo ya uwekezaji wa klabu hizo mbili.
NB; Yawezekana wanahabari walikua hawapingi Mo kuwekeza katika Simba,bali walikua hawana uelewa mfumo wa uwekezaji ndani ya Simba unavyo fanya kazi.Kwakua mchakato haukua shirikishi na hadi sasa bado wengi hawaelewi ,inakua vipi mtu anakua Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ambayo hana hisa? Hana hisa kwa maana hajalipia hisa kwa kuwalipa wenye timu tshs 20 bil.
Inakua vipi mqekezaji awe na haki kwenye assets za Simba kama majengo na viwanja wakati kwanza amevikuta pale,pili hajalipia hisa kwa wenye klabu yao!
Maswali yataendelea kuulizwa kwa pande zote zinazo fanya mabadiliko kwakua hii ni mifumo mipya na hizi klabu zinamilikiwa na wananchi.
Angalia Azam, hakuna maneno maneno kwakua klabu ni yao, haikubadilishwa kutoka kuwa ya wananchi na kuwa ya wawekezaji.