Siamini kama kuna mtu alizaliwa aje kuwa maskini.Ila waafrika wengi ni maskini kutona na sababu kadhaa.Ngoja nikuelezee chache kama ifuatavyo:
1.UVIVU
Hapa utakubaliana na mimi kuwa uvivu ni tatizo kubwa sana kwetu waafrika.Japo tunatofautiana kiwango cha uvivu,lakini kwa ujumla wengi ni wavivu.
Tunapenda sana mteremko na easy way.Hakuna anayependa kujituma.Utendaji kazi wetu ni mdogo lakini starehe na matumizi yako juu.
Kwa mtindo huu wa maisha sidhani kama tutaweza kupiga hatua.Na hata tukipiga hatua,basi itakuwa ni za kunyata.
2. MENTALITY
Blacks and African kwa ujumla we got negative perspective in most of the things.
Tunaendekeza sana imani potofu na kukatishana tamaa au kuwa katisha tamaa wengine.
Mtu yuko radhi aghairi kufanya jambo mara tu baada ya kudhani litakuwa gumu.Tunakata tamaa hata kabla hatujajaribu.
Kwa kiasi flan uoga wa kushindwa umetukwamisha sana.
3.SELFISHNESS
Dah,mkuu ili ni tatizo kubwa sana sehemu nyingi.Ila kwa bahati mbaya kwetu ni janga kubwa sana.
Ni vigumu kuwa na maendeleo ikiwa wanaokuzunguka wana hali mbaya kiuchumi,maana kila siku watakuwa wanakupiga mizinga na kukurudisha nyuma.
Ila endapo jamii inayokuzunguka ikiwa walau ipo vizuri kiuchumi basi hata maendeleo huweza kuja haraka.
Watu hupenda kujifkiria wao wenyewe bila kujali wengine,ndio maana hata maendeleo yanagoma.
Mfani viongozi watajifkiria wao kwanza alaf ndio waje kuendeleza nchi.Miaka minne ya uongozi wanachumia matumbo yao kwanza.Alaf mmoja uliobaki watautumia kuwa karibu na wananchi kwa ajili ya kujitengenezea mazingira ya kuchaguliwa tena kipindi kijacho.
4.UPENDO
Matajiri usaidiana walau wawe juu na waweze kupiga hatua,ila wengi wetu (hasa Africans) huwa tunafurahia wenzetu wanapoanguka.Kuna siku nilimsikia mama mmoja akicheka huku anamwambia mwenzake "Afadhali mwanae amefeli kama mwanangu,maana angefaulu ingekuwa kero hapa mtaani" Nilibaki najiuliza tu,tutafika kwa mtindo huu??
Upendo hakuna kati yetu.Aliyenacho hataki kumsaidia walau mawazo yule hasiyenacho.
Na hasiyenacho ameshakata tamaa na hana mpango wa kujishughulisha zaidi.
Kiukweli tunasafari ndefu sana ili tuje kufika salama mwisho wa hii safari.
#Analyse