Kwanini Simba SC inachukiwa na waandishi /wachambuzi?

pamba boy

Senior Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
181
Reaction score
266
Leo Haji S. Manara amethibitisha hili lakini nimebaki najiuliza maswali kwa nini iwe hivyo?

Ni kweli mchakato wa mabadiliko wa simba ulikumbana na vikwazo vingi sana kutoka kwa wachambuzi na baada ya FCC kuleta hoja zake wachambuzi wakaishupalia sana! leo hii hakuna hata mmoja aliekosoa mchakato wa yanga bali ni kusifia!

Inawezekana hawa wachambuzi ndiyo kaburi la Yanga kwa sifia sifia yao kumbe wanapotoshwa.
 
Mchakato wa yanga umenyooka.. kila mwanachama ameshirikishwa.. na ndio maana unachukua muda mrefu...

Ila mchakato wa simba haueleweki ndio maana una utata..

Mfano Yanga bosi mkuu ni msolla na amepata nafasi kwa mchakato wa wazi.. simba bosi mkuu ni babra nafasi kaipata kwa utaratibu gani, haieleweki
 
Mchakato wa yanga umenyooka.. kila mwanachama ameshirikishwa.. na ndio maana unachukua muda mrefu..
inasikitisha sana ulivyo na akili finyu? unajua kwamba cheo cha CEO ndicho zamani kilikuwa kinaitwa katibu? kwani katibu wa yanga alichaguliwa na nani? unajua katibu(CEO) analipwa mshahara? hujui simba ina mwenyekiti anaitwa mangungu?

unaongelea mfumo hata hujui unachokiongea, nyie subirini kupokea mitambo ya magoli airport ligi ianze muanze kupoteana, mwezi wa 9 huko CAF muanze kuchezea vipigo muanze kulaumu TFf na karia
 
Leo Haji S. Manara amethibitisha hili lakini nimebaki najiuliza maswali kwa nini iwe hivyo?...
TOFAUTI KATI YA MFUMO WA YANGA NA SIMBA KATIKA UTARATIBU WA UWEKEZAJI.

Kuna tofauti ya mfumo wa uwekezaji wa Simba na ule wanao taka kuutumia Yanga. Pengine wale waliokuwa wanapinga utaratibu wa Simba yawezekana hawakupewa semina ili waelewe mfumo wa Simba, au walielewa lakini hawakuridhika.

Baadhi ya tofauti zilizopo katika uwekezaji wa Simba na Yanga ni hizi zifutazo.

i) Katika mfumo wa uwekezaji wa Simba, Mwekezaji anapewa timu hata kabla ya kununua hisa. Mfano Mo anaendesha shughuli za timu lakini hakuwahi kulipia hisa zake 49% ambazo ni tshs 20 bil kwa wenye timu yao ambao ni wanasimba na Mo ni mwekezaji pekee katika uwekezaji wa Simba.

Yanga baada ya kubadili Katiba, wataanzisha kampuni ,kampuni hiyo itakua ya Yanga kwa 100%, baada ya hapo watauza hisa 49% kwa wawekezaji 3 au wasio zidi 4, wawekezaji maximum watakua 4 na minimum watakua 3. Na mwekezaji atapewa cheti cha uwekezaji baada ya kulipia hisa zake (Hakuna mali kauli au mkopo)

2) Katika Simba,ili kupata thamani ya "Simba, tathmini, ilizingatia mali zote za klabu ya Simba yakiwemo majengo nk. ndio maana akina Mzee Kilomoni walikua wanalalamika, kwanini Mo apewe haki ya kumiliki majengo na viwanja vya Simba, wakati hajalipia hata hela ya hisa? Ndio maana uwanja wa Bunju ukaitwa Mo Arena. Ule uwanja ni wa SSC sio wa mwekezaji, mwekezaji ameukuta.

Katika kutafuta thamani ya klabu ya Yanga, tathmini inafanyika kwa kuangalia fan base, kuangalia nembo ya Yanga, yaani mtaji wa Yanga ni mashabiki, wapenzi na wanachama. Vitu kama majengo viwanja nk vinabakia mali ya Yanga FC ,havihusiki katika Kampuni.

3) Uwekezaji ndani ya Simba ,yule mwenye hisa ndogo ndiye mwenye mamlaka, yaani ndiye Mwenyekiti wa Bodi , lakini katika uwekezaji wa Yanga Mwenyekiti wa Bodi atatokana na yule mwenye hisa kubwa.

Hizo ni baadhi ya tofauti katika mifumo ya uwekezaji wa klabu hizo mbili.

NB; Yawezekana wanahabari walikua hawapingi Mo kuwekeza katika Simba,bali walikua hawana uelewa mfumo wa uwekezaji ndani ya Simba unavyo fanya kazi.Kwakua mchakato haukua shirikishi na hadi sasa bado wengi hawaelewi ,inakua vipi mtu anakua Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ambayo hana hisa? Hana hisa kwa maana hajalipia hisa kwa kuwalipa wenye timu tshs 20 bil.

Inakua vipi mqekezaji awe na haki kwenye assets za Simba kama majengo na viwanja wakati kwanza amevikuta pale,pili hajalipia hisa kwa wenye klabu yao!

Maswali yataendelea kuulizwa kwa pande zote zinazo fanya mabadiliko kwakua hii ni mifumo mipya na hizi klabu zinamilikiwa na wananchi.

Angalia Azam, hakuna maneno maneno kwakua klabu ni yao, haikubadilishwa kutoka kuwa ya wananchi na kuwa ya wawekezaji.
 
Mimi nilitamani tu kufahamu iwapo huyu msemaji wa simba kama anavuta bangi, au la! Siamini kama anafanya vile kwa sababu ya ulemavu wake wa ngozi!

Maana kwa akili ya kawaida, huwezi kuwakalipia waandishi wa habari kwa namna ile.
 
Hivi kila siku wanavyozunguka kuelezea maredioni huwa huskilizi?
Pitia hata youtube basi ujifunze kuhusu simba.
 
Mimi nilitamani tu kufahamu iwapo huyu msemaji wa simba kama anavuta bangi, au la! Siamini kama anafanya vile kwa sababu ya ulemavu wake wa ngozi!

Maana kwa akili ya kawaida, huwezi kuwakalipia waandishi wa habari kwa namna ile.
Kujibizana na Haji ni kama kucheza miereka na nguruwe kwenye matope, wakati wewe unachafuka yeye anafurahia
 
Utopolo mbona mnateseka na Simba?
 
Mimi nilitamani tu kufahamu iwapo huyu msemaji wa simba kama anavuta bangi, au la! Siamini kama anafanya vile kwa sababu ya ulemavu wake wa ngozi!

Maana kwa akili ya kawaida, huwezi kuwakalipia waandishi wa habari kwa namna ile.
Yule jamaa hana akili timamu! Anajiona yuko juu huyu faler!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mwana simba ila alichoongea Manara anastahili kuomba radhi
Na hii ni mara ya pili anaongea shit kwa vyombo vya habari na bado wanamfuatafuta tu ndio maana ana wabagaza anavyotaka. Mie pia ni Simba ila kauli zake baada ya mechi kuhairishwa na hii ya kumbwatukia mtangazaji wa clouds sio sawa kabisa.

Namuelewa Haji kwa kuhamashisha ila hana skills za kudeal na vyombo vya habari japo anajisifu ni mwanahabari pia.

Anakua na mihemko isiyo ya lazima na kama ana issue personal na baadhi ya waandishi basi afanye insta huko na sio kwy press za club ana haribu brand ya Simba tunaonekana wa hovyohovyo
 
Uliangalia habari za michezo za leo magazeti yote? Mi ilinishangaza sana ila baada ya haji kuongea nikaconnect dots! Hao waandishi sijui wachambuzi wanazingua sana, inakueje uchambuzi ufanane magazeti yote kwa siku moja? What a coincidence! Hiyo lazima ni conspiracy.
 
Hadi kesho labda ataomba radhi
 
Labda elezea ulikuaje, maana hata taaluma ya habari nayo sikuhizi inapwaya sana wengi wao ni spoon feeding. Japo haitoi uhalali kwa Haji kubwatuka namna ile he must be smart and professional
 
Mimi nilitamani tu kufahamu iwapo huyu msemaji wa simba kama anavuta bangi, au la! Siamini kama anafanya vile kwa sababu ya ulemavu wake wa ngozi!

Maana kwa akili ya kawaida, huwezi kuwakalipia waandishi wa habari kwa namna ile.
Waandishi wamemlea sana huyo jamaa kila siku anawatukana bado wananchekea
 
Nafasi ya barbra ni kama alivyo cenzo huko utopolo hyo nafasi ya msola yupo mangungu ambaye Kachaguliwa km alivyochaguliwa msola ukitaka kujua simba sc Barbra kapatikana vp kawaulize utopolo wenzio cenzo kapatikana vp
 
hukuona ile clip ya mzee mpili ofisini kwa enginer hersi hukusikia sauti ya privaldinho wa clouds fm akimuuliza maswali yule mzeee, wanaichukia simba sana hata kufungwa na kaizer chiefs walifurahi sana
kwa kweli huwanga hata wanatoaga maelekzo redioni wakijifanya wanachambua kwamba simba ukitaka kuizuia uwagonge gonge nafkiri uliona polisi na azam walivyocheza dhidi ya simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…