Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumekopa mpk hela ya kulipa mishahara ya wafanyakazi toka nchi za magharibi kwahiyo siyo rahisi tukapinga jambo ama msimamo wao.Kama hawa wamejitoa, kwanini sisi tunaogopa kujitoa? Januari Makamba anaogopa nini? Wabunge wetu wanasema nini?
Hatupingi jambo au msimamo wao wowote bali tunataka tu tuwaombe na sisi waturuhusu kuyanunua hayo mafuta ya bei nafuu kama walivyo iruhusu Japan.Tumekopa mpk hela ya kulipa mishahara ya wafanyakazi toka nchi za magharibi kwahiyo siyo rahisi tukapinga jambo ama msimamo wao.
Nadhani ni kwa sababu ya kuogopa kuharibu mahusiano yetu ya kidiplomasia na jamaa zetu ambao wanaweza pia kutuwekea vikwazo (sanctions) kama ambavyo wameanza kuiwekea sanctions nchi ya Uganda kwa kupitisha sheria kali sana dhidi ya mashoga na wana LGBTQQIP2.Japan wamekea Russia vikwazo kwa mambo mengine, lakini mafuta hayamo kwenye orodha ya vikwazo. Sisi hatujaiwekea Russia vikwazo kabisa, kwa nini tuombe ruhusa kununua mafuta ya Russia?
Kama wao wenyewe wenye vikwazo wananunua, kwa nini sisi tusinunue kwa uhuru?
Hiyo ni kweli kabisa. Serikali na bunge limwagize CAG na TAKUKURU kulifanyia special audit jambo hili linaloangamiza uchumi wa nchi yetu. Hawa jamaa watashiba lini na kuacha upigaji huu? Imefikia hadi wanabadili tarakimu za invoice za wanaotudai hususani ile invoice ya ndege ya mizigo aliyoigundua raisi wetu.Mimi nina mashaka huko wanakonunua sasa kuna cha juu wanapata, maana sio kwa ujinga huu wa kuumiza watu kiasi hiki.
Japan waliruhusiwa na G7 kununua haya mafuta yaliyowekewa international sanction ya bei nafuu. Kwa nini na sisi tusiwaombe hawa rafiki zetu waturuhusu na sisi kuyanunua haya mafuta ili kunusuru uchumi wetu?
Ni kweli kabisa Bw. Kennedy. Inabidi kuwa wanyenyekevu na kuyaomba kwa heshima na taadhima, mataifa haya makubwa duniani yaturuhusu kufanya hivyo. Kazi hii waziri wetu wa mambo ya nje anaimudu sana kwa niaba ya raisi wetu.Kwanza Ujue Nchi Ombaomba Huwa Masuala Mazito Ya Migogoro Hasa Ya Mataifa Yenye Nguvu Duniani Hubaki Njia Panda Yakitazama Tu Yasijue Yafanye Nini
Lazima Huwezi Kununua Mafuta Ya Nchi Iliyowekewa Vikwazo Wakati
Sisi Hatujiwezi, Maana Yake Endapo Utanunua Vikwazo Vikiwekwa Ndani Saa 24
TTutakuwa Hoi Maeneo Yote Na Uchumi Utazorota
Yanapatikana kule ambako hayajawekewa sanctions. Kule ambako USA na EU wanakonunua. Ni kule nchi za Uarabuni isipokuwa Iran ambayo iko kwenye sanctions kwa mingi. Baada ya vita ya Ukraine kuanza na Urusi kuwekewa sanctions kwenye mafuta na gesi yao, hawa Waarabu walipandisha maradufu bei za mafuta yao na gesi na bado wanaendelea kuyapandisha hadi sasa.Una uhakika ni wapi mafuta yetu yanapatikana?
Naam tupo Pamoja, Mkuu.Nadhani sasa Bw. TUJITEGEMEE tuko pamoja.
Japan waliruhusiwa na G7 kununua haya mafuta yaliyowekewa international sanction ya bei nafuu. Kwa nini na sisi tusiwaombe hawa rafiki zetu waturuhusu na sisi kuyanunua haya mafuta ili kunusuru uchumi wetu?
Issues zote za uagizaji mafuta, karibu mitaa hii
P
Issues zote za uagizaji mafuta, karibu mitaa hii
P
Nadhani jibu la maswala yako yote ni ufisadi, ufisadi, ufisadi tu. Hii ndiyo sababu iliyotufanya na inayoendelea kutufanya tusinunue mafuta hayo ya bei nafuu toka Urusi. Hizo sababu zingine ni visingizio tu.Naam tupo Pamoja, Mkuu.
Sema sasa, yameshuka maswali kibao kichwani mwangu:
1. . Sasa najiuliza, sanction amewekewa Russia ama amewekewa Russia na Sisi(Tanzania)? Hivi kutoelewana kwa US na Russia juu ya suala la Ukraine inakuwaje sisi tuwekewe vikwazo (haturuhusiwi kununua mafuta ya bei nafuu huko Russia)?
2. Kwanza sera yetu ya mambo ya nchi za nje nadhani haijabadilila, kuwa sisi kama nchi ya Tanzania hatufungamani na upande wowote. Sasa inakuwaje sasa tunaamua kukubali kumuunga mkono (kufungamana) US kujizuia(sina hakika kama tumezuiwa) kutonunua mafuta ya bei nafuu kutoka Russia na Iran ikiwezekana? Kwa nini, yaani ?
3. China na India wananunua mafuta Russia ya bei nafuu, na hizo ni nchi huru, na sisi Tanzania ni nchi huru, Sasa iweje sisi tushindwe kwenda kununua mafuta ya bei nafuu huko Russia? Au inatakiwa itakangazwe rasmi kuwa Tanzania siyo nchi huru kiasi haiwezi kujiamulia mambo yake yenyewe? Yaani kwamba sasa inatakiwa kuanza 'movement' mpya ya kupigania uhuru upya wa kujiamulia mambo yanayotuhusu kiuchumi hasa kama anavyofanya J. Malema wa Afrika Kusini? Kwamba sasa ni muda muafaka kuanzisha 'EFF' nchini?
4. Russia ina ubalozi nchini na sisi tuna ubalozi Russia, ni kwa nini tunasusia kununua mafuta ya Russia ili tuweze kupata unafuu wa kupunguza gharama za maisha nchini, maana mafuta ni bidhaa muhimu kwenye maendeleo?
5. Kwa nini tusitumie India na China marafiki zetu wanunue mafuta ya Russia kwa niaba yetu watueletee ama tukachuke kwao, kama labda wanunuzi kutoka kwetu hawawi kuongea kirussia wakati wa manunuzi?
Yaani maswali maswali maswali...sielewi kabisa kinachoendelea?
Dr Akili na wengineo kama mtapata wasaa pitia na maswali haya.
Natanguliza shukrani kwa majibu.
Mkuu, Pascal Mayalla , ukipata wasaa naomba urudi Tena Wizara umtafute yule Mkurugenzi/kamishna wa "uagizaji mafuta" uliyezungumza kwa kirefu kwenye video uliyotuwekea.The top importers of Russian gasoline, despite the sanctions as from March 2022 up to January 2023 in USD billions are as follows:
China $ 66.6 Billions, Germany 26.1, Turkey 25.9, India 24.1, Italy 14.8, Poland 12.18, France 9.5, Belgium 9.2, Hungary 8.68, Bulgaria 6.28, Japan 6.08, South Korea 6.08, Spain 5.88, Austria 5.78, Egypt 5.48, Greece 4.58, Czechia 4.28 and UAE 4.18
Mimi nadhani hakuna haja ya kuwaomba, bali ni kuwalazImisha, kama hawataki, tutafute wananunuaji wengine wa mafuta. Na hii ndiyo hasara ya kuwa na ununuzi wa " Bulk " Kwa namna moja ama nyingine, Bulk ni aina nyingine ya "cartel"!!!! Vinginevyo, labda Mimi sielewi haya mambo hivyo nahitaji kuelimishwa.Kwa nini na sisi tusiwaombe hawa rafiki zetu waturuhusu na sisi kuyanunua haya mafuta ili kunusuru uchumi wetu?
Naunga mkono hoja kwa asilimia 100% chini ya 100%.Mkuu, Pascal Mayalla , ukipata wasaa naomba urudi Tena Wizara umtafute yule Mkurugenzi/kamishna wa "uagizaji mafuta" uliyezungumza kwa kirefu kwenye video uliyotuwekea.
Ukimpata, umueleze kuwa takwimu zinaonyesha bado Russia Anaendelea kuuza mafuta yake kama kawaida na Hata nchi zilizomuwekea vikwazo bado Zina nunua mafuta yake. Muonyeshe takwimu alizotuletea Dr Akili kudhibitisha hoja, hoja inayopingana na maelezo yake.
Baadaye tutamuomba Dr Akili atupe link ya chanzo cha takwimu zake hizi.
Kwa staili ya kupashana habari baina yetu wananchi kupitia JF kisha Baadaye kwa serikalini kupitia connection yetu hapa jukwaani ya Ndugu yetu wa Kwa maslahi ya Taifa' Bwana Pascal Mayalla tunaweza kulisaidia Taifa letu kusonga mbele endapo tu hakutakiwa na Hila ya aina yoyote kwa watendaji na wananchi pia.
www.visualcapitalist.com