Kwanini TACAIDS na Waziri wa Afya imenyamazia ishu ya Cherry na Dotto Magari?

Kwanini TACAIDS na Waziri wa Afya imenyamazia ishu ya Cherry na Dotto Magari?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
Kutwa Serikali kupitia Wizara pamoja na TACAIDS mlikuwa na Kampeni yenu ya Kupinga Unyanyapaa kwa Watu walioathirika na VVU.

Sasa kama ile Kampeni yenu ilitumia Mabilioni ya Fedha kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari kupinga Unyanyapaa hivi ingekuwa kweli imefanikiwa huu Upumbavu wa akina Cherry, Dotto Magari na Isa Tambuu pamoja na hata Members wengine hapa kuanza Kukejeli Waathirika wa VVU na Kuchafuana ungekuwepo?

Njooni huku nchini Uganda muone jinsi gani Waganda wametuacha mbali katika suala hili zima la Stigmatization (Unyanyapaa) kiasi kwamba Mtu akiwa na UKIMWI / VVU baada ya Kugundulika wala hashtuki na hata Wananchi pia hawashtuki kwani wameshaelimishwa kuwa VVU / UKIMWI siyo Kufa au mwisho wa Mtu kuendelea kupambana na Maisha.

Wasomi wazima tunaacha kujadili Mambo ya maana ya kuikomboa Kiuchumi Tanzania yetu Sisi kutwa tuko katika Kushadadia jambo la Kawaida sana kwa wenye Akili kubwa.

Tunamcheka Dotto Magari kuambiwa ana VVU ambao hata hatujahakikisha kama anao kweli huku tukisahau kuwa wengine hapa huko katika Familia zetu si tu tunauguza bali tumeshazika Ndugu zetu wengi na baadhi yetu pia (GENTAMYCINE Simo) tumeshaathirika, ila tunazuga tu kupitia Kumcheka Dotto Magari.
 
Na tulivyo Wapumbavu zaidi tunamcheka Dotto Magari kuambiwa ana VVU ambao hata hatujahakikisha kama anao kweli huku tukisahau kuwa wengine hapa huko katika Familia zetu si tu tunauguza bali tumeshazika Ndugu zetu wengi na baadhi yetu pia (GENTAMYCINE Simo) tumeshaathirika, ila tunazuga tu kupitia Kumcheka Dotto Magari.
Kwa hio unavyotaka kutuambia DOTTO MAGARI ana umeme wa kuchomelea Mageti au ana umeme gani grid ya Taifa?
 
Back
Top Bottom