Kwanini tamisemi hawajawapangia vituo vya kazi za ualimu wahitimu wa st john-dodoma campus..?

Joined
Mar 5, 2014
Posts
7
Reaction score
0
Takribani siku tatu zimepita tokea post za ualimu zitangazwe na tamisemi,ila kinachonishangaza ni kutokupangiwa vituo vya kazi wanafunzi waliosomea shahada ya sana na ualimu katika chuo cha St John University of Tanzania(Dodoma campus) .Na tokea watangaze hizo post hawajatoa tamko lolote linalo huasia na kutokuwapangia wahitimu hao vituo vya kazi.

Je hili limechangiwa na nini? ingekua na vyuo vingine hawajapangiwa wa masomo hayo ingekua kawaida ila kwanini iwe chuo kimoja tu?

Je Tamisemi wanamakusudi gani kutokutoa tamko lolote linalohusiana na tatizo hilo?

Je ni st John tu au kuna chuo kingine ambapo wahitimu wa sana na ualimu hawajapangiwa vituo vya kazi?

Ndugu zangu mwenye taarifa zozote zinazohusiana na taarifa hizi unaweza nipa habari ili nielewe chanzo cha kutokupangiwa kwa wahitimi wa St john-capus ya Dodoma.

INAWEZEKANA, TIMIZA WAJIBU WAKO!
Asanteni:canada::A S 103::A S 103:
 
Ndugu yangu mi ni mojawapo wa wahitimu wa sjut-dom(ualimu),tunashangaa majina yetu hayapo ya watu 300+,tunawashangaa sana tamisemi mbona wenzetu wa sjut-dsm wamepangiwa?au ni vyuo viwili tofauti?Tamisemi lijibuni hili mapema.
 
Ndugu yangu mi ni mojawapo wa wahitimu wa sjut-dom(ualimu),tunashangaa majina yetu hayapo ya watu 300+,tunawashangaa sana tamisemi mbona wenzetu wa sjut-dsm wamepangiwa?au ni vyuo viwili tofauti?Tamisemi lijibuni hili mapema.
poleni sana. Kama una ndugu yako yupo Dar es salaam muombe akafuatilie wizara ya Elimu, huenda kuna tatizo ambalo labda hawajaligundua kama hamkupangiwa ajira. Au kama una ndugu Dodoma (m) muombe akaulizie pale Tamisemi.
 
Asante ndugu,cku zote nlkuwa tu nasikia tamisemi hawapo makini hata kwa masuala madogo kama hawa sasa nmeamini.
 
Labda wamegundua ni vilaza.
 
nawahakikishia mnaoangiwa baada ya wiki hii,nina uhakika na ilo.
 
naskia uongozi wenu wa chuo ndo uliochelewa kupeleka majina wizaran...majina yalifika wakati post zishapangwa...but mtaajiriwa tu!.
 
poleni sana,naamini second sellectiön mtakuwepo kwa sababu ifuatayo,mwaka 2012 wanafunz wote tuliomaliza mwenge university hatukupangiwa vituo vya kaz kwa sababu chuo hakikupeleka majina tamisemi kwa wakati husika,wachache waliopata awamu ya kwanza waliandika barua wizara ya elimu bila kutegemea chuo kupeleka majina,awamu ya pili wote tulipata baada ya tamisemi kupata majina yetu,msijal Mungu yupo nanyi,mtapata ajira.
 
sio nyie tu hata baadhi ya walimu wa diploma hawakupangiwa nahisi tamisemi walipanga kulingana na bajeti yao,ila MSikate tamaa kaeni mkao wa kula second selection inakuja soon.
 
pole zenu....!

ila mpaka sasa sidhani kama kutakuwa na uwezekano wa kupangiwa shule zenye uafadhali wa huduma za jamii km maji, umeme na hospitali...

hawa wenzetu watakuja bwagwa sehemu zenye utata mwingi sana!
 
Hakijaisajili program hiyo tcu. Lkn nch yetu ina ardhi ya kutosha. Na kama una elimu ya chuo kikuu basi kalime utatoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…