Ni hivi unaweza kumuonesha mtu udhaifu wake akajiona mjinga yeye mwenyewe bila kuitwa mjinga.
Sio busara kuita watu wajinga, kwa mfano na mimi nikija na maneno makali utaona tunaanza kuhamisha mjadala wenye hoja zenye afya kuhusu mada kuu tutabaki na matusi, na hapo uliowalenga watakosa hoja zako nzuri.
Wakati mwingi ni rahisi mtu kufuata ushauri wako kama haujajaribu kumtweza utu wake, au niite hauja 'mdharirisha', mtu akiumizwa nafsi anakuwa mgumu kupokea ushauri wako na mtaishia uadui na ushindani usio na faida.
Jambo jingine lazima utambue suala la udhaifu wa hoja ya mtu ni mtazamo, unachokiona wewe ktk nafasi uliyopo na taarifa ulizo nazo unaweza kuona hoja yako ni ndio sahihi, lakini ukiwa sehemu nyingine au katka nafasi nyingine ambayo unaona hoja yake dhaifu unaweza kuona yeye aliona au alijua kitu sahihi na wewe hoja yako ilikuwa dhaifu kwa muktadha huo mpya.
Its about perspective, we view things from different angle, different perspectives.
Tafadhari sana mkuu nakuomba uangalie hiyo video ya mdau toka Harvard utajifunza kikubwa sana na kuanza kuheshimu mawazo ya kila mtu. Usisahu ku-switch on subtitles , captions.