Kwanini TAKUKURU hawatakiwi kuendesha kesi

Kwanini TAKUKURU hawatakiwi kuendesha kesi

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2008
Posts
2,502
Reaction score
741
kwanini pccb wasiachiwe kuendesha kesi zao, hivi wanaoelewa hili mnasemaje?
 
polisi walibambika sana watu kesi kwa mfumo huo.
 
Ubungoubungo ile case ya Ikerege mbona imeendeshwa na mwanasheria wa PCCB na angalau kashinda case japo kwa adhabu ndogo. Sasa ukisema PCCB sio wazoefu, hao wa DPP Wameshinda case gani? Au case zao zote ni kulalamika ushahidi hautoshelezi?
 
Last edited by a moderator:
mengi ni ya kweli lakini hapa labda tu ni uadilifu wa mtu., maana siku hizi hata hao waendesha mashtaka wa serikali wamekuwa wakichukua advantage faili likifika kwao kama linamapungufu ya kisheria au ushahidi badala ya kumshauri mpeleleze arekebishe wao wanavuta mkwanja toka kwa mlalamikaji kesi holaaaa
 
very correct,

sio haki taasisi ileile ifanye uchunguzi, kukamata na kushitaki mahakamani, hapo lazima kutakuwa na double standard tu. utaiaminije taasisi moja kufanya hayo yote.

however kwenye suala la uadilifu ni kweli mawakili wanatakiwa kuchujwa na kuadibishwa kama wanachukua rushwa. lakini nakubaliana na mtoa hoja kuwa si sahihi taasisi moja kujilimbikizia majukumu yote hayo,kuna uwezekanoo kubambika mtu kesi. all in all vyovyote vile itakavyokuwa kama haki inatendeka basi hakuna shida.

watu wanahitaji haki ionekane kutendeka kuliko kusikia tu.
 
Law is living entity Ndg yangu, Maisha yake yako kama wewe mtanzania katika serikali ya kitanzania!

Be patient.
 
mbona wanaendesha kesi wenyewe wewe
anachosema ni cha kweli kama atakuwa anaongelea kesi za pale kisutu na mahakama za juu zaidi, ila kama ni mikoani wanaendesha wao wenyewe pccb. kama kuna wakili mwenzangu wa kujitegemea humu tunajua kesi kubwa kama zile za epa ambazo walitakiwa kuendesha wao tunaona wanaendesha mawakili wa serikali, inasemekana pccb walimwomba dpp msaada wasaidiwe kuendesha ndio maana huyo jamaa anasema hawaendeshi kesi nafikiri. kesi kubwa waliyoshinda ni ile ya kajala na hiyo ya juzi ya jamaa wa tbs, nyingine zote kama za kina katiti, maranda n.k hawaendeshi pccb.

sitaki kuingilia mambo yenu nyie waendesha mashitaka lakini ukweli unabaki palepale kwamba pccb ni wabovu kupita kiasi ukiwa na mteja wako kwenye kesi ya pccb na hasaidiwi na mawakili una uhakika asilimia 100 utashinda. wale mawakili wa serikali wanasaidiwa na wakubwa wao principal state attorneys, na hata bila hivyo wamewazidi pccb mbali sana kiuzoefu na ufanisi. nashauri pccb na dpp washirikiane tu wasishindane.

wakishindana mmoja anataka kuendesha kesi mwengine hataki, mwengine anataka kuanzisha mahakama ya kwake n.k, utaanzisha ya pccb ukaacha ya madawa, na ukaacha ya pembe za ndovu? nilisikia pccb wanasema wanataka kuanzisha mahakama yao maalumu...hapo mana yake na kitengo cha madawa kitataka kiwe na mahakama yao kwasababu madawa ni serious kama ilivyo corruption, na nyara za serikali hivyohivyo tuwe na mahakama nne, hizi za kawaida, ya nyara, ya madawa na ya pccb....vipi hapo?
 
Well said brother,umenifungua sana hapo mwanzo nilikuwa nikifikiri madai ya Dr hosea dhid ya dpp ni sawa kumbe Haiko ivo
 
Kwa sababu ya uwepo wa mambo ya utawala bora yanayotaka kuwepo kw mgawanyiko wa madaraka/responsibilities. Sio vizuri jtu mmoja kuwa investigator na at the same time kuwa prosecutor, atashindwa kubalance interest. FROM THE RULES OF NATURAL JUSTICE
 
Taasisi ya kupamba na kukuza rushwa ~ takukuru

Zimepambwa haswa kwa majina chekwa epa..escrow..rikmond..dawa nzi..kagoda..meremeta...tangold...rada..import support...mabilioni uswisi....ndege ya raisi...uda...atcl.. wahindi wa trl..airtel..
 
Wapewe meno washtaki...

Tuone ikiwa huo mtizamo hapo juu utabadilika
kuna report ilitoka 2013 nakumbuka pccb ilikuwa namba 3 kwa rushwa ikitanguliwa na mahakama na polisi. wanakurupuka sana na wako kisiasa zaidii kuliko uhalisia ndio maana hata kikwete aliwapiga dongo juzi kuwa "MNAKURUPUKA: lile lilikuwa dongo anawapiga pccb, wanakurupuka sana wakati hakuna ushahidi matokeo yake kesi hawashindi na walikuwa wanashitakiwa wanalipwa fidia na serikali.

dunia nzima, hauwezi kukakamata wewe, ukapeleleza wewe, ukashitaki wewe mwenyewe, lazima kunakuwa na uonevu naubambikaji wa kesi. pccb wameshaprove failure mara nyingi sana hasa kwenye upelelezi na hakika hawatakiwi kuendesha kesi. wao wapeleleze, walete ushahidi mzuru wapeleke kwa dpp/attorney general office ili ashitaki, ndio kazi yake hiyo. tatizo pccb wapo kisiasa zaidi.
 
Ninaungana na wachangiaji wote wanaosema PCCB hawapaswi kuendesha kesi kama inyoendelea kufanyika katika jeshi la polisi.

japo mabadiliko siyo makubwa langalau kidogo kwa upande wa polisi unaona polisi anabakia kuwa shahidi nakitengo cha prosecution kinaendela kufanya kazi ya uendeshaji kesi.

huu ni mfimo wa common legal system. lakini hdi hivi naandika hapa bado jambo hili halijafanyiwa kazi 100% kwani tunaona PCCB wanaendelea kuendesha kesi wenyewe .

mfano wa hivi karibuni, mkurugenzi wa halmadhauri ya mikindani na halmashauri ya mufindi wapefikishwa mahakamanai na PCCB, na mwansheria wa PCCB ndiye aliyesoma charge sheet(hati ya mashtaka).

kwa hiyo imebaki kuwa changamoto.
 
Back
Top Bottom