Kwanini sisi waafrika pekee tuna rangi nyeusi tii, tofauti kabisa na binadamu wa mabara mengine?

Kwanini sisi waafrika pekee tuna rangi nyeusi tii, tofauti kabisa na binadamu wa mabara mengine?

The king mswati

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2020
Posts
787
Reaction score
825
Wakuu merry chrismass.

Nimekaa nimewaza na kufikiri naona kama kuna kitu hakiko sawa kuhusu sisi waafrica.

kitu cha kwanza ni kwanini sisi waafrika pekee tuna rangi nyeusi tii, tofauti kabisa na binadamu wa mabara mengine, mfano ulaya ni weupe,asia ni weupe,australia ni weupe,america kaskazini na kusini ni weupe (isipokuwa black americans tu ambao nao pia wanatokana na mababu zetu waliopelekwa utumwani kule).
so najiuliza kwanini only africans are the black people ? Kwa majujibu wa takwimu za population, dunia mpaka sasa ina watu bilion 7.8, na africa pekee ina watu bilion 1.3 tukijumlisha na yale masalia ya america na carribean labda tunakuwa 1.4 au 1.5 billion ndo watu pekee weusi duniani, maana ake kati ya watu bilion 7.8 weusi ni 1.5 bilion pekee,wengine wote wanaobaki ni weupe, kwanini yani weupe mbona wengi sana, je imekuwaje weusi wakawa wachache alafu wametengewa bara lao, maana mabara yote 6 yenye watu matano ni weupe isipokuwa bara moja tu la africa ndo weusi tii why mbona sipati majibu sahihi ? Sijichukii kwa sababu mimi mweusi ila najiuliza tu kwanini waafrica pekee ndo weusi ? Alafu pia wakawa wachache kuliko weupe ? Kuna laana gani ilipita hapa ebu nambieni wadau.

Kitu cha pili, kwanini sisi watu weusi tunaonekana tuko nyuma kwa karibu kila kitu, kuanzia ustaarabu watuletea watu weupe, teknolojia nyingi zimetoka kwao (asilimia karibu 90 ya kila tunachotumia waafrica kilianza kwanza kugunduliwa na mweupe), kwanini mweusi akawa nyuma sana ? Kuna laana gani hapa ? Kwanini sifa ya mwafrica ni ya umaskini na ujinga tu why this ? Walitutawala kwa karne karibu 4, wakatutumikisha kwenye ardhi yetu wenyewe na kutufanya watumwa na sisi tukakubaliana na hali, why only africans we became very stupid ? Mbona sisi hatukuanza kuwatawala ila wao weupe wakaanza? Tuna rasimali kibao ila tumeshindwa kuzitumia zituboreshee maisha badala yake bado tumkabidhi mtu mweupe, kwanini sisi watu weusi tuna nini ebu nipeni majibu!

Cha mwisho, kwanini ngozi nyeusi inabaguliwa (racisim) na kuonekana duni, nadhani tunashuhudia wenzetu walioko ng'ambo jinsi wanavyobaguliwa na kuitwa nyani, ina maana sisi weusi duniani tulikuja bahati mbaya au ni vipi yani !...niki mnukuu mwarabu moja mweupe pale libya ambaye aliwateka waafrica wakiwa wanatorokea ulaya kupitia mediterania aliwaambia hivi "mnaenda wapi nyie watu weusi kutoka kuzimu watumwa mliolaaniwa ninyi"

Unaweza kuona ni jinsi gani sisi watu weusi tunavyochukuliwa na watu weupe, sasa kwanini sisi waafrica tukaumbwa weusi (rangi ya kudharaulika,duni) alafu tukawa wachache na bado haitoshi tukapewa bara la peke yetu weusi (bara la africa) wakati weupe wao wakaumbwa wengi alafu wakasambazwa kwenye mabara matano tofauti na pia wakapewa upeo wa uelewa kuliko sisi ? Au ni kweli mungu alitulaani nini sisi weusi ? Au sisi weusi ni uzao wa shetani kama wanavoamini baadhi ya weupe ?

NB: Sijaudharau uafrica wangu ila najiuliza tu kwanini mweusi anadharauliwa na kudunishwa wakati mweupe yupo mbele yetu kwa karibu kila kitu?
 
Mimi wa kwanza,

Ngoja nijaliwa kwa uelewa wangu.
Mbongo (African)siyo mweusi tu bali yeyote anaweza kuwa muafika.

Kuhusu rangi nyeusi isikupe shida ni Nature yenyewe ikumbukwe hili bara linapata jua kamili hivyo kuwa weusi nikwasababu ya ngozi iweze kuhimili miale mibaya ya jua (mawazo yangu).

Halafu bara letu ni zuri kuliko huko unakokusifia sisi hatuna mavimbunga sijui yakutisha, masunami, matetemeko, mavolcano hata kama yapo lakini siyo kama wao.

Pia kuhusu kutawaliwa na weupe ni sawa hii inaitwa kutesa kwa zamu hata sisi tulishawahi kuwatawala ila sema ilifichwa na hao hao kuogopa aibu, Kuna mtu alikuwa anaitwa Malkia wa Sheba, kuna hawa jamaa Mafarau wa misri, inasemekana walikuwa weusi kabisa na hii ijulikana kupitia ugunduzi wa ile miili kufukuliwa kwenye makabuli huko Cairo na kukuta jamaa ni weusi tii.

Ngoja waje wataalam wakupe mkuu.
 
Huyu ni mhindi
1640410720742.png
 
Mimi wa kwanza!
Ngoja nijaliwa kwa uelewa wangu.
Mbongo {African}siyo mweusi tu bali yeyote anaweza kuwa muafika.
Kuhusu rangi nyeusi isikupe shida ni Nature yenyewe ikumbukwe hili bara linapata jua kamili hivyo kuwa weusi nikwasababu ya ngozi iweze kuhimili miale mibaya ya jua {mawazo yangu}
Halafu bara letu ni zuri kuliko huko unakokusifia sisi hatuna mavimbunga sijui yakutisha, masunami,matetemeko,mavolcano hata kama yapo lakini siyo kama wao.
Pia kuhusu kutawaliwa na weupe ni sawa hii inaitwa kutesa kwa zamu hata sisi tulishawahi kuwatawala ila sema ilifichwa na hao hao kuogopa aibu,
Kuna mtu alikuwa anaitwa Malkia wa Sheba,kuna hawa jamaa Mafarau wa misri,inasemekana walikuwa weusi kabisa na hii ijulikana kupitia ugunduzi wa ile miili kufukuliwa kwenye makabuli huko Cairo na kukuta jamaa ni weusi tii.
Ngoja waje wataalam wakupe mkuu.
mkuu kuna kitu hapa ndo naanza kukiskia kwako kwa mara ya kwanza kwamba "hata sisi tumewahi kuwatawala ila ilifichwa kwa kuogopa aibu" je ni kweli ulisemalo ? waweza nambia labda ni kipindi gani ama karne gani tuliwahi kuwatawala wazungu ?
 
Wahindi wengi ni weusi, Australia kabla mzungu ilikuwa watu weusi, Papua new guinea weusi, Hawaii kabla mzungu weusi, Amerika ilikuwa weusi kabla colombus kufika, Spain & Portugal(Iberia) ilikuwa watu weusi wakati moors walitawala Uhispania, South Amerika vile vile haswa Equador, Honduras, Colombia na Caribbean.
 
Rangi ya mwafrika inatokana na mazingira ukandaa tunaoishi ni wajua kali so melalinin inablock uv ili isiharibu seli za ngozi ili tusipate kansa, kuwa nyuma kimaendeleo hii naiweka katika sehemu mbili kwanza vurumai la ukoloni/utumwa(dini za kigeni) la pili ni sisi waafrika kutotaka kuendelea na misingi yetu ya maisha kuvurugwa mfano hatu mfumo wa kupata viongozi sahihi viongozi wetu ni kama sio washamba wa wazungu/non-african basi wanawatumikia wazungu/non-african.

Nimalize kwa kusema, iamini sayansi uokoke.
 
Si Waafrika tu wenye ngozi nyeusi, isipokuwa sisi ni baba wa watu wenye ngozi nyeusi...

Hizi races zilizopo duniani, zina wanadamu wenye asili ya awali kuliko wengine na kuna races ambazo ni mchanganyiko wa aina mbili au zaidi ya races za awali...

Melanesians (hawa wanapatikana visiwa vile vidogo vidogo vilivyo ndani ya bahari ya Pacific)...

Indigenous Australians 'Aboriginal' (hawa ni watu ambao ndio asili ya mwanadamu aliyekuwa akiishi Australia kabla ya uvamizi wa wazungu)...

Blasians, Siddi, Negritos n.k n.k zote hizi ni jamii za watu weusi waliopo Asia na visiwa vyake, yaani hawa ni weusi tii, ukiwaleta Afrika wala hutawashangaa...
 
mkuu kuna kitu hapa ndo naanza kukiskia kwako kwa mara ya kwanza kwamba "hata sisi tumewahi kuwatawala ila ilifichwa kwa kuogopa aibu" je ni kweli ulisemalo ? waweza nambia labda ni kipindi gani ama karne gani tuliwahi kuwatawala wazungu ?
Andalusia 700AD - 1400 AD Granada and Cordoba in Spain. Ndio maana wahispania na Portuguese wako tofauti sana kimaumbile ukilinganisha na wenzao kutoka Britain na Scandinavia.
 
Hoja yako ya kwanza kuhusu Weusi Ni hoja ya kijinga kabisa kabisa...

Yani mbugani Swala ajiulize kwanini kwanini sisi tunaliwa sana na Simba?

Yani badala ya kujivunia kuwa uko Unique unaanza kusema Weusi ni laana? Ndugu unakosea sana, tena sana.

Umepewa bara kubwa hili lina kila kitu, nasema kila kitu, post yako ilitakiwa ianze kwenye aya uliyoanza kuzungumzia uduni waaendeleo ya Afrika hapo ungekuwa unaongea vitu vya msingi...
 
kwanini weusi wanadharauliwa, wanadunishwa,wanabaguliwa, kwani kuwa mweusi ni laana gani hapo
Tuanze na historia ya ubaguzi. Tuonze na waarabu then tuje kwa wazungu.
Waarabu walianza kubagua waafrika kwasababu waliamini hawamjui mungu wao allah na wakatumia vitabu vyao vya dini kuwa kumchukua mtu yeyote utumwani kama sio muislamu.

Kutokana na maagizo ya vitabu vyao na mazoea ya kuchukua waafrika utumwani wakajijengea mazoea ya kudharau waafrika mpaka leo mpaka siku mwafrika atapoachana na ushamba dhidi ya dini yao na ushamba dhidi ya uarabu wao.

2. Mzungu ndio kinara wa ubaguzi yeye ndio alifanya ubaguzi dhidi ya waafrika uzagae ulimwengu mzima kupitia biashara ya utumwa, ukoloni then dini na vipindi vya video, vitabu, michoro , vibonzo na vinginevyo.

Mzungu ndio aliyeweka ubaguzi wa kimkakati (systematic and institutional racism) tuanza na papa wa vatican kuandika barua ya kuruhusu wazungu kuchukua waafrika utumwani kwasababu ya rangi yao.

Wareno, wahispania , wafaransa na waingereza kupitisha sheria kandamizi za kibaguzi dhidi ya watumwa wa kiafrika.

Waingereza ndio walikua vinara ila kwasasa wamarekani ndio wafalme wa ubaguzi.

NB: waafrika hatuna rafiki zaidi ya sisi wenyewe ni vile tuu tumeamua kumuachi mustakabali wa maisha yetu kitu kinachosadikika ni mungu. Ambayo kwenye vitabu hivyo tunavyovifuata huyo mungu alikua anahamasisha watu wachukuliwe utumwani
 
Rangi ya mwafrika inatokana na mazingira ukandaa tunaoishi ni wajua kali so melalinin inablock uv ili isiharibu seli za ngozi ili tusipate kansa,
kuwa nyuma kimaendeleo hii naiweka katika sehemu mbili kwanza vurumai la ukoloni/utumwa(dini za kigeni) la pili ni sisi waafrika kutotaka kuendelea na misingi yetu ya maisha kuvurugwa mfano hatu mfumo wa kupata viongozi sahihi viongozi wetu ni kama sio washamba wa wazungu/non-african basi wanawatumikia wazungu/non-african.

nimalize kwa kusema , iamini sayansi uokoke
nianze kwa kusema sayansi na kuokoka havina uhusiano bali vina ukinzani, lakini la msingi ninalotaka kukwambia ni kwamba "suala la sisi kuwa weusi kunasababishwa na mazingira" hili nakataa kwa asilimia mia.

hivi kwa mfano ww na mke wako kama ni waafrica mkaenda kuishi nchi ya ICELAND penye baridi kali kabisa, unataka kunambia kuna siku nyie mtazaa mzungu kisa hakuna jua ? Walah nakwambia hata kizazi chako cha mia moja toka wewe na mkeo bado hakitazaa mzungu hata mmoja, kwa hiyo suala la mazingira mi naona linafeli halina mashiko kabisa.

Mfano mwingine angalia nchi kama INDIA watu hufa na joto kali kila mwaka lakini mbona wanazidi kuzaliwa weupe, kuna nchi kibao ziko jangwani (hasa za kiarabu) na joto lipo la maana tu, mbona waarabu hawazaliwi weusi wanazidi kuzaliwa weupe ? Point yako ya mazingira haijitoshelezi kabisa, ni sawa na kutuambia binadamu alitokana na sokwe wakati sokwe wa sasa hawageuki kuwa binadamu.
 
Wahindi wengi ni weusi, Australia kabla mzungu ilikuwa watu weusi, Papua new guinea weusi, Hawaii kabla mzungu weusi, Amerika ilikuwa weusi kabla colombus kufika, Spain & Portugal(Iberia) ilikuwa watu weusi wakati moors walitawala Uhispania, South Amerika vile vile haswa Equador, Honduras, Colombia na Caribbean.
kama walikuwa ni weusi saivi wameenda wapi mbona kunakaliwa na weupe, kuna mtu aliwahi kunambia hata WAYAHUDI walikuwa ni weusi sasa sijui hawa kina NETANYAHU wametokea wapi
 
nianze kwa kusema sayansi na kuokoka havina uhusiano bali vina ukinzani, lakini la msingi ninalotaka kukwambia ni kwamba "suala la sisi kuwa weusi kunasababishwa na mazingira" hili nakataa kwa asilimia mia.

hivi kwa mfano ww na mke wako kama ni waafrica mkaenda kuishi nchi ya ICELAND penye baridi kali kabisa, unataka kunambia kuna siku nyie mtazaa mzungu kisa hakuna jua ? Walah nakwambia hata kizazi chako cha mia moja toka wewe na mkeo bado hakitazaa mzungu hata mmoja, kwa hiyo suala la mazingira mi naona linafeli halina mashiko kabisa.

Mfano mwingine angalia nchi kama INDIA watu hufa na joto kali kila mwaka lakini mbona wanazidi kuzaliwa weupe, kuna nchi kibao ziko jangwani (hasa za kiarabu) na joto lipo la maana tu, mbona waarabu hawazaliwi weusi wanazidi kuzaliwa weupe ? Point yako ya mazingira haijitoshelezi kabisa, ni sawa na kutuambia binadamu alitokana na sokwe wakati sokwe wa sasa hawageuki kuwa binadamu.
naomba uanze kwa kusoma historia ya mwanadamu wa sasa homo sapiens utaelewa sis tumetokawapi mpaka kufika hapa. Hakuna mwanadamu hapo ulimwengu ambaye asili yake sio afrika.

Mutation na evolution haitokei kwa vizazi vinne au vitano kwa viumbe kama binadamu wazungu walitoka afrika miaka 12000 iliyopita , so mazingira yalipekea kutokea mutation ya gene inayocontrol melanin ikawa inapungua nguvu na chance ya kusurvive kwa watu waliokuwa weupe ikawa kubwa kwasababu sehemu walizokuwa wazungu hakuna jua so weupe waliweza kutengeneza vitamin D nyingi zaidi ya watu weusi waliokuwa huku ulaya . Ndio maana mpaka leo watoto wote ulaya wanapewa dawa ya vitamin D na waafrika wa ulaya wanashauriwa watumie vitamin D sana maana ngozi yao inapunguza uwezo wa kufonza nguvu za kujua kutengeneza vitamin d

kusema iamini sayansi na uokoe namaanisha kuwa sayansi ndio itakuokoa usipate magonjwa uondokane na ujinga na kukuepusha na utapeli mwingi wa huu ulimwengu

Napenda kuwaalika Kiranga Scars kuongezea information pale ambapo hapajatosha.
 
Hakuna kingine zaidi ya laana.Maana tuko nyuma kwa kila kitu,kuanzia uchafu hadi majungu. Nadhani ni Nature yenyewe ndiyo iliyotuchagua hivyo.

Ndo maana ata hivyo vizazi vya binadamu weusi walioko uko kwenye mabara mengine yenye binadamu weupe ni matokeo ya waafrika kupelekwa uko na watu weupe kama nguvu kazi.kwahiyo walivyofika walizaana ila bado ustaarabu wao na tabia zao hazitofautiani sana na sisi tuliozaliwa huku afrika.

Kwahiyo utaona jinsi ambavyo kuna chembechembe flani za tofauti kwenye binadamu mweusi haijalishi kazaliwa wapi.

Tatizo ninaloliona ni kwamba inawezekana tuna limit ya uwezo wetu wakufikiri na kutenda tofauti na binadamu wengine, inawezekana tumeumbwa mechenical zaidi tofauti na wengine ndo maana hatusumbui sana vichwa kufanya maboresho ya maisha yetu na gunduzi mbalimbali.

Kwa hali hiyo lazima tuzarauliwe kwasababu hatuna jambo lolote kubwa la kujivunia dhidi ya race zingine.zaidi sana tunasubiri wao ndio wafikiri kwa niaba yetu kisha watuelekeze nini cha kufanya.

Hapo bado sisi wenyewe kwa wenyewe hatupendani na tunadharauliana.Ata kuongozana tu kistaarabu hatuwezi. Kwahiyo iko shida ndani yetu japo wengi watakataa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Labda tuombee msamaha kwa Muumba maana hata hatujui maana ya "mda". Waafrika tunaishia kuangalia Wazungu wakigundua mambo kisayansi.

Namshangaa hata walipoleta dini zao hawakuamini kama mwafrika ni binadamu kamili. Pata huu usemi " kama wewe ni binadamu ninakubatiza, kwa jina la Baba Mwana na Roho mtakatifu"

Kulikuwa na kitabu cha kuombea "washenzi wa Afrika" .Ila tunaweza kufanya mapinduzi ya kifikra, tuache kudharauliana, wivu, kupiga madili.

Swala ni kujiamini.
 
Hoja yako ya kwanza kuhusu Weusi Ni hoja ya kijinga kabisa kabisa...

Yani mbugani Swala ajiulize kwanini kwanini sisi tunaliwa sana na Simba?

Yani badala ya kujivunia kuwa uko Unique unaanza kusema Weusi ni laana? Ndugu unakosea sana, tena sana.

Umepewa bara kubwa hili lina kila kitu, nasema kila kitu, post yako ilitakiwa ianze kwenye aya uliyoanza kuzungumzia uduni waaendeleo ya Afrika hapo ungekuwa unaongea vitu vya msingi...
Kwani wewe laana unafikiria ni kitu gani?.Hiyo hali yakukufanya uwe duni dhidi ya wengine ndo laana yenyewe.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom