Kwanini sisi watu weusi hatuvumbui vitu?

Yote hapo majibu. Pia ongeza ubinafsi na roho mbaya ni moja pia ya sababu. Ndio maana mzazi anashindwa kujenga nyumba halafu anazaa anataka watoto ndio wamjengee.. hatuna utaratibu wa kua na dira.
 
Kweli kabisa, shida kubwa ni mitaji ya kuchezea hadi kitu kije kukubalika na jamii

Mfano sisi wakati tuko wadogo miaka kabla ya kuja simu za mkononi tulikuwa tunaweka nyuzi za manila kwenye vikopo viwili halafu mmoja anasimama umbali wa mita mia tunaanza kuongea na sauti zinasikika vizuri tu
 
Kati ya point zoote 13 ulizo orodhesha hapo umesahau ile ya kunyimwa kwa makusudi FURSA. Kwa mfano wapo wataalam wa UDOM majuzi kati hapo walidai kugundua dawa ya kuponyesha na Kutokomeza kabisa UKIMWI lakini walikosa kuungwa mkono na Serikali; pia wapo wengine huko Arumeru na Sngida lakini ufuatiliaji/ kuwaendeleza imekuwa ni shida.
Wapo Watz wengi wenye vipaji tofauti-tofauti lakini wanakwama kwenye uwezeshwaji
 
Kwa nini hawawezeshwi, tatizo ni nini?
 
Kwa nini hawawezeshwi, tatizo ni nini?
Mkuu; Ni majanga tupu. Hebu fikiria/Tafakari wakiwezeshwa na ikathibitika ni kweli inaponyesha kabisa; vile viwanda vya kutengeneza ERVs si vitafungwa? Ni hasara kubwa sana kwa matajiri-wamiliki wa viwanda hivyo. Kwa mantiki hiyo wale Big Pharma companies hawatakuacha salama. Wataweza kuwanunua wakubwa ili wakukwamishe. Ukizingua zaidi watakupoteza mazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…