Kwanini simpendi mbunge huyu wa Bunge la Katiba?

mhalisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
1,181
Reaction score
322
Kwanini simpendi mbunge huyu wa Bunge la Katiba?

KWA kuwa wiki iliyopita niliahidi kuendelea na makala iliyochapishwa katika safu hii ya Dokezo la Wadau na kwa kuwa, siwezi kuendelea na makala hiyo kwa sababu maalumu na muhimu, niwaombe radhi wasomaji wa safu hii ya Dokezo la Wadau kwa usumbufu uliojitokeza.

Nawaomba radhi wasomaji wangu kwa kunukuu maneno ya mwanafalsafa Dk. Phili McGraw aliyewahi kusema; kuna wakati unaweza kufanya uamuzi sahihi na wakati mwingine kufanya uamuzi kuwa sahihi (Sometimes you make the right decision, sometimes you make the decision right).

Baada ya hapo, nitaendelea na mjadala wa leo kuhusu Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba ninayemchukia angalau kwa siku hizi za awali za vikao vya Bunge la Katiba, nikijenga matumaini huenda akajirekebisha hapo baadaye.

Lakini ili kujadili vizuri zaidi, nigusie kidogo kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobeli katika Fasihi, Ernest Miller Hemingway, ambaye nitarejea sehemu ya maelezo yake ‘kushindilia' mjadala wangu wa leo.

Kwa muhtasari tu ni kwamba, Hemingway ni mtu wa aina yake, ni mwandishi wa habari na mtunzi wa vitabu aliyewahi kuwa dereva wa gari la kubeba wagonjwa wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na alijiua Julai 2, mwaka 1961. Lakini kabla ya hapo (kujiua) alinusurika kifo katika ajali mbili za ndege.

Ni kati ya watu wachache duniani wanaotajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika karne ya 20, kwa kutazama maisha na matokeo ya kazi zake.

Alishinda Tuzo ya Nobeli katika fasihi mwaka 1954 na amewahi kuandika vitabu saba, ni raia wa Marekani lakini aliyepata kumudu kuishi maisha magumu katika nchi mbalimbali duniani, ikiwamo Cuba na hata barani Afrika.

Kuna mambo mawili ambayo Ernest alikuwa akiyaamini wakati wa uhai wake, ambayo nitayatumia kwenye mjadala wangu wa leo kuhusu mbunge ninayemchukia sana ndani ya kumbi za Bunge la Katiba.

Jambo la kwanza, aliamini; namna bora zaidi ya kujiridhisha kwamba unaweza kumwamini fulani basi kwanza ni sharti utangulize imani yako kwake, vinginevyo hutaweza kumwamini kamwe.

Lakini jambo la pili aliamini; watu wote duniani hatima yao inafanana, yaani kifo. Uwe daktari, mkulima, mwalimu, rais, waziri, mbunge au mfugaji kifo ni lazima, isipokuwa kinachoweza kutofautisha kati yako na wengine ambao nyote mmekufa au mtakufa ni taarifa kuhusu namna gani uliishi duniani na aina ya kifo chako (It is only the details of how he lived and how he died that distinguish one man from another.

Huyo ndiye Ernest miongoni mwa magwiji waliokuwa na ushawishi ndani ya karne ya 20 kutokana na kazi zao. Naam, awali nimeeleza kuhusu mbunge ninayemchukia ndani ya Bunge la Katiba.

Lakini kwa sababu Bunge hilo bado halijashika kasi sawa sawa, nitaeleza tu sifa za mbunge huyo ninayemchukia bila kumtaja jina, nikiamini kwa sasa sifa hizo pekee zitamweka katika hali ya kumtambua kwa kadiri ya matendo yake wakati wa mijadala ya Bunge.

Ni mbunge gani huyo?

Mbunge huyu anachukua posho kama wenzake wa Bunge la Katiba, ni nadhifu kwa mavazi (sitaki kutaja ni mwanamke au mwanamume).

Si mwepesi wala mzito kuzoeana naye, lakini sifa yake kubwa ni mbishi, na ni dhahiri haamini katika kile anachoamini Ernest Miller Hemingway kwamba, ingawa wabunge wote wa Bunge la Katiba watakufa, lakini kitakachowatofautisha mbele ya vizazi kadhaa vijavyo ni namna walivyotumia fursa ya kuwapo bungeni kuandika Katiba Mpya endelevu.

hii ni makala ambayo ameiandika mwandishi Godfrey Dilunga wa gazeti la Raia Mwema.

Kati ya matatizo makubwa ya mbunge huyu ni kwamba, ndani ya ubishi wake anapenda mno kung'ang'ania hoja za kundi lake ndizo zishinde hata kama hazina maslahi kwa taifa.

Kwake yeye kauli mbiu ni; msimamo wetu kwanza nchi baadaye, yaani msimamo wa kundi lake ni muhimu kuliko maslahi ya taifa yanayojitokeza kwenye hoja za wengine.

Taarifa nilizonazo ni kwamba mbunge huyo amejiandaa kubishana kuhusu muundo wa Muungano ambao utaligawa Bunge la Katiba katika pande kuu mbili; upande unaotaka muundo wa serikali mbili na upande unaotaka muundo wa serikali tatu.

Namchukia mbunge huyu kwa sababu hataki kusikiliza kabisa hoja za wenzake wanaotaka muundo ambao yeye na kundi lake hawautaki, na mnaweza kumbaini wakati wa mjadala atakuwa akizomea wengine wenye hoja tofauti.

Huyu yuko tayari kwa lolote. Yuko tayari kupewa rushwa na viongozi wa kundi lake ili kushawishi kwa kuwanunua wengine walioko kundi kinzani kwa lengo la kufanikisha malengo ya kundi lake hata kama hayana uhusiano na maslahi ya taifa.

Anatamani sana mabavu ya kipolisi na nguvu za dola yatumike kupitisha hoja anayoshabikia katika mvutano wa muundo wa serikali mbili au tatu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbunge huyu amekuwa na wasiwasi kwa kila mtu anayepinga au kukosoa anachokiamini yeye na kundi lake, wasiwasi ambao unaziba kabisa masikio yake kusikiliza utamu wa hoja kinzani kutoka kwa wenzake wanaotanguliza maslahi ya taifa wakati wa uwasilishaji wa hoja zao.

Mbunge huyu ni mtumwa wa mawazo ya kundi lake, utumwa ambao ni mbaya zaidi katika enzi hizi za uhuru wa mawazo na hasa mawazo ya ndani ya Bunge ambayo uhuru wake unalindwa kwa nguvu za kisheria. Fikra zake zimekwenda likizo na sasa kichwa chake kimesheheni fikra za kundi lake.

Kwa kweli nawashauri waangalizi wa usalama bungeni waongeze umakini kuhusu mbunge huyu, wampekue kwa uangalifu kila anapoingia ndani ya Bunge, ni mkorofi pale hoja anazozitaka yeye na kundi lake zinapopingwa.

Askari wahakikishe si tu haingii na silaha ya aina yoyote, bali hata kalamu yake (kama anayo) waichunguze, inawezekana imepachikwa sindano ndani yake ya kumchoma fulani ndani ya ukumbi wa Bunge.

Kwa kadiri Bunge la Katiba litakavyokuwa likiendelea na vikao vyake, mtamjua tu mbunge huyu hata kama kwa siku hizi za awali ameficha makucha yake. Ndiyo, mtamjua tu, si mrefu sana wala mfupi, anatokea upande mmojawapo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni kwamba ukipinga hoja ya kundi lake, basi kama ni rafiki yako, ujue urafiki umeingia doa, wewe ni adui si tu kwake bali kundi lake. Ni mbunge asiyetaka kuamini kwamba wengine wanauwezo wa kufikiri na kuibua hoja zinazotanguliza maslahi ya taifa. Ni mbunge limbukeni, amejiandaa vilivyo kuhakikisha hoja za kundi lake zinapita bila mabadiliko.

Ni mbunge asiyejua mantiki ya majadiliano, kwamba mwisho wa majadiliano ni kupitisha uamuzi kwa kuzingatia nguvu za hoja na si hoja za nguvu.

Namchukia sana mbunge huyu na kwa kweli hata Watanzania wengine, wakiwamo wabunge wenzake wataanza kumchukia siku za awali tu Bunge litakapokuwa limeanza kujadili rasimu ya Katiba Mpya itakayowasilishwa bungeni na Jaji Joseph Warioba.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Hata mm naamini ni yule yule sijui uli sindika anaitwa,he is really a bore!
 
Dah, yaani hapa nabaki kukodoa macho tu. Maana yeye anaogopa kumtaja, sisi tutamtaja vipi?? Uoga wa ajabu huu!!!
 
Mimi nahisi ni Ole Sendeka, jamani huyu baba yukoje ni maslahi gani anayopigania hayo? Maana ni kama mtu aliyetumwa kwa kazi maalumu. Ashindwe kabisa atuachie tupate katiba bora, anavuruga mambo tu.
 
nI yULE ALIYEKUWA NA KESI YA KUPIGANA WAKATI WA KAMPAINI ZA MWAKA 2015
 
Huyu jamaa, ole nadhani ameahidiwa uwaziri mkuu 2015 hivyo lazima ajiwekee mazingira bora yakiutawala kama sio ya kifalme.
 
Mimi nahisi ni Ole Sendeka, jamani huyu baba yukoje ni maslahi gani anayopigania hayo? Maana ni kama mtu aliyetumwa kwa kazi maalumu. Ashindwe kabisa atuachie tupate katiba bora, anavuruga mambo tu.

Siyo Ole Sendeka kwa sababu (1) Sendeka yuko kinyume na wale wanaotaka serikali mbili; (2) Ole sendeka hajaficha makucha yake sasa kwa vile amekuwa mchangiaji mzuri sana kwenye mchakato wa kupitisha kanuni.
Vipi kuhusu yule wa jimbo la Iramba ...? Vigezo vyote vinamkubali isipokuwa hakutajwa kama ni waziri kwa sababu kwa kufanya hivyo mhalisi angekuwa ametegua kitendawili.

Tukumbuke anatajwa kuwa ni hatari na hivyo anahitaji kupekuliwa na askari. Ni mbunge gani tena mwenye sifa hiyo isipokuwa Mwigulu Nchemba?
 
Mseme tuu ni mtikisa ------ OLE S na kiherehere km shoga yake Kilango...haka kajamaa kana shida haswa.
 
Mleta mada amehangaika wakati uandiahi wenyewe badoooo...

Mara lakini, ntarejea... Sio muda mrefu wala mfuno.. Blah blah nyiiiingi
 
Na Godfrey Dilunga: https://www.facebook.com/godfrey.dilunga

Nawaomba radhi wasomaji wangu kwa kunukuu maneno ya mwanafalsafa Dk. Phili McGraw aliyewahi kusema; kuna wakati unaweza kufanya uamuzi sahihi na wakati mwingine kufanya uamuzi kuwa sahihi (Sometimes you make the right decision, sometimes you make the decision right).

Baada ya hapo, nitaendelea na mjadala wa leo kuhusu Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba ninayemchukia angalau kwa siku hizi za awali za vikao vya Bunge la Katiba, nikijenga matumaini huenda akajirekebisha hapo baadaye.
Lakini ili kujadili vizuri zaidi, nigusie kidogo kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobeli katika Fasihi, Ernest Miller Hemingway, ambaye nitarejea sehemu ya maelezo yake ‘kushindilia’ mjadala wangu wa leo.

Kwa muhtasari tu ni kwamba, Hemingway ni mtu wa aina yake, ni mwandishi wa habari na mtunzi wa vitabu aliyewahi kuwa dereva wa gari la kubeba wagonjwa wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na alijiua Julai 2, mwaka 1961. Lakini kabla ya hapo (kujiua) alinusurika kifo katika ajali mbili za ndege.
Ni kati ya watu wachache duniani wanaotajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika karne ya 20, kwa kutazama maisha na matokeo ya kazi zake.

Alishinda Tuzo ya Nobeli katika fasihi mwaka 1954 na amewahi kuandika vitabu saba, ni raia wa Marekani lakini aliyepata kumudu kuishi maisha magumu katika nchi mbalimbali duniani, ikiwamo Cuba na hata barani Afrika.
Kuna mambo mawili ambayo Ernest alikuwa akiyaamini wakati wa uhai wake, ambayo nitayatumia kwenye mjadala wangu wa leo kuhusu mbunge ninayemchukia sana ndani ya kumbi za Bunge la Katiba.

Jambo la kwanza, aliamini; namna bora zaidi ya kujiridhisha kwamba unaweza kumwamini fulani basi kwanza ni sharti utangulize imani yako kwake, vinginevyo hutaweza kumwamini kamwe.
Lakini jambo la pili aliamini; watu wote duniani hatima yao inafanana, yaani kifo. Uwe daktari, mkulima, mwalimu, rais, waziri, mbunge au mfugaji kifo ni lazima, isipokuwa kinachoweza kutofautisha kati yako na wengine ambao nyote mmekufa au mtakufa ni taarifa kuhusu namna gani uliishi duniani na aina ya kifo chako (It is only the details of how he lived and how he died that distinguish one man from another.

Huyo ndiye Ernest miongoni mwa magwiji waliokuwa na ushawishi ndani ya karne ya 20 kutokana na kazi zao. Naam, awali nimeeleza kuhusu mbunge ninayemchukia ndani ya Bunge la Katiba.
Lakini kwa sababu Bunge hilo bado halijashika kasi sawa sawa, nitaeleza tu sifa za mbunge huyo ninayemchukia bila kumtaja jina, nikiamini kwa sasa sifa hizo pekee zitamweka katika hali ya kumtambua kwa kadiri ya matendo yake wakati wa mijadala ya Bunge.

Ni mbunge gani huyo?

Mbunge huyu anachukua posho kama wenzake wa Bunge la Katiba, ni nadhifu kwa mavazi (sitaki kutaja ni mwanamke au mwanamume).
Si mwepesi wala mzito kuzoeana naye, lakini sifa yake kubwa ni mbishi, na ni dhahiri haamini katika kile anachoamini Ernest Miller Hemingway kwamba, ingawa wabunge wote wa Bunge la Katiba watakufa, lakini kitakachowatofautisha mbele ya vizazi kadhaa vijavyo ni namna walivyotumia fursa ya kuwapo bungeni kuandika Katiba Mpya endelevu.
Kati ya matatizo makubwa ya mbunge huyu ni kwamba, ndani ya ubishi wake anapenda mno kung’ang’ania hoja za kundi lake ndizo zishinde hata kama hazina maslahi kwa taifa.

Kwake yeye kauli mbiu ni; msimamo wetu kwanza nchi baadaye, yaani msimamo wa kundi lake ni muhimu kuliko maslahi ya taifa yanayojitokeza kwenye hoja za wengine.
Taarifa nilizonazo ni kwamba mbunge huyo amejiandaa kubishana kuhusu muundo wa Muungano ambao utaligawa Bunge la Katiba katika pande kuu mbili; upande unaotaka muundo wa serikali mbili na upande unaotaka muundo wa serikali tatu.

Namchukia mbunge huyu kwa sababu hataki kusikiliza kabisa hoja za wenzake wanaotaka muundo ambao yeye na kundi lake hawautaki, na mnaweza kumbaini wakati wa mjadala atakuwa akizomea wengine wenye hoja tofauti.
Huyu yuko tayari kwa lolote. Yuko tayari kupewa rushwa na viongozi wa kundi lake ili kushawishi kwa kuwanunua wengine walioko kundi kinzani kwa lengo la kufanikisha malengo ya kundi lake hata kama hayana uhusiano na maslahi ya taifa.

Anatamani sana mabavu ya kipolisi na nguvu za dola yatumike kupitisha hoja anayoshabikia katika mvutano wa muundo wa serikali mbili au tatu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge huyu amekuwa na wasiwasi kwa kila mtu anayepinga au kukosoa anachokiamini yeye na kundi lake, wasiwasi ambao unaziba kabisa masikio yake kusikiliza utamu wa hoja kinzani kutoka kwa wenzake wanaotanguliza maslahi ya taifa wakati wa uwasilishaji wa hoja zao.

Mbunge huyu ni mtumwa wa mawazo ya kundi lake, utumwa ambao ni mbaya zaidi katika enzi hizi za uhuru wa mawazo na hasa mawazo ya ndani ya Bunge ambayo uhuru wake unalindwa kwa nguvu za kisheria. Fikra zake zimekwenda likizo na sasa kichwa chake kimesheheni fikra za kundi lake.

Kwa kweli nawashauri waangalizi wa usalama bungeni waongeze umakini kuhusu mbunge huyu, wampekue kwa uangalifu kila anapoingia ndani ya Bunge, ni mkorofi pale hoja anazozitaka yeye na kundi lake zinapopingwa.
Askari wahakikishe si tu haingii na silaha ya aina yoyote, bali hata kalamu yake (kama anayo) waichunguze, inawezekana imepachikwa sindano ndani yake ya kumchoma fulani ndani ya ukumbi wa Bunge.

Kwa kadiri Bunge la Katiba litakavyokuwa likiendelea na vikao vyake, mtamjua tu mbunge huyu hata kama kwa siku hizi za awali ameficha makucha yake. Ndiyo, mtamjua tu, si mrefu sana wala mfupi, anatokea upande mmojawapo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni kwamba ukipinga hoja ya kundi lake, basi kama ni rafiki yako, ujue urafiki umeingia doa, wewe ni adui si tu kwake bali kundi lake. Ni mbunge asiyetaka kuamini kwamba wengine wanauwezo wa kufikiri na kuibua hoja zinazotanguliza maslahi ya taifa. Ni mbunge limbukeni, amejiandaa vilivyo kuhakikisha hoja za kundi lake zinapita bila mabadiliko.
Ni mbunge asiyejua mantiki ya majadiliano, kwamba mwisho wa majadiliano ni kupitisha uamuzi kwa kuzingatia nguvu za hoja na si hoja za nguvu.

Namchukia sana mbunge huyu na kwa kweli hata Watanzania wengine, wakiwamo wabunge wenzake wataanza kumchukia siku za awali tu Bunge litakapokuwa limeanza kujadili rasimu ya Katiba Mpya itakayowasilishwa bungeni na Jaji Joseph Warioba.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Swali: Mbunge Huyu Ni Nani?

Source:Raia Mwema - Kwanini simpendi mbunge huyu wa Bunge la Katiba?
 
Back
Top Bottom